Maoni: Rais JK Tafadhali Hutubia Taifa Kabla Ya Sensa...!

JK hawezi kuhutubia Taifa. Nani atamsikiliza? Labda aanze na sentensi hii: Dodoso la sensa tumelibadilisha ghafla. Tumeweka kipengele cha dini. Lakini ajue huo utakuwa mwanzo tu wa vita vya kidini nchini. Kwa ujumla wake suala la dini ni dogo sana hapa. Watu wanagoma kuhesabiwa kwa kuchoka utawala uliopo uliojaa rushwa na dhuruma. Tumekosa dira kama Taifa, tumekosa uongozi wa nchi. Nchi imeendelea kutotawalika. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa nchi.
 
Liwalo na liwe mtahesabiwa hata kwa mabomu ya machozi na risasi za moto na kwa wanao jidai kuonyea ongea mabwepande inawasubiri...
 
JK hawezi kuhutubia Taifa. Nani atamsikiliza? Labda aanze na sentensi hii: Dodoso la sensa tumelibadilisha ghafla. Tumeweka kipengele cha dini. Lakini ajue huo utakuwa mwanzo tu wa vita vya kidini nchini. Kwa ujumla wake suala la dini ni dogo sana hapa. Watu wanagoma kuhesabiwa kwa kuchoka utawala uliopo uliojaa rushwa na dhuruma. Tumekosa dira kama Taifa, tumekosa uongozi wa nchi. Nchi imeendelea kutotawalika.
Mkuu
Umeongea pwenti tupu!
Tatizo ni Utawala irresponsible.
 
Liwalo na liwe mtahesabiwa hata kwa mabomu ya machozi na risasi za moto na kwa wanao jidai kuonyea ongea mabwepande inawasubiri...
Tunahitaji sana rais Dikteta kwa sasa, lakini udikteta wa hivi hauna nafasi!
 
Tunahitaji sana rais Dikteta kwa sasa, lakini udikteta wa hivi hauna nafasi!

Dictatorship is an outcome of incompetent leadership. Kuna haja ya kuonesha dira ya utatuzi wa matatizo ya watu. Ukifanikiwa kwa hilo hakuna haja ya uongozi wa kiimla.
 
anajua hakuna atakayemsikiliza so ni kupoteza muda tu kuhutubia ndo maana anaona bora amalize kufnga sita swala halafu aende zake ethiopia kwenye msiba
 
Dictatorship is an outcome of incompetent leadership. Kuna haja ya kuonesha dira ya utatuzi wa matatizo ya watu. Ukifanikiwa kwa hilo hakuna haja ya uongozi wa kiimla.
Mkuu
Kama unayo Dira hiyo au Road-Map waweza ukatusaidia? maana tunaelekea kuangamia sasa!
Waliokasimishwa madaraka na nguvu za kisheria wako likizo...wanakunywa whisky Bahamas
 
Bora hasitoe hotuba maana atasema hajui kwa nini watu wanagomea sensa na ana washangaa!
 
Mkuu
Kama unayo Dira hiyo au Road-Map waweza ukatusaidia? maana tunaelekea kuangamia sasa!
Waliokasimishwa madaraka na nguvu za kisheria wako likizo...wanakunywa whisky Bahamas

Wanasema giza likizidi asubuhi inakaribia,tusichoke mkuu tuendeleze libeneke,kitaeleweka tu!
 
Bora hasitoe hotuba maana atasema hajui kwa nini watu wanagomea sensa na ana washangaa!
Umuhimu wa kutoa hotuba yenye ukali (km ile ya Mbayuwayu) hawezi kuukwepa ni muhimu mno(deadly important). Bila hivyo anaweza akasababisha watu wamwamini sana Mnyika na kauli yake maarufu aliyitoa huko bungeni, na ikamgharimu kutolewa nje ya BUNGE.
 
Mkuu
Kama unayo Dira hiyo au Road-Map waweza ukatusaidia? maana tunaelekea kuangamia sasa!
Waliokasimishwa madaraka na nguvu za kisheria wako likizo...wanakunywa whisky Bahamas

Mkuu umesahau Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025 Yenye lengo kuu la kuwa na watanzania wenye maendeleo endelevu?
 
JMK anasubiri zoezi liende vibaya kisha aseme NI WAPINZANI. Atawananga, atawatishia kuwafunga. Ataongea haya yote tarehe 2/9/2012, katika "Hotuba ya mwisho wa mwezi wa 9!" Nachooona ni less creativity. UDHAIFU MTUPU! Kama kweli anaweza, aongee na vyombo vya habari, pamoja na mambo mengine, issue ya Malawi. Afafanue wale "wapinzani" wanaoutaka urais, kupitia sala Malawi ni kina nani hasa, kama siyo wana CCM wenzake!
 
Mwenendo wa nchi yetu kwa sasa ni alarming, kama ni geji ya fuel kwa sasa iko under Empty!.

Zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo limebakiza siku mbili tu tokea leo limekumbwa na majaribu mengi, ambapo kwa mwenye umakini yeyote anatabiri waziwazi kuwa ufanisi wake utaathiriwa kwa kiasi kikubwa...Kwa Taifa makini na linalomaanisha maendeleo ya kweli kwa raia wake, huu ni msiba wa Kitaifa!
Huku mitaani tunakoishi hali ni mbaya sana kuhusu zoezi hilo la sensa. Ni watu wengi mno wanaoapa kutohesabiwa, sio tu kwa sababu za dini na Posho, bali pia kwa kuona serikali yetu ni ya wachache wanaoifaidi!

Sensa tokea zamani imekuwa ni moja kati ya nguzo zilizokuwa zinatuunganisha Watanzania wa makabila dini na rangi zote.

Kuna matukio mengine mengi ya kitaifa km Zoezi la Katiba, vitambulisho, uchaguzi mkuu 2015, ambapo tusipokuwa makini yanaweza kutumiwa na wasioitakia mema nchi kama chanzo cha kusambaratisha nchi, na tukafutika kwenye ramani ya dunia.

Ninachoweza kusema ni kwamba mambo yote haya yameletelezwa(gradual instil) na ukimya wa serikali ya JK kwenye matukio makubwa yanayoimaliza nchi yetu. Uzalendo wa wananchi umeporomoka, na hawaoni tena sababu ya kuheshimu Mamlaka.
Kutochukua, au kuchelewesha mno hatua za kinidhamu(stern measures) ndiko kunakosababisha wananchi kufikia maamuzi ya kuingiza misimamo yao kuvuruga serikali kama hili la sensa.

Rais angekuwa mkali kwenye mambo kama ya akina Jairo, Ngeleja, Mhando na wenzie, Mramba, Mzee wa vijisenti, mar.Balali, na kwenye skendo zote za ufisadi zilizoikumba nchi9ambazo ni nyingi mno), angalau kungekuwa na nidhamu(japo hata ya woga).

Namwomba Rais wangu JK ahutubie Taifa haraka iwezekanavyo ili kuweka msimamo mkali wa kitaifa, akiongelea suala la sensa 'parse' bila kuingiza mambo mengine yoyote, wala kuwananga WAPINZANI...

Hotuba hii haiwezi kuwabadilisha wenye misimamo hasi na sensa 'overnight', lakini inaweza kuwa stepping stone ya misimamo mingine itakayosaidia nchi hii huko mbele ya safari.

Imagine nimesoma mahali, imefikia hata wenyeviti wa mitaa na vijiji wanawagomesha wananchi kuhesabiwa!!(My hairs)...tuko wapi kama Taifa?
Wazee hakuna kwenye nchi yetu?...kwanini wana'underestimate hasara ya wrong data ya Population ya Watanzania?

Taifa kwa mara nyingine linakula hasara ya ajabu kwa fedha zilizotengwa kwa zoezi hili kupotea bila kudeliver kile kilichotarajiwa.
..i can smell census-gate soon to be on pipe-line!
Naamini wasaidizi wa Rais mnaosoma hapa mtamweleza na kumshauri Rais haraka.

Mungu Ibariki Tanzania.

huko kwenye red, nadhani alikusikia na walikusikia! At least!!!?
 
Back
Top Bottom