Maonesho ya kimataifa Dar, Sabasaba 2010....

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Maonesho ya kimataifa ya Dar, sabasaba 2010 yanategemewa kufunguliwa tarehe 28 Juni 2010. Nimekuwa na kawaida ya kutembelea maonesho hayo huko nyuma lakini nakatishwa tamaa na baadhi ya bidhaa zinazokuwepo pale. Yaani watu wengine wanaleta zile takataka za Kariakoo na kuweka kwenye mabanda yao. Hata hivyo kuna makampuni yanakuwa na vitu vya maana. Mfano, mwaka jana (2009) nilifurahishwa na banda la Wizara ya Maliasili na Utalii. Walikuwa na vitu vizuri sana kwa watu wengi ambao hawana nafasi ya kwenda mbugani. Wanyama wazuri sana waliletwa kwenye banda lao.

Naomba mwenye kuona kitu ambacho wadau tunaweza kufaidi atujuvye. Niko mbali kidogo lakini week ijayo lazima niwapeleke vijana wakashangae shangae kidogo!
 
Hakuna wadau wa Sabasaba watupe news na updates?

Kuna watu wa Magereza na JK huwa wanategeneza furniture nzuri sana. Ila niliwahi kufuatilia vituoni kwao sikupata kitu. Huwa pale sabasaba wanaleta vitu kwa ajili ya sifa?
 
Mwaka huu 77 itakuwa poa zaidi kwani kwa mara ya kwanza serikali na makampuni ya brazili yatashiriki..

Raisi wa brazili inacio lula da silva atakuwa gh na huenda hata ile team ikaja tena kutia hamasaa.....
 
Mkubwa napo pale pamekaa kifisadi zaidi, kupaki gari siajabu this yr ikawa laki 1 kuingiza ndani nje 20 elfu ukiingia ndani hakuna cha maana cha kununua msongomano mkubwa ka nini .....
 
Mkubwa napo pale pamekaa kifisadi zaidi, kupaki gari siajabu this yr ikawa laki 1 kuingiza ndani nje 20 elfu ukiingia ndani hakuna cha maana cha kununua msongomano mkubwa ka nini .....

Mimi nakerwa na takataka za kichina ila kuna baadhi ya vitu ni bomba sana. Hivi hizi furniture za JK na Magereza haziwezi kutegenezwa tukajaza maduka yetu yalijaa vumbi za Dubai na China?
 
Mwaka huu 77 itakuwa poa zaidi kwani kwa mara ya kwanza serikali na makampuni ya brazili yatashiriki..

Raisi wa brazili inacio lula da silva atakuwa gh na huenda hata ile team ikaja tena kutia hamasaa.....

khaa ina maana fainali ya WC2010 inaweza kuhamishiwa uwanja wa taifa siyo..duu
 
Ufunguzi wa maonesho ni leo. Hakuna mtu aliyehudhuria? Jamani i wengine tuko mikoani na tunataka kuja kumtembelea yule mama wa bia za Heneken!! Fidel, Xpin, Teamo, Bht etc.... jamani hiyo njia ya Kilwa road hamuijui au mna RB?
 
Poor preparations... mpaka leo vitambulisho kwa ajili ya washiriki bado havijatolewa... esxcuss... washiriki ni wengi sana. Leo ndo wameanza kuscrutinise maombi ya washiriki ili kuprocess vitambulisho, wengine hata picha hawajapigwa.
 
Hapo sasa ndo wabongo tunakera. Maandalizi yanafanyika mwaka mzima halafu tunakuwa na upuuzi kama huu dakika za mwisho?

Vipi mabanda lakini, yanavutia? Nimeona highlight za banda la Wizara ya Maliasili, nadhani litakuwa kivutio.

Ngoja nijiandae sasa kuondoka huku Dom, nami nishuhudie mwenyewe. Naona washikaji walioko Dar wanatuminyia, hawataki kutupasha news!
 
Chama cha wenye viwanda Tanzania, wamerudi? Walijitoa baada ya maonyesho kugeuzwa ya wamachinga.
 
ukweli navutiwa na makampuni machache ya nje na machache ya ndani lakini yolobaki ni fujo tupu sio maonyesho tena ni maduka ya vitu vya kichina vya kkoo na cm zinaamishiwa 77 tena kwa bei ya juu zaidi ukiuliza unaambiwa kodi kubwa
 
Kama makampuni gani na yanauza nini? Hebu tumegee kidogo, safari inakaribia kwa hiyo tujiandae!
 
Back
Top Bottom