Maombi Ya Uchaguzi Mkuu 2010

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,488
86,004
MUNGU Baba, wewe uliyetukuka sana, wewe ustahiliye kuabudiwa na kila kiumbe, wewe MUNGU wa mababa zetu, tuko mbele zako wana wako, tuko mbele zako leo Baba, tunakuja tena kwa kulia na kuomboleza, tukiililia Nchi yetu, Nchi ambayo wewe MUNGU ndie ulieamua sisi tuzaliwe hapa.

Tunakuomba sana kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa nchi yetu 2010, tujalie utuongoze katika kufanya uchaguzi wa haki na huru, waaibishe na kuwafedhehesha wale wote wenye mapenzi mabaya na nchi yetu BABA.

Tunamchagua mwanadamu tena mwenye mapungufu Baba, tunaomba ulinzi wako uwe juu yetu, tubariki na utuvushe katika kipindi hiki, wengi walilia na bado wengi wanalia, nchi zinaomboleza, maafa, damu, vita kila mahali Baba, tuponye tunakuomba Baba.

Mbinu zote chafu, mawazo yote machafu dhidi ya wagombea hawa nazifunga katika DAMU ya YESU Kristo, wewe MUNGU uliewavusha wana wako katika matatizo mbali mbali katukumbuke na sisi leo Baba, sikia maombi yetu Baba, Wewe ni MUNGU unaejibu maombi, wewe ni MUNGU ulie HAI, tunakusihi Baba, tunakuomba Baba yetu, tuponye na machafuko na vita ili sisi tukaseme siku moja kwa ushuhuda kwamba "Kama si wewe BWANA...mwanadamu na aseme sasa".

Nawaombea wooote watakaosoma na kuielewa sala hii, si katika hali ya kupinga bali katika hali ya kuelewa, uwape kibali mbele yako, wao na familia zao na ndugu zao, na wale wooote MUNGU watakaopinga sala hii, kwa namna moja au nyingine Wabariki pia

Ni katika JINA la YESU KRISTO tunaomba.....Na wote mseme AMEN
 
Tuiombee Tanzania jamani
Every time I remember I'm a Tanzanian I really pray for my country.
When I see all injustice, theft and the poor Tanzanians in their blessed land, I can't help but pray with tears.
In short, All the time, my Love for my country drives me into my knees.
God is gracious, God is good!
He will take us off this yoke....in Jesus precious Name!
 
Ee Mungu, Tupe kiongozi aliyetokana na maamuzi ya wananchi kwa ustawi wa taifa la tanzania.
 
We come before THEE,ooh Father GOD...and hope that You will put Your hand upon our lovely country.
Let Your glory reign,let Your power be manifested unto us...oooh LORD as we commit every person who
is involved in one way or the other to this election.
We rebuke any negativity in Your name...and allow Your righteousness to dwell.
Amen!!
 
every time i remember i'm a tanzanian i really pray for my country.
When i see all injustice, theft and the poor tanzanians in their blessed land, i can't help but pray with tears.
In short, all the time, my love for my country drives me into my knees.
God is gracious, god is good!
He will take us off this yoke....in jesus precious name!

amen!
 
eeeeh Mungu tupe Dr Slaa kama ulivyomchagua Yusuph kuwa kiongozi mkuu..Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi Amen
 
Ee mungu tunaomba uingilie kati kikwete asirudi tena madaeakani kwani atatugawa watz kwa udini(mahakama ya kadhi & oic)na ukabila (shule za kata)..........hatumtakiokabisa
 
Chama cha wlokole kamwe hakokublika kwa wananchin kuendesha nchii hii secular country. niwazi mtabadilisha ikulu kuwa kanisa!! Mungu aepushe mbali na balaa lenu na mshindwe !!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom