Maoni Binafsi: Ujio wa Bwana James Ole Millya ndani ya CHADEMA

Mkuu Laptan,

Nakubaliana na hoja ... Mwalimu Nyerere aliposema upinzani utatoka CCM alimaanisha kwamba watakapotofautiana kiitikadi na mtazamo kuhusu approach ya maswala mbali mbali. Sasa wengi wa wanaoondoka CCM baada ya kukosa uongozi sio kwamba kinachowatofautisha ni Itikadi, NO, bali ni ulaji ndo unakuwa umeleta shida.

Hapo kwenye mfano wa Kenya naomba tuweke rekodi sawa: KANU ilisambaratika baada ya Mzee Moi kumteua Kenyatta kuwa mgombea urais na kuwaruka wengine ambao walikuwa wanategemea. Waliondoka ni pamoja na huyo Mzee Saitoti (Prof) pamoja na akina Rutto na Odinga, wakaenda kuanzisha Rainbow Coalition (hii nayo ni mfano wa papo kwa papo) ambayo haikudumu kwa sababu hawa watu walikutana ghafla hakuna cha itikadi wala nini, wameona kwamba ulaji anapewa mwingine wakaamua kutimka.

NARC ilipotwaa madaraka, ndoa ya hao wana siasa ilikuwa ya muda mfupi, ndipo akina Odinga, Kalonzo, Rutto, Balala na wengineo walipojitenga na kuanzisha ODM. Bado hao watu walikuwa na itikadi tofauti na wote wanataka ulaji tu na si vinginevyo. Kalonzo Musyoka alikuwa na matarajio makubwa sana, lakini alipoona kwamba hawezi kupata tiketi ya kugombea Urais akaamua kujitenga.

Kwa hiyo hoja yangu iko pale pale kwamba haya mambo ya papo kwa papo ni hatari zaidi maana huwezi kujua hidden agenda ya mhusika.

Keil,

Tahadhari ni jambo la muhimu.Ndiyo maana kwenye hoja yangu ya jana niksizitiza juu ya chama kuandaa darasa la itikadi.Hata Benno malisa tunamkaribisha sana>Hata waziri mkuu aliyejiuzulu anaweza kuwa accomodated na kumpitisha jando ya kisiasa ya CHADEMA

Naendelea kuandika niliyoandika jana muda mfupi baada ya Millya kuchukua uamuzi.

Karibu CHADEMA Millya.Njoo tupige kazi kamanda.......

Sitakuwa cynic ku-question motive yako ya kujiunga na CHADEMA kama ambavyo imekuwa ikisemekana wewe ni mmoja wa watu katika kambi fulani ndani ya chama mwenye ambition kali za kuukwa Urais 2015.Sita-doubt motive yako kuwa ni mkakati wa kuingia ndani na kupata mwanya wa kuihujumu Chadema.

Sitafikiria umejiunga kwa hasira kwa kuwa hukupitishwa kwenye uchaguzi wa EALA.Ni kweli mara nyingi huwa sipendi watu wahame vyama kwa hisiasa kwani hasira kutokana na kukosa objectivity katika maamuzi

Badala yake nitaendelea kutoa maoni kwa chama changu sasa tujiandae kupokea watu na darasa la kutosha la itikadi.Tujiandae sasa kuigeuza fan base kuwa loyal base.

Vijana wote ambao ni wapambanaji wa kweli karibuni CHADEMA.Njooni tujenge chama.....Millya usikubali kuwaacha wenzako nyuma,ndani ya chama chenu hoja haziangaliwi tena.Huko ni itikadi za matusi na ghiliba tu.

Should we continue to vote the same people who have presided over the decline in quality of life in Tanazania for the last 50 years?

Shamefully, these people are openly canvassing a desire to rule Tanzania forever(comment kutoka kwa katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM/msemaji wa CCM)

Tanzanians must reject these ‘political zoo keepers' and stop them in their tracks. And stop them now. During the last 50 years, they have almost transformed Tanzania into the proverbial animal farm where sycophants dominate both the airwaves and print media.

Enough of CCM, Enough of them! The CHADEMA movement is poised to restore confidence in our people. We are providing the platform that would enable the country break out of the present stranglehold. We in the CHADEMA see and share the plight of the suffering citizens. We offer a political platform whose imperative is to rescue Tanzania and reposition it for greater economic development and social well being. As such the first order of business for the CHADEMA-led government would be to secure Tanzania better and to manage it better. The priority will be to end the feeling of insecurity in the country.

The young people of this country deserve much better deal than what they have been getting. Unemployment, deprivation, poverty, hopelessness and insecurity are part and parcel of our young men and women today.

It is my firm belief that politics and democracy must be willing to provide answers to such fundamental societal issues as youth employment.

