Maongezi vijana wa Tanzania; 96% ni pumba

Hivi unamkuta kijana anakariri majina ya wanaspoti wa ulaya ili mradi tu naye apate la kusema kijiweni. Nafikiri kuna haja kufikiri upya. Kama lengo c kuwa mchambuzi wa kulopwa ya nini wakati kuna meigi ya kujifunza
 
Mimi huwa nachukia hasa wanapokuwa wakizungumzia mpira,hasa wanaposema timu yangu imefungwa sina hamu au mwaka huu tunamsajili fulan,kama wana ubia na timu za Ulaya ilhali hata hawajulikani huko,na wakati mwngne ubishi huweza sababisha kugombana au kukosana na kutoleana matusi
 
Aiseee kweli mie mwenyewe nikipitia ktk hivyo vikundi huwa sipati kitu zaidi ya majungu.matusi.masengenyo na unywaji wa kugongea wa viroba(london) wa Kutisha
wako vizuri hao wanajua acc za
matajiri , na wasani wa bongo kama vile wanafanya kazi bank .
 
Nyinyi wazee wa zamani ndo mmetufikisha pabaya nchi hii.. Nchi imejaa ufisadi, nchi imejaa wala rushwa na wote mmesababisha nyiny wazee wa zamani.
Mnalalamika hatujiajiri wakati maofisi ya serikali yote mmejaa nyiny wazee, nyiny mbona hamjiajiri?
Mnasema sisi wavivu hatufany kazi si mlitulea nyiny wenyew, ina maaana mlitulea vibaya hapo awali.
Muache kutulaumu maisha yenyew mafupi haya kila mtu aishi anavyotaka
Ngoja nika bet kwanza mnanipotzea mda tu humu..
Charity begin @ home.
 
tena umkute kijana ndo amehitimu kile chuo chetu pendwa St. Josefu ama pale Muslim Univ. ndo utabaki mdomo wazi kwa pumba azitowazo
 
Ingekua na maana kubwa ungekuja na suluhisho. But kwa staili hii umeleta hoja alafu ina hang still inarudi kule ilikotoka... Amen
 
Vijana Pumba Production >>>>>Ligi za Mipira ya Ulaya, Muziki, Bongo Muvi na kuuza sembe ndo mnajivunia. BADILIKENI
 
Mourinho katua kwenye chama letu Man U. Utawasikia wazalisha pumba.
 
Vijana wengi wa kitanzania (Sehemu za miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya) 96% ya maongezi yao ni pumba tupu na vitu visivyowasadia katika kujikwamua kimaisha ikiwemo mpira wa ulaya (FA, EPL, UEFA n.k.), Wasanii wa bongo na skendo zao, namna mheshimiwa anavotumbua majipu. Ni ngumu kumkuta kijana wa miaka 18 - 35 akiongea vitu vya maana vya kujenga uchumi (binafsi, jamii na taifa) kwa muda unaozidi dakika 5 mfululizo bila kuchomeka Tusi.

Hivi interview/kazi huwa mnapataje aisee? na bomba la mafuta tumeambiwa linapita Tanzania kweli namna hii mtapata kazi kweli? au ndo watajaa wa kenya kama kawaida? (Mfano STRABAG, Nakumatt?)

NB: Fuatilia kwa wauza magazeti, vijana wengi hununua magazeti ya michezo, udaku n.k. na kuacha magazeti yenye fursa na habari za maana kwa mustakabali wa nchi. Sad!

Nyoka hawezi kuzaa paka
 
Nakuunga mkono hata humu wamejaa sana pitia tu kule MMU utawakuta wengi.!
 
Aisee umegusa "Ikulu" hawatachangia hapa kabisa.............................. Yaani ukikuta wanaongelea mpira wa Ulaya dah huwa nachoka kabisa yaani siwaelewi kiukweli yaani utasikia ooohhh kuna "Demu" japo hilo neno huwa silipendi sana kulisikia kaja kwa fulani, ooohh yule jamaa aliuwa na pesa sasa kafulia, yaani majungu full huwa nawachukia mpaka saa nyingine nawamwagia maji kwa makusudi nikipita na gari................. yaani umbea umbea tuuuu
Kuandika kote huko unataka tufaham kuwa unagari? Poa tumefaham! Ati hiyo gari ni aina gani mkuu?
 
Nadhani kuna tatizo katika akili za vijana waliozaliwa miaka ya themanini kwenda juu.......

Yaani unaweza ukadhanj ni wendawazimu......kwani ukiyatazama mambo wanayojishughulisha nayo ambayo yanachukua asilimia kubwa ya maisha yao ya kila siku na ukiutazama ulimwengu unavyokwenda kasi na mabadiliko kiuchumi basi unabaki kuwaonea huruma huku wao wakikushangaa wewe na kukuona ni mjinga kuliko.....

Kitu kingine kikubwa kinachowaangamiza vijana wa sasa ni ubishi....na kutokupenda kushaurika.....

Watu wazima wazima ni watu waliowahi kuliona jua kabla yako kwa hiyo wakati wewe bado upo kwenye viungo vya uzazi vya wazazi wako wao wanaishi duniani kwa hiyo wanayafahamu mengi ya dunia.....anapokuambia kuwa jambo fulani usifanye sio zuri kwako ni kwamba limemkuta yeye mwenyewe kwani hata yeye alikuwa kijana kama wewe au la kuna mtu wake wa karibu limemkuta....kwa hiyo si vyema kupuuzia ushauri au makatazo ya watu wazima.......

Vijana wa miaka hii hawana subira hata chembe kwenye mioyo yao.......wanataka kuyafanya mambo ya miaka kumi kwa siku moja tu......wanapenda starehe na utajiri wa haraka lakini hawapendi kufanya kazi na hata wakipata kazi hawana nidhamu ya matumizi ya pesa zao.....mwisho wanakuwa vibaka tu.......

Utandawazi nao umewafanya vijana waishi maisha ya kufikirika kuliko uhalisia wenyewe......

Kwa kifupi kuna tatizo kubwa kwa vijana wetu wa sasa.....

Na haohao bado wanaendelea kuzaliana...,kwhy hapo ni tatzo juu ya tatzo lnaongezeka!!
 
Back
Top Bottom