Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

Hapa ndipo tunaopokesea Watanzania kwenye hoja/mambo mengi sana. Tuna-personalise mambo bila ulazima wowote.

Rais amekwenda kama Ofisi sio kama Kikwete...kwanza hiyo ziara ya Ivory C. (sijui kama kuna nchi zingine zitakuja) zimetengewa Bilioni 7. Sasa kwa hela hiyo sio Rais tu na Bunge lote (bila kupewa posho..!!) lingetakiwa kufika hapo uwanja wa Taifa kuweka msisitizo zaidi.

hakwenda kama Rais kwani hakuna ulazima wa Rais kwenda; ni kama kwenda kufungua hoteli ile ya Arusha ambapo hakukuwa na ulazima wake. Kama alitakiwa kwenda Rais angeenda Makamu wa RAis au hata Waziri Mkuu.. Au angalau ingekuwa ni mechi ya kugombania nafasi fulani au point fulani muhimu..
 
si kweli; hivi leo hii Taifa Stars ingeifunga Ivory Coast si tungeshabikia kwa kuchanga nusu bilioni nyingi kuisaidia Stars kama tulivyofanya ilipoifunga Togo; Rais hakuwa na sababu hata chembe ya kwenda kwenye mechi hii ya kirafiki isiyo na umuhimu wowote (i repeat haina umuhimu wowote ule) kwa soka la Tanzania. Tunajidanganya tukifikiria kuwa kwa kucheza na Ivory Coast basi wachezaji wetu wamejifunza kitu.. Si tulifikiria hivyo hivyo walipoenda Brazili?


Mkuu,

Hapa tuko pamoja, kama suala ni kuendeleza soka basi tunafanya mambo kinyume kabisa...tulitakiwa tuanzie chini, mashuleni, vyuoni n.k. Nakubaliana na wewe kabisa; hata kuwa na kocha wa Taifa Mbrazili au atoke Mbinguni...ili tuinue soka lazima tuazie kwenye grass roots.

Ila hapa kwa mujibu wa post yapo hapo juu; hoja sio hii.

Ni nani leo hii akiwa amefiwa na ndugu yake ambaye amemzika siku mbili nyuma anaenda kucheza cheza na kuruka ruka kwenye michezo isiyo na maana wala mantiki?

I beg to differ, naona na wewe una-personalise hii issue. Rais sio Mjomba wa nchi, Rais ni mtumishi wa nchi. Leo hii hata kama akifiwa yeye binanfi (God forbid) Taifa likimuhitaji; anatakiwa aweke majonzi yake pembeni akalitumikie Taifa.

Nitasita kujibu maoni yako kuhusu mchozo wa Footbal kwa sababu hapa kwa uelewa wangu hoja sio umuhimu wa football kwa taifa wala iwapo football ni mchezo makini au ni mchezo wa "kucheza cheza na kuruka ruka"

Aliyetutangazia msiba huu "mkubwa wa kitaifa" na ambaye alishindwa kujizuia machozi ndiye wa kwanza kwenda kushangilia mechi ya mpira ambayo matokeo yake hayana maana yoyote kwa Taifa Stars wale kwa Ivory Coast zaidi ya kuwapa taste ya matumizi ya uwanja wetu mpya..

Taifa kuwa msibani haimaanishi kabisa kuwa Ofisi ya Rais inasimama kulitumikia Taifa.

Hii spirit aliyonyeshwa na ofisi ya Rais inahitajika kwenye kila Sekta ya Taifa letu.
 
hakwenda kama Rais kwani hakuna ulazima wa Rais kwenda; ni kama kwenda kufungua hoteli ile ya Arusha ambapo hakukuwa na ulazima wake. Kama alitakiwa kwenda Rais angeenda Makamu wa RAis au hata Waziri Mkuu.. Au angalau ingekuwa ni mechi ya kugombania nafasi fulani au point fulani muhimu..

MKJJ

Unaangalia ziara hii ya Ivory Coast kwenye angle moja tuuu "FOOTBALL" angalia kwa pande zote ambazo zimepelekea Serikali kutenga Tshs Bilioni 7 (nisieleweke kuwa naunga mkono matumizi haya). Ndio maana nikasema kwa gharama hizo I don't care tumefiwa jana au leo; life has to go on.

Kama Taifa tumeadhirima vya kutosha na desturi za aina hii. Labda sasa wakati umefika tubadilike.
 