Wale wote wanaoamini katika dhamira hii ya chadema kwa nchi yetu watajiunga nasi ,watakuwa sehemu ya kusimamia dhamira hii na harakati za kufikia lengo hili.Vijana na wazee karibuni CHADEMA.CCM ilipoteza intergrity baada ya Mwl.Nyerere kutangulia mbele za haki
 
This was a keen observation. Chama kimekuwa na lazima kipate changamoto kama hizi. Hivyo kila mtu ndani ya CDM achukue tahadhari.
 
Huu ni uchambuzi nzuri sana. Ni matumaini yangu kuwa uongozi wa chadema ( mbowe na dr slaa) watapitia hii thread na kuifanyia kazi. Kimsingi huyu jamaa apokelewe kama mwanachama au mshabiki wa kawaida wa chadema. Apewe muda wa kuonyesha kweli yuko kwa ajili ya itikadi ya chadema.
 
Mbwa akija kupumzika nje ya bucha si kwamba hapendi mifupa,la hasha akipata mpenyo tu atafanya kweli,Milya ni pro EL hili haliitaji utabiri na ramri,hapa kuna mawili
1.Kasoma alama za nyakati za kuporomoka kwa EL na anataka kutoanguka nae.
2.Yawezekana ni mpango madhubuti wa El kupenyeza kimeta chake CDM ili kupunguza nguvu ya CDM.
CDM nadhani walishajifunza kwa Shibuda na wawe makini sana,shetani hata angetubu vipi hana nafasi mbinguni kwa alishakataliwa!
 
u r very bryt mkuu..mbowe hawezi kutuaminisha kile tunachofahamu..kuwa cdm si kuwa toy kwa kila kinachosemwa na viongozi..yeye kama anamuona msafi mi namuona si msafi..labda kama kuna ajenda.. cdm haihitaji watu kutoka ccm ili kukijenga..sababu hata tuliokuwa hatuna vyama sasa tunasapoti cdm..huyu ni askari mtiifu kwa lowasa..

tunaichukia ccm yote sababu ya ufisadi wa wenzao..kwani nape ana hatia gani..?mbona huwa tunamsema vibaya..ni sababu yupo ccm..millya hata kama hana tuhuma anaem backup amejaa tuhuma ambazo cdm wamekuwa wakizisema..cdm don make us fools..pliz..millya hajawahi kusimamia kile cdm inachoamini.. Angalau samwel sitta au nape nnauye..cdm inalewa umaarufu

Kwa maoni yako hata Dr. Slaa afukuzwe CDM kwakuwa alitokea CCM?, Mi nadhani usimhukumu Mbowe kiasi hicho, ni vema kukawa na umakini katkika kupokea wanachama wapya kama Milya, na alichosema Mbowe kama binadamu ndicho anachoamini na kumbuka maamuzi si ya kwake kama Mbowe mwisho wa siku taratibu za chama lazima zifuatwe.

Millya tumpe nafasi, tumpime na tukimuona hafai tutamshibuda na taratibu atajifia. Unapohitimisha kuwa labda Sitta na Nnauye, hao ndiyo wanafiki wakubwa, umesahau CCJ? lakini nao wakitaka kuja tutawatakasa, suala la CDM kulewa umaarufu naona huo ni wivu wa kijinga tena wakubomoa na si kujenga, CDM ipo kwenye mioyo ya watu kutokana na yale wanayojipambanunua nayo wakiongozwa na Makamanda wake.

Mbowe ameshakuwa na mchasngo mkubwa kuliko unavyodhani wewe ambaye emerukia tu kwa kusukumwa na upepo
 
thanks for an analysis...Nadhani chama kina procedures , na codes of conduct...akipewa kazi atafanya kulingana na maelezo ya mkuu wake wa kazi...Mpk akahama C.C.M kuna mengi nyuma yake...time will tell
 
Maangalizo yako si ya kubezwa CDM halahala kijiti na macho.........wanaohamia wawekwe kwenye tanuri kwanza kabla ya kuanza kukitumikia CDM
 
Cha msingi mtu wowote apokelewe ila wasishirikishwe mambo ya ndani asije akawa mamluki 'spy' ila yeyote yule ruksa kujoin
Mwalimu aliposema upinzani wa kweli utatoka CCM usiyachukue maneno hayo kwa uzito Mwepesi Kwa kuamin kirahisi hivyo CHADEMA itakua Chali Kabla ya 2015
 
Wahenga husema, "ngoma ikilia sana, mwisho wake itapasuka". CDM sasa hivi, ngoma yao inavuma kila kijiji hapa Tanzania. Na kila mTanzania sasa hivi anatamani kuingia ngomani kucheza. CDM wasipokuwa makini, watawapokea fisi ngomani. Badala ya binadamu.

hii para toka kwa Collezione ni muhimu CDM wakaizingatia sana sana!!
 
