Maoni katiba mpya kulikoni???

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Tume inayokusanya na kuratibu maoni juu ya kuandika katiba mpya imeshaanza kazi chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba! Nafikiri imeshaanza kazi mikoa ya kusini, nimekuwa nikifuatilia kwenye vyombo vya habari hususani magazeti ili kuona wananchi wanashiriki vipi kutoa maoni, mahudhurio, na wanajikita hasa kwenye mambo gani hasa amabayo wangependa yaingizwe kwenye katiba mpya!Kwa mshangao habari hizi hazipewi kipaumbele na vyombo vya habari na hata hapa JF Sijaona watu wakizungumzia namna wananchi wenzetu wanavoipokea tume na utoaji wao wa maoni!!
Sasa sijui ile sheria iliyounda tume inakataza vyombo vya habari kutangaza habari za tume maoni ya wananchi?? Naombeni yeyote mwenye taarifa kuhusu mwenendo wa tume hii ya katiba mpya atupenyezee tujue watanzania wenzetu wanajadili nini??
 
Back
Top Bottom