MKJJ

Marehemu Kawawa hakuwa Nyerere, sio kwa Cheo, Utashi wala Elimu. Usichanganye viongovi hawa wawili ili kujenga tu hoja yako.

Kwa kifupi JKN alikuwa Rais tena kwa miaka zaidi ya 20, na tangu amengatuka nchi imekuwa na maraisi 3 tu baada yake....sasa tangu Kawawa angatuke/aondolewe Uwaziri Mkuu tumekuwa na Mawaziri Wakuu wangapi..?? Hizi ofisi 2 moja ni kubwa sana kuliko nyingine...in fact hatuhitaji hata kuwa na Waziri Mkuu (but that's a topic for another thread).

well.. hakuwa Nyerere ni kitu ambacho mtu yeyote anakijua lakini mchango wake kwa Tanzania huwezi kulinganisha na wa Msuya, Warioba, Malecela, Lowassa, Salim wala hata Sokoine. Historia ya Tanzania tuijuayo sasa hivi haiwezi kuandikwa bila majina ya Nyerere na Kawawa kutajwa kwenye sentensi moja.

Na nafasi yake haiwezi kupimwa kwa vipimo unavyotumia. Aliyevuma baharini alikuwa Papa (Nyerere) na wengine walikuwepo.. Tatizo yawezekana unaamini sana stori za caricature ya RMK ambayo wengi wetu tulikuwa tunaamini.

nitakupa mfano..

She adds that the African Liberation Committee, formed by the Organisation of African Unity in 1963 to support liberation movements, “has information on the ANC, Madiba and the anti-apartheid movement. Some of these records will be added to the Foundation’s Mandela Materials database.”
“I had thought I would get more information from the TANU records. (The party has since changed its name to Chama Cha Mapinduzi.) I was however unable to access these records and the records of Mr Rashidi Kawawa, former Prime Minister of Tanganyika and of Tanzania in 1972-1977, who assisted Madiba in 1962 when he was in Tanzania en route to Ethiopia, Algeria and the rest of Africa,” says Ms Riba. These records are kept in Dodoma, the capital of Tanzania, 486km (300mi) from Dar es Salaam, where Ms Riba was based and where many government offices are located.

Hilo la msaada wa Kawawa kwa Mandela hata Mandela mwenyewe alirudia alipokuwa kwenye kesi yake mwaka 1964. Alisema hivi kwenye hili hotuba ya "Nimejiandaa kufa"

It was on this note that I left South Africa to proceed to Addis Ababa as a delegate of the ANC. My tour was a success. Wherever I went I met sympathy for our cause and promises of help. All Africa was united against the stand of White South Africa, and even in London I was received with great sympathy by political leaders, such as Mr. Gaitskell and Mr. Grimond. In Africa I was promised support by such men as Julius Nyerere, now President of Tanganyika; Mr. Kawawa, then Prime Minister of Tanganyika; Emperor Haile Selassie of Ethiopia; General Abboud, President of the Sudan; Habib Bourguiba, President of Tunisia; Ben Bella, now President of Algeria; Modibo Keita, President of Mali; Leopold Senghor, President of Senegal; Sekou Toure, President of Guinea; President Tubman of Liberia; and Milton Obote, Prime Minister of Uganda. It was Ben Bella who invited me to visit Oujda, the Headquarters of the Algerian Army of National Liberation, the visit which is described in my diary, one of the Exhibits.

utaona kuwa msaada wa Tanganyika unatajwa kwanza na ni nchi pekee ambapo aliona ulazima wa kutaja majina yote mawili la Nyerere na Kawawa! Of course wengine watasema Nyerere ndiye aliyestahili..!

No sir, mchango wa Kawawa hatujaungalia vizuri zaidi na hili limethibitishwa na kitendo cha kpuuzi cha JK kwenda mpirani wakati nchi iko kwenye maombolezo ya kitaifa. Yes I said "cha kipuuzi"!
 

I beg to differ, naona na wewe una-personalise hii issue. Rais sio Mjomba wa nchi, Rais ni mtumishi wa nchi. Leo hii hata kama akifiwa yeye binanfi (God forbid) Taifa likimuhitaji; anatakiwa aweke majonzi yake pembeni akalitumikie Taifa.

Atakuwa ni RAis mpuuzi kweli kama baada ya kufiwa na akaamua kwenda kushangilia netball kwa ababu taifa linamhitaji! Kama kushangilia mechi isiyo na umuhimu wowote ndio kumhitaji Rais basi tumekwisha!



Taifa kuwa msibani haimaanishi kabisa kuwa Ofisi ya Rais inasimama kulitumikia Taifa.

Kama kwenda kushangilia mechi kama hii ndiko kutumikia taifa basi tumekwisha!


Hii spirit aliyonyeshwa na ofisi ya Rais inahitajika kwenye kila Sekta ya Taifa letu.

Not really.. roho ya namna hii inahitaji kukemewa!
 
we babako akifa then within 2 days toka umzike tukuone bar umeshika fimbo ya kuchezea pool unadhani tutakuelewa??in simple terms hatuna rais serious....

Kazungukwa na banyamulenge na mafisadi kibao unafikiri nini?
 
SO hoja hapa ni:

1. taifa kama taifa kuto 0bserve ''maombolezo" kama tulivotangaziwa, au
2. Rais kwenda kuangalia mpira wa kirafiki kati ya Taifa stars na Ivory Coast?
 
Asilimia kubwa ya waTz hususani wasomi reasoning capacity yao ni ndogo sana but wao wenyewe hujiona ni wajanja na ndiyo maana mtu akiwa mjanja kidogo tu nakuligundua hilo basi atawadrive the way anavyotaka na kukaapembeni akicheka maana anaweza sema kitu kwa kutegesha uone respond ya Great thinkers....WATZ WANAJUDGE NANI KASEMA NA SIO KASEMA NINI HASA NA KINA ENDANA NA TUKIO AU MAANA HALISI?????........na WANASIASA WATZ wanalijua sana na ndoo maana wataendelea kutesa kwa kwenda mbele.....
" IF YOU REAL HAVE A BRAIN YOU WILL KNOW WHAT I REAL MEAN"
 
Lakini Kikwete ni kawaida yake hata wakati alipokuwa ziarani Uingereza alikutana na Watanzania kwa muda wa nusu saa na baadaye alikwenda kuangalia mpira wa timu yake ya Spurs.(Kipenzi cha roho). Huyo ndiye rais mliyemchagua. Watanzania walisafiri kwa matreni kutoka kila sehemu zaidi ya masaa kadhaa kumbe yeye alikuwa na hamsini zake.

Na hiyo ni tabia yake hawezi kuacha na utendaji wake wa kazi ndio hivyo hivyo goi goi. Sijui atakwenda kubembea wapi safari hii.
 
Hivi kuna mtu anakumbuka mara ya mwisho tulipokuwa na maombolezo ya kitaifa ilikuwa ni lini?
 
Hivi hizo 7 billioni zilikuwa kwenye bajeti na kupitishwa na bunge au ndio dharura yenyewe? Sikuona dharura kule Temeke Hospitalini.
 
It's just not a good look for him to be out there at a football game while the country is supposedly still observing seven days of mourning. He should have just stayed at home and watched the game if it was that serious. It is things like this that call into question his judgement as a leader.
 
Asilimia kubwa ya waTz hususani wasomi reasoning capacity yao ni ndogo sana but wao wenyewe hujiona ni wajanja na ndiyo maana mtu akiwa mjanja kidogo tu nakuligundua hilo basi atawadrive the way anavyotaka na kukaapembeni akicheka maana anaweza sema kitu kwa kutegesha uone respond ya Great thinkers....WATZ WANAJUDGE NANI KASEMA NA SIO KASEMA NINI HASA NA KINA ENDANA NA TUKIO AU MAANA HALISI?????........na WANASIASA WATZ wanalijua sana na ndoo maana wataendelea kutesa kwa kwenda mbele.....
" IF YOU REAL HAVE A BRAIN YOU WILL KNOW WHAT I REAL MEAN"

Kwani umesahau Jakaya aliposema asilimia 70 wanafuata upepo. Sasa angalia wewe mwenyewe sijui unafuata upepo upi?
 
It's just not a good look. He should have just stayed at home and watched the game. It is things like this that call into question his judgement as a leader.

ndio tatizo la watu walichoshindwa kusoma nilichoandika na wewe umekinyambulisha vizuri. Sina tatizo kama Rais angeamua kuangalia mpira huo kama mamilioni ya Watanzania wengine kwenye luninga.

Kwa kwenda kwake mpirani wakati yeye mwenyewe katutangazia msiba mkubwa wa kitaifa kumetrivialize umakini wake na zaidi ya yote umeonesha kuwa anasukumwa na vitu vidogo vidogo tu! Aliwahi kukatiza ziara kadhaa muhimu na kwenda misibani hapo nyumbani na kurudi na kuendelea na ziara hizo..

Kwa sababu huko mbeleni watakufa watu kwenye janga moja na jioni yake mtamuona anaangalia watu wanacheza ready!
 
MKJJ; Mzee Kawawa RIP si nasikia alikuwa upande wa JK wakati wa uteuzi wa mgombea urais?Historia ya Mzee Kawawa kuhusiana na huu ufisadi uliopamba moto iko vipi?
Mh Rais naona alikuwa na sababu "Nzito" za kutokuikosa mechi hiyo?
Duh!Ama kweli mla nawe si mfa nawe.
 
hii intuthibitishia kuwa sisi ni wanafiki wakubwa ,tunajidai kuwalilia watu ilhali moyoni hatuwafeel,binafsi naamini haikuwa sahihi kabisa kwa rais kuongoza kushangilia wakati taifa lipo kwenye majonzi angeangalia kwenye tv basi kama alikuwa na shida ya kumuona drogba angeenda tareha 7 watakapocheza na rwanda hii isingeleta picha mbaya ila kwa leo MR PRESIDENT im sorry to say this but umechemsha
 
Leo hii Sam Najuma ametuma salamu hizi:(tanzania daima)


RAIS mstaafu wa Namibia, Dk. Sam Nujoma, amemtumia salamu za rambirambi Rais Jakaya Kikwete kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais, Rashid Mfaume Kawawa.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ilieleza kuwa Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Kawawa wataendelea kukumbukwa daima kwa mchango wao mkubwa katika harakati za kupigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika.
"Tulipokuwa katika harakati za kupigania uhuru wa Afrika kutoka kwa Makaburu, Wareno na Waingereza, viongozi wetu Mwalimu Nyerere na Mzee Kawawa walishiriki kwa juhudi kubwa katika ukombozi huu, tutawakumbuka daima," ilisema taarifa hiyo.

sasa alipopewa taarifa hiyo akiwa uwanjani au Ikulu alifanya nini. Sitoshangaa alikataa kuifungua isije ikamharibia mood yake ya kushangilia taifa stars!
 
si kweli; hivi leo hii Taifa Stars ingeifunga Ivory Coast si tungeshabikia kwa kuchanga nusu bilioni nyingi kuisaidia Stars kama tulivyofanya ilipoifunga Togo; Rais hakuwa na sababu hata chembe ya kwenda kwenye mechi hii ya kirafiki isiyo na umuhimu wowote (i repeat haina umuhimu wowote ule) kwa soka la tanzania. Tunajidanganya tukifikiria kuwa kwa kucheza na Ivory Coast basi wachezaji wetu wamejifunza kitu..

Hapa unakosea. Mechi ni muhimu sana babu mbili. Moja, viwango vya FIFA hupimwa katika mechi zote ikiwemo za kirafiki. Mbili, Ivory Coast ni timu iliyo katika kombe la Dunia na hivy kuna umuhimu wa kuwavutia weeke kambi hapa Tanznaia kala ya kwenda Afrika Kusini na hivyo nchi kufaidika na kuitangaza.

Inawezeana Rais nkwenda ni tatizo lakini umuhimu wa mechi ni mkubwa sana kwa Taifa.
 
Leo hii Sam Najuma ametuma salamu hizi:(tanzania daima)




sasa alipopewa taarifa hiyo akiwa uwanjani au Ikulu alifanya nini. Sitoshangaa alikataa kuifungua isije ikamharibia mood yake ya kushangilia taifa stars!

una kikwetephobia? taarifa Rais hapew uwanjani. Taarifa hii ya Nujoma imeletwa toka jumapili na mimi nimesikia ikisomwa taarifa ya habari ya TBC Taifa juzi juaa mbili usiku.Mechi ilikuwa leo
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?

Mi nafikiri kuna tofauti kati ya maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti. Nafikiri kinachofanyika ni bendera kupepea nusu mlingoti lakini kama ni maombolezo huwezi omboleza kwa burudani (kwenda mpirani).
1999 baada ya kifo cha Nyerere tulikaa mwezi mzima bila mipira kuchezwa wala TV na vyombo vya habari kutangaza au kuonesha burudani
 
Back
Top Bottom