Maoni kwa Michuzi yamepungua sana nadhani ni Jamiiforums...

Jamaa ni moja wa mafisadi, kwani anasafiri na JK kwa kodi ya watanzania...

Vile vile hatoagi comment zinazoponda issue za serikali..

Michuzi lazima itafungwa kwa kukosa wasomaji kwani Slaa akishinda hana kazi tena..
 
hIYO NI KWELI KWANI MICHUZI SASA HIVI NI MIONGONI MWA MAKADA WA CCM INGAWA HAKUTANGAZA RASIMI HATUMLAUMU ANAPALILIA UGA WAKE TUNAMLAUMU KWA KITU KIMOJA KUTTOTUARIFU KUHUSU POST YAKE MPYA MUNGU IBARIKI TANZANIA
nadhani hapo ndipo tunapoona tofauti ya blog na forum
 
Mwache huyo michuzi azidi kupanga picha za jk na vilema kwa kuwadhihaki kana kwamba leo ndo anakumbuka kutatua matatizo yake..
Hatutaki tena raisi anayekenua 365 days na kusafiri kama rubani au air hostess!!..akawe raisi bagamoyo hata milele!!
Halafu imagine raisi anasaidia kilema mmoja mmoja inashangaza sana.. Badala ya kuweka sera nzuri za kuwasaidia wote yeye anagawa bajaji kwa mmoja wawili, ni ajabu sana.
 
Thread nyingine bana.. \

wasted
Hukulazimishwa kuchangia hapa. kama huna sera kaa kimya. Kila wazo lina maana yake hata kama hukubaliani nalo ndio maana nchi kama USA iko mbali sana kwa sababu hawadharau maoni hata ya maadui zao wanayafanyia kazi.
 
Hakuna kitu kwa michuzi. ameingia kwenye mtandao na habari zake nyingi ni za kuwasifu mafisadi. wadau wameamua kuigomea
 
Heeh! hivi issamichuzi blog bado ina-exist? mie sijatembelea siku nyingi kweli maana ilifika mahali nikawa kila nikifungua naona kichefuchefu na hizo bendera zake za kijani. Anyway, ni maoni tu.
 
Alishindwa kusoma alama za nyakati. Watembeleaji wengi wa blog yake ni watu wenye mtazamo wa kimaendeleo zaidi, yeye ameruhusu mafisadi kuinajisi blog yake na kumfanya mtumwa kwa kuifanya blog ya CCM.
 
Kweli kabisa sikumbuki ni lini nimecoment michuzi the last time! Si hilo tu magazeti yoye yenye mlengo wa kukitetea chama cha mapinduzi na yenyewe yamepoteza mvuto vile vile! CCM imegeuka kero na karaha kubwa sana kwa watanzania!
Pengine tatizo lipo hapo! UCCM na UCHADEMA (Michuzi vs Jamii Forums) kwani hata ile hadhi na postings za maana ndani ya JF zimeanza kuyayuka.
 
Nilitembelea kule nikakuta posts zingine hazina comments kabisaaa.
nadhani watu wameona wanalishwa upupu na jamaa keshapoteza soko. subiri baada ya uchaguzi ile globu itakosa watembeleaji na yeye atakuwa miongoni mwao. RUSHWA mbaya sana

Atafunga tu blog
 
tulimtumie email za kumuonya hakusikia, kila siku ni habari za ccm tuuuuu, aaah! mwache aende bwana wana ccm wenzake watamtembelea
 
Michuzi anajulikana yuko bias kwani habari ambayo hai support CCM haweki kabisa kwenye blog yake. Kwanza yeye anajulikana kabisa ni CCM na huwa mara nyingine anavaa hata zile T-shirt zao na Kofia. Kwa hiyo hajifichi. Tulikimbia blog yake baada ya kutoripoti hata mkutano mmoja wa DR. Slaa kwenye blog yake
 
Ni kweli Michuzi analalia CCM kama JF inavyolalia CHADEMA.

Ama kweli nyani haoni......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom