MAONI:Serikali ilivyoshughulikia vurugu za kanisa la EFATHA vs UAMSHO

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
mimi sina kipaji cha uchambuzi au upembuzi yakinifu hivyo ningependa kusikia maoni ya great thinkers juu ya suala hili.
Je tunaonaje responce ya serikali dhidi ya chokochoko ya vikundi hivi?
Je kuna usawa katika kudhibiti ukiukwaji wa sheria uliofanywa na vikundi hivi?
Je intelijensia ya polisi imefanikiwa kujua malengo ya vikundi hivi?

Naomba tuwe fair na huru kama ilivyo tabia yetu.tusionee dini au chama flani
 
Ni jambo la kusikitisha sana kama serikali inashindwa kufanya maamuzi kuhusiana na suala hilo. Wakristo wanapofanya kosa fulan ama wasifanye wanaandamwa na hao wanaoitwa vyombo vya usalama, ninashindwa kuelewa mwisho wake utakuwa nini! Je itakuwa ni vita ya kidini imeshaanza au maana yake nini serikali kulifumbia macho jambo nzito kama hilo?
 
mbona kama unataka kuchanganya mtindi na soda?
huwezi fananisha watu wanaodai kaeneo kadogo kama kale ka Mang'ula na wale wanaodai jiardhi kubwa la visiwa vya Unguja na Pemba.
Mathalani tujenge fikra kuwa makundi haya yote mawili yamekiuka sheria na yawe yanakabiliwa na shtaka au mashtaka. Ni wazi ndugu zangu wa UAMSHO wakashtakiwa kwa kosa la uhaini wakati wale wa pale EFATHA wakastakiwa kwa kosa la madai.
Umehoji kuhusu uhalali wa ushughulikiaji wa vurugu zilizotoke. Mkuu labda rudi nyuma kidogo na uangalie madai ya vikundi hivi viwili. Efatha wao wanadai ardhi waliyokwisha inunua na vielelezo stahiki wanavyo,vilevile mtu wanayemshutumu ni Afro Plus.
Kwa upande mwingine UAMSHO wao kidogo ni ngumu kujua nini wanataka. Kwanza ni kikundi chenye usajili wa kidini, (hii ni kwa mujibu wa hotuba za Shein na Kikwete) ambacho kinadai uhuru wa Zanzibar(kuvunjwa kwa Muungano) au kwa lugha nyepesi ni kujitenga kutoka katika JMT.
Kwa haraka tu utaona miono na malengo tofauti baina ya madai, uhalali wa,kudai na jinsi ya kudai.
 
Back
Top Bottom