Ukweli ni kwamba tucwe wajinga wala wapumbavu, milya na lowassa wana lao jambo kubwa ni kupunguza nguvu ya chadema ktk maeneo ya wafugaji hususan wamasai, halafu kuwa mpelelezi wa MOSSAD kwa fisa mkuu lowassa, na ictoshe huyu jamaa ni power monger i mean Milya futilieni alipokuwa Tumaini ya Iringa amehonga hadi kawa rais wa Chuo then alikuwa kibaraka wa ccm siku zote.

Ndugu zangu Chadema na wazalendo wote amabao tunalilia ukombozi wa tabaka la chini na tunao pinga rushwa kwa gharama zote huyu millya bado ni askari mtiifu wa Lowassa na shushushu wa ccm.

Tumwangalie mana Shibuda itakuwa cha mtoto, halafu ntawapeni habari zake kule kwao simanjiro hasa Orkesumet anako toka na wazazi wake.

Cku zote CDM kwa sasa mnawindwa kama pembe za faru zinavyotafutwa, cc tupiganie haki na hawa wenze2 ambao bado hawaja badilika mpango upo mbioni kwa sasa.

Wakubwa nawasilisha ila kwa millya mwacheni hakika ni mtalii tena CIA.
 
that is very true . anatakiwa afanyiwe uchunguzi nz uangalizi wa kina sana. asije akatugeuke kama SHIB....DA
 
Millya kama watanzania wengine anayohaki ya kuchagua chama anachoona kitamfaa. Inawezekana kweli alikuwa au ni mfuasi mtiifu wa Bw Lowassa lakini amejitafakari akagundua njia anayofuata si sahihi. Pia anaweza akawa bado anatumika na huyo jamaa. Hatutakuwa wanademokrasia wa kweli kama tutahoji kujiunga kwake chadema kwa kuangalia historia.

Na pia tukumbuke kuwa hata Lowasa mwenyewe ameanza kujikana na kubadili mwelekeo wa maisha yake kwenda makanisani kuwadanganya waumini na vijisenti vyake! Kwahiyo ni haki yake kwenda kanisani na kutoa anachofikiri ni msaada kwa waumini lakini waumini na viongozi wake ndiyo wenye jukumu la kupima uhalali wa misaada inayotolewa na huyu 'donor'.

Kama ni wana 'demo'krasia kweli na siyo 'theo'krasia Millya atapokelewa na atafunzwa kuachana na mienendo michafu na kufuata utakatifu unaosisitiza nguvu za umma..

Mimi nina imani na viongozi wa CDM kuwa wanao nguvu za kutosheleza kumvua huyu kijana utu wake wa awali uliojaa u-CCM na kumvalisha utu mpya uliojaa uzalendo na DEMOkrasia.

Millya Karibu kwenye chama cha waungwana ukijua kuwa hii ni nguvu ya umma na si CCJ...
 
Ah kwa nini tunawakumbatia wanaotoka kwenye uozo huyo kaitumikia ccm mpaka kupata cheo hicho si mchezo! Sasa kavurunda huko anakuj wapi? Cdm haina njaa ya wanachama mpotezeeni kama vipi
 
Ukiwa na akili timamu ukishika mkaa wa moto ukaonja joto lake nafikiri hutarudia tena kulishika. Chadema walishalishika kwa hiyo si wajinga wakalishika tena! Nafikiri wana karata ambayo wameishika kwa kupitia huyu aliyehama kambi ili baadaye waitumie kufunga goli la kisigino. We just wait and see how the card will be played. I EXPECT A KILLER BLOW.
 
Mtazamo mzuri sana.
Umefikiria vizuri na umeupa uwezo ubongo wako kudadavua.Hata mimi binafsi ninashaka sana na ujio wa huyu kijana ndani ya CDM.Labda mimi nadhani angetangaza kwanza kujiondoa kwenye mikono ya mtuhumiwa wa ufisadi.Naunga mkono hoja.Peeeeeeeeoooooooopleeeeeeeeeesssssssss.............................................
 
CHADEMA wawe makini hapo.
Afu ndo hiki kitu nilikua nasema kila siku. CHADEMA, wanatakiwa wawe na kanuni au katiba madhubuti kwa ajili ya kupokea member wapya. Na pasiwe na upendeleo katika hili.

Wasipokee watu tu, kama dampo. Wazingatie kanuni, katika mchakato wa kupokea watu (hasa waasi kutoka vyama vingie). La_sivyo inawezekana ikawa mtego, kwa chama kizima.

CCM imekufa, kwa sababu ya kupokea mamluki bila kufuata taratibu. Hatimaye hayo mamluki yanaingia kwenye chama kwa nia ya ufisadi, na mwisho wake kuhujumu chama.

Wahenga husema, "ngoma ikilia sana, mwisho wake itapasuka". CDM sasa hivi, ngoma yao inavuma kila kijiji hapa Tanzania. Na kila mTanzania sasa hivi anatamani kuingia ngomani kucheza. CDM wasipokuwa makini, watawapokea fisi ngomani. Badala ya binadamu.
CCM Haina mamluki mkuu, CCM wote wameoza
 
Back
Top Bottom