Maoni kuhusiana na miswaada ya sheria april 2012

tembeleh2

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
765
165
Kuna miswaada ya sheria miwili 1)muswaada wa sheria ya taasisi za utafiti ya mwaka 2011 na 2)Muswaada wa sheria ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2011. miswaada hii inatarajiwa kujadiliwa kwenye bunge la april. Taarifa hii imetolewa kwenye blog ya michuzi kwa ajili ya vyombo vya habari ikiwahimiza wananchi na wadau wote kwa ujumla washiriki kuboresha miswaada hii. Taarifa hii haijaeleza wananchi wanatakiwa washirikije?. Wana JF ni kweli watu hawa wako makini na swala hili? ni kweli wanahitaji michango ya wananchi na wadau wengine?
 
Tuwekee hapa hiyo miswada tuione, tuchangie. kwa kuwa watunga sheria na watunga sera wanapita humu basi watachukua maoni yetu hata kama hawata acknowledge.
 
Kuna miswaada ya sheria miwili 1)muswaada wa sheria ya taasisi za utafiti ya mwaka 2011 na 2)Muswaada wa sheria ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2011. miswaada hii inatarajiwa kujadiliwa kwenye bunge la april. Taarifa hii imetolewa kwenye blog ya michuzi kwa ajili ya vyombo vya habari ikiwahimiza wananchi na wadau wote kwa ujumla washiriki kuboresha miswaada hii. Taarifa hii haijaeleza wananchi wanatakiwa washirikije?. Wana JF ni kweli watu hawa wako makini na swala hili? ni kweli wanahitaji michango ya wananchi na wadau wengine?

Usiri huu una maana kuwa kuna vested interests kwenye miswada hiyo ndio maana wanaificha wananchi wasiione. Bungeni kuna walalaji/awsinziaji wa CCM upinzani ukilala tu itapishwa miswada ya na kuwa sheria za ajabu.
 
wanatakiwa waitoe mapema wananchi na wadau mbali mbali waipitie mapema na kutoa maoni yao sasa taarifa inatoka wakati wakati huu ambao imebaki wiki moja tu bunge kuanza huo muda wa kuchangia uko wapi waache ujinga
 
sometimes inaumiza kichwa bil sababu, kama serikali na mahakama hazifuati sheria mwananchi ataanzia wapi kuzifuata hizo sheria, inafikia stage sioni umuhimu wa hizi sheria ndogo ndogo, ni bora kujikita kwenye katiba mpya labda italeta mabadiliko. Mfano mzuri ni hii sheria ya ardhi ya mwaka 2007, kila mara when it comes to government interest huwa inapindishwa na sheria ya mwaka 1977 kuchukua mkondo wake, does it mean sheria hii iliwekwa kuwalinda watu wachache tu? Mfano serikali ilipotaka kuchukua eneo la kariakoo gerezani ilitumika sheria ya 1997, ilhali ya 2007 tayari ilikuwa ishapitishwa. Wanawagwaya hao walionunua nyumba za obey, masaki na upanga wakijua sheria ya 2007 itatumika na serikali haitokuwa na uwezo wa kuwalipa! Tanzania ya leo katiba mpya ndio solution!
 
Back
Top Bottom