Maombi ya mvuta bange yafanikiwa kuliko ya mchungaji

Midavudavu

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
287
59
Kijana mmoja wakati wa kijiandaa na mitihani ya kidato cha 4 alikuwa anasoma na wenzake usiku gheto. Huko gheto wenzi wakamfundiosha kuvuta bangi. Bangi ilipomkolea akachanganyikiwa akawa anasema hovyo na kupagawa. Baada ya wenzie kumrudisha kwa wazazi wake ikabidi aitwe mchungaji jirani ili amuombee. wachungaji kama mnavyojua tena akaaanza "toka kwa jina la......na .........hakuna kilichotokea na badala yake jamaa makelele yakazidi. Mmoja kati ya wale aliokuwa anavuta nao bange akashauri "huyu dawa yake nyepesi tu mpeni miwa ale" Ikatafutwa miwa usiku huohuo na jamaa baada ya kufakamia miwa akapata nafuu. Wazazi wakambana jamaa aeleze imekuwaje hadi akajuwa ugonjwa wa mtoto wao unaweza kupona kwa kila miwa. Naye hakuficha " jamani hapa hakuna pepo wala nini sisi tulikuwa tunavuta bange gheto na bahati mbaya jamaa yetu ni mwepesi katika mambo haya". Wazazi angalie makundi ya prep. wanayoshiriki watoto wenu je yanawasaidia au yanachangia kuwaharibu zaidi?. Hili ni tukio la kweli, utani umechukua sehemu ndogo sana.
 
1.ukweli ni kuwa tunafanya makosa kwa kukariri hata kwa vitu vya kutumia logic ya kawaida, mlokole ameaibika kwa kumwita .... atoe mapepo wakati ishu haiusiani na hayo mapepo. Wanafanya makosa haya mara nyingi sana utakuta mtu malaria imepanda kichwani badala ya kumpeleka hospitali wao wanampeleka kanisani kumuombea!! YESU HATAKI WAPUMBAVU HATA KIDOGO!
2. tunatakiwa kuangalia tulipojikwaa sio kuhangaika na tulipoangukia.
BIG UP!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom