Maombi maalumu kwa Rais John Joseph Pombe Magufuli

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Wana JF na Watanzania wenzangu,
Rais wetu wa A5 amekuwa akisistiza kwenye speech zake mara kwa mara kwamba Watanzania na hasa viongozi wa dini zote wamwombee maana ameomba kazi ngumu ambayo haiwezi peke yake hivo anahitaji support ya maombi toka kwa Watanzania. Kuna viongozi wa dini wamekuwa wakiomba maombi ya kinafiki yenye kulalia upande mmoja kwa kuwalaumu CHADEMA kuwa wanataka kuchochea vurugu ilhali ukweli wenyewe ni kwamba Rais ndiye aliyeanzisha chokochoko hizi kwa kuzuia mikutano na maandamano ambayo yanaruhusiwa Kikatiba na Kisheria.

Leo nimeonelea nilete maombi yangu hapa ili Rais John Joseph Pombe Magufuli popote atakapokuwa maombi haya yatamtafuta yamfikie na yafanye kazi ndani yake kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu. Biblia inasema,''Maombi ya mwenye haki yafaa sana akiomba kwa bidii' na kwamba ''Eliya alikuwa mwanadamu kama sisi aliomba kwa bidii na mvua haikunyesha kwa miaka 3 na nusu duniani na ikawa hivo na ''HERI WENYE KULIA NA KUUGUA JUU YA MACHUKIZO YANAYOFANYIKA JUU YA NCHI'' .Kwa sasa kinachofanyika kwenye hii A5 kuna machukizo ambayo lazima tuombe na kuugua ili Mungu aepushie mbali!

Maombi:
''Baba Mungu muumba wa mbingu na nchi, katika jina Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wetu naomba Roho wa Mungu akamshukie Rais wa Tanzania John Joseph Pombe Magufuli ili ampe hekima, busara, maarifa na ufahamu wa kuongoza Taifa hili. Kama kuna roho yoyote ya ukatili na uonevu ndani yake naikemea katika Jina la Yesu Kristo ikashindwe na kulegea na ikarudi kuzimu. Bwana Yesu Rais huyu aliapa kwa kutumia Kitabu chako Biblia kwamba atailinda na kuitetea Katiba ya JMT lakini kwa sasa anaonekana ame kengeuka na kuacha kuilinda Katiba kwa kuwakataza Watanzania wenzake wasio wana CCM kufanya mikutano na maandamano ya Kisiasa kwa kisingizio kwamba watamchelewesha kufikia malengo na ahadi alizotoa kwa Watanzania.

Bwana Yesu, naomba roho ya kikatili ya kutaka kuwazuia Watanzania na Wana chadema kwa kutumia Jeshi la Polisi ikashindwe katika Jina la Yesu Kristo. Baba Mungu ni hivi karibuni tu kuna ASKARI POLISI AMEFUNGWA MIAKA 15 KWA KUTEKELEZA MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI kwa mazingira kama haya kwa amri ya Polisi. Hivo Bwana Yesu inapokaribia siku ya tarehe 1, Septemba 2016 mpe Rais hekima na busara ili akaweze kuwaamuru hawa Polisi wake wasije wakasababisha mauaji ya kina Duadi Mwangosi wengine.

Bwana Yesu, wewe umeumba wanadamu wenye roho na tabia tofauti tofauti akiwemo Rais JPM. Yawezekekana kabisa JPM ni Rais katili asiyejali nafsi za watu, mwenye roho ya kisasi, kulipiza, kutesa, kunyanyasa na kudhalilisha wengine. Kama roho hii iko ndani ya Rais huyu wa Tanzania naomba ukaiondolee mbali. Ondoa moyo wa kijiwe,kiburi, jeuri na kujivuna ndani yake na ukampe moyo wa UPOLE, UNYENYEKEVU, BUSARA,HEKIMA na USIKIVU wa kuiongoza Tanzania.

Mungu Baba naomba pia Roho wa Mungu akamshukie IGP Ernest Mangu na Jeshi lake la Polisi ukaondoe roho ya UKATILI NA MAUAJI ambayo inamnyemelea kwa kuanzisha mazoezi ya VITISHO katika ya majiji na miji. Mungu iangalie nchi hii ambayo ilikuwa mstari wa mbee kupigania haki za WAAFRIKA waliokuwa wakigandamizwa na minyororo ya Ukolone, na hatimaye kuwasaidia ndugu zetu wa Afrika Kusini na nchi nyingine kujipatia Uhuru wao. Lakini leo hii Tanzania ya JPM inataka kugeuka kuwa nchi ya MAKABURU kwa Polisi kutesa na kupiga Raia wake kwasababu ya maandamano. Tunakemea kwa JIna Yesu hali hii usije ukaruhusu itokee hiyo tarehe 1,Septemba. Naikemea roho ya mafarakano, mashindano na mabishano kati ya CCM na CHADEMA, Rais Magufuli na Viongozi wote wa UKUTA(Mhe. Mbowe, Mhe. Lowasa, Mhe. Mbatia n.k.) Weka roho ya mapatano ndani yao ili wakapatane ili tusifikie vurugu kabla ya tarehe 1 Septemba,2016. Hii nchi ni yetu sote wana CCM na wana CHADEMA na hakuna mwenye hati miliki. Itakuwa ni aibu kwa Tanzania kama damu itamwagika kwasababu ya ujinga wa mtu mmoja kukosa Hekima, Maarifa na Busara..

