Maoni na Mtazamo wangu

mwikumwiku

Senior Member
Jul 15, 2011
153
35
Mapema leo asubuhi nilipost thread kuhusiana na mtazamo wangu juu ya namna ambavyo mchakato wa mjadala wa muswada Wa mapitio ya katiba ulivyotekwa na kuathiriwa na baadhi ya watu "elites" kwa kisingizio kwamba wanatuwakilisha wananchi. Aidha, nilijaribu kutaadharisha kuwa michakato ya kutunga katiba katika nchi nyingi imeathiriwa na kuondoa maana baada ya michakato hiyo kutekwa na "elites" na mwisho wa siku kutunga katiba ya "elites" badala ya wananchi waliowengi.

Leo hii hii kabla ya jua kuzama tunaanza kuona ni namna gani "elites" kwa kutumia weledi wao wanataka kutuondole au kuingilia haki yetu ya kupata katiba mpya tunayoitaka. Kitendo cha baadhi ya "ellites" wanasiasa' kutaka ku-frustrate mchakato kuweka utaratibu utakaotupatia nafasi sisi walala hoi kushiriki kutunga katiba tunayoitaka sidhani kama wanatutendea haki!

My Take
tuachieni sisi wananchi tuamue katiba tunayoitaka. ni vema Waheshimiwa wabunge wakafahamu kuwa sisi tunawaona wao ndio kikwazo cha kupatikana katiba mpya! Kwa mfano jioni hii mmetuvuruga na mmetutlekeza! Raiti wote mngeamua kubaki ndani ya bunge na kusimamia hoja zote za msingi kama zilivyowasilishwa na mheshimiwa Lisu naamini mngefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko hivyo mlivyofanya! Mbona asubuhi mmesimamia mbambo mengi na yakaingizwa kwenye sheria ya manunuzi! Kwanini msingefanya hivyo hivyo na kwa muswada huu. Kwa hakika mmetuvuruga na mmetuterekeza!
 
tatizo maagamba wanataka kuandaa rasimu zao kwa nguvu yeyote ile,huyu bibi kiroboto alikua hataki hata kusikia kitu kinachoitwa muongozo na kuwabeba magamba wenzake
 
That is all about silly Tanzanaia politics. Go and ask JK to deal with the mayhem in Mbeya and Arusha. It is his creation. Like all other african leaders, he has tasted honey, and found honey to be sweet. So he wants to change the " peoples constitution" to create more powers for himself so he could rule Tanazania forever.
 
Mtoa hoja una mawazo mazuri sana lakini hujui namna ambavyo katiba mpya ni muhumi kwa msingi kuwa inaweza ikamaliza ujambazi wa CCM au kuendeleza ujambazi wao...Hivi unafanananisha mswada wa manunuzi na katiba? Hawa jamaa kwa vyovyote vile wamejiandaa kutupelekesha.Kwa mtu mwenye akili timamu hata useme wabunge wa CDM na NCCR waliotoka wangebaki hakuna chochote kingefanyika....Ninachoona CCM wamejipanga katika hili kutumia nguvu zote za wasomi(kumbuka maneno ya Prof Palamagamba kabudi) jana,watu wengine,na baadhi ya wabunge wa CUF leo...kuna dalili tosha zinazoonyesha kuwa CCM wamejipanga hata kwa kumwaga damu ili mradi watimize matakwa yao..Neno moja ninalosema,CCM watatumia kila njia,lakini mwisho haki itashinda..kuna siku watu watawaelewa CDM na wabunge wachache wa NCCR....
 
Mimi pia namuunga mkono mtoa hoja,ishu hapa ni kwamba wabunge waliosusa wangebaki kutetea kile wanachokiamini ndani ya bunge na wananchi wazidi kupata ufafanuzi wa kile wanachokipinga.kususa ni ishu za kike na watu makini tunaona wamepotoka.kesho warudi bungeni wapambane bungeni mpaka hatua ya mwisho.Kususia sio suluhisho
 
Mimi pia namuunga mkono mtoa hoja,ishu hapa ni kwamba wabunge waliosusa wangebaki kutetea kile wanachokiamini ndani ya bunge na wananchi wazidi kupata ufafanuzi wa kile wanachokipinga.kususa ni ishu za kike na watu makini tunaona wamepotoka.kesho warudi bungeni wapambane bungeni mpaka hatua ya mwisho.Kususia sio suluhisho

wewe na mtoa hoja maskini hamuelewi mnachokisema au mnataka kupotosha kwa makusudi? walichofanya wapinzani ni kuelezea ubaya wa mswada,mapendekezo yao na zaidi hoja ya kutaka msada usomwe kwa mara ya kwanza ili urudi tena kwa wananchi watoe maoni yao totauti na kama walivyong'ang'ania CCM na CCM +CCM D (Mrema) kwani kwa kusomwa mara ya pili basi wananchi hawawezi tena kutoa maoni yao. kwa hatua hiyo wapinzani ililazimu kunawa mikono ili wasishiriki dhambi hiyo kwa kutoka nje. aidha kumbuka hata miongozo walijaribu kuomba bila mafanikio.sasa ulitaka wapambane vipi kwa ngumi nini? acha unafiki ama ujinga unapotoa hoja kwenye jambo muhimu kama hili.
 
Mimi pia namuunga mkono mtoa hoja,ishu hapa ni kwamba wabunge waliosusa wangebaki kutetea kile wanachokiamini ndani ya bunge na wananchi wazidi kupata ufafanuzi wa kile wanachokipinga.kususa ni ishu za kike na watu makini tunaona wamepotoka.kesho warudi bungeni wapambane bungeni mpaka hatua ya mwisho.Kususia sio suluhisho

Unapoona jambo ni tatizo kwako,zipo njia za kuliepuka,unaweza kunyamaza kabisa,au kuondoka au vinginevyo,vipi kama wangeamua kuporomosha matusi pengine hata ya nguoni,picha si mbaya?Kimya pia ni jibu,hata kuondoka ni jibu
 
Inaonyesha watu tuna matatizo ya kusahau, kikao cha kwanza cha bunge hili la kumi cdm walisusia hotuba ya rais na wakabezwa sana lakini ile ilisaidia kupeleka ujumbe kwa watawala wetu. Hii waliofanya leo itawapelekea ujumbe watawala wetu hilo halina ubishi. Ni seme hivi ikitokea machafuko hapa nchini kuhusu uundwaji wa katiba mpya basi atakaye sababisha ni spika wetu mama makinda tena kwa kukosa busara kidogo tu.
 
Back
Top Bottom