Mtumishi wako Sulemani mwana wa Daudi katika Kitabu cha MITHALI 8: 13-17 amesema nami nanukuu:

12 Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu; Natafuta maarifa na busara.
13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
14 Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi; Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu.
15 Kwa msaada wangu wafalme humiliki, Na wakuu wanahukumu haki.
16 Kwa msaada wangu wakuu hutawala, Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.
17 Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

Mungu Ibariki Tanzania na Mungu ibariki Afrika na watu wake,

Amen and Amen.
 
Duuuuh we jamaa umenifanya na mimi nimuombee mtu ambaye sipendi kumuombea, eeh Mungu wangu nilikuwa nasoma tu sala ya huyu ndugu yangu ila si kuwa na nia ya kumuombea huyo muombewa kwa hiyo naomba ufute maombi yangu badala yake nakuomba uwalinde wananchi wa taifa lako. Amen
 
Mhh sala juu ya sala kinyume cha sala
 
ILA MKUU HII SALA/DUA IMEKAAKAA KAMA VILE MKULU ANA PEPO VILE UNAMUOMBEA LIMTOKE.....UNAKUMBUKA SAULI ALIKUWA NA PEPO AKAWA ANATAKA KUMUUA DAUDI ILA MKONO WA MUNGU ULIKUWA JUU YA DAUDI NA ALIMLINDA DHIDI YA UPANGA WA SAULI MFALME?

MKULU ANATAKIWA KUPIGIWA KINANDA NA KINUBI PEPO HUYO ATULIE ILI AELEZWE HAYA MAMBO MAZITO NA TAIFA LITAEPUSHWA NA DHAHAMA HILI LINALOTUNYEMELEA......

HIVI MKUU UNAMKUMBUKA NEBUKADREZA....MALME ALIYESHIKIKISHWA ADABU NA MUNGU KWA KUVULIWA UFALME NA KUTUPWA PORINI AKALA MAJANI NA SWALA NA WANYAMA WA MBUGANI KWA MIAKA SABA HIVI?.......

MKULU INABIDI ASOMEWE MAANDIKO HAYO YAMKUMBUSHE KUWA KUNA MUNGU ANAYEISHI....NA ANAWEZA KUMKWEZA AU HATA KUMSHUSHA YEYOTE POPOTE PALE ALIPO.....
 
Duuuuh we jamaa umenifanya na mimi nimuombee mtu ambaye sipendi kumuombea, eeh Mungu wangu nilikuwa nasoma tu sala ya huyu ndugu yangu ila si kuwa na nia ya kumuombea huyo muombewa kwa hiyo naomba ufute maombi yangu badala yake nakuomba uwalinde wananchi wa taifa lako. Amen
Hahaahha we kiboko
 
MKWEPA KODI,
Kwanza nakuombea uanze kulipa kodi usije ukatumbuliwa bure na JPM. Huyo ni pepo wa kukwepa kodi lazima akutoke. Lakini kwa hili la JPM kukandamiza Demokrasia kwa kusigina Katiba na Sheria za nchi lazima tuikemee roho hii ili Mungu abadilishe moyo wa Rais wetu.
 
Maombi koko kutoka kwa mwombaji koko.
Kabla ya uchaguzi mlikesha kumwomba Mungu awape raisi akamleta huyo ambaye Mungu anamtaka.Kwa kuwa vichwa vyenu vilikuwa na mtu wenu kichwani mlikuwa mkiomba maombi ya kinafiki sababu mlikuwa mkisema mnamwachia Mungu awachagulie kumbe mioyoni mwenu mna jina lenu.Kwa nini mlienda kumsumbua Mungu kuwa tuchagulie tuchagulie wakati mtu mnaye vichwani mwenu? Mwombaji koko wewe?

Pili eti unaombea vyama.Vyama vina dini na vimebatizwa na kuwa vikristo? Vyama havitambuliki kwa Mungu we mwombaji koko.Eti naiombea CHADEMA.loooooo huna haya wewe mwombaji koko
 
Bwana Yesu,
Angalia mtu huyu anayejiita YEHODAYA, unamjua hapo alipo kwa Jina na kwa sura. Biblia inasema MUNGU HADHIHAKIWI. Tazama huyu mtu ananajaribu kuleta dhihaka ma mizaha kwenye jambo la msingi linalohusu mstakabali wa nchi ya Tanzania. Mungu msamehe maana hajui atendalo. Sijali ni mwana CCM au mwana CHADEMA au chama chochote hapa tunaomba kwa ajili ya Usalama na Amani ya nchi yetu si kwa jili ya chama fulani.Naomba Mungu ukashughulike na roho hii ya machukizo na ukaizamishe katika vilindi vya kuzimu na ikatoweke. Biblia inasema katika MATHAYO MT 5:9.''HERI WAPATANISHI MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU''

Amen........
 
Mna dhihaka mara mnakuja Timu ya Taifa tuiombee mara yanga na huyo tena dua au sala za Wagonjwa wasiojiweza hospitalini mpo kimya hayo maombi ya woga kwa baadhi ya watu mkiwaacha wanaotakiwa kuombewa mnamaanisha nini..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom