Elections 2010 Maombi kwa ajili ya uchaguzi

Ngigana

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
2,102
1,435
Mungu uliye umba mbingu na nchi, uliyeumba Tanzania na watu wake; kesho watanzania wanapiga kura kuwachagua viongozi wao. Wapenda amani twakusihi uchaguzi uwe wa amani na haki. Kila mgombea avune anachostahili na matokeo yatangazwe sawa na idadi ya kura alizopata. Wale wote wanaopanga kuiba kura wapigwe upofu na mipango yao isifanikiwe! wale wote wanaopanga kuchakachua kura wakati wa kujumlisha, iwe kwa kuvuruga na kuingilia mitandao (IT) hao wapigwe wazimu wachanganyikiwe kabisa ili uovu wao usifanikiwe! Muumba mbingu na nchi weka malaika zako wema katika kila kituo cha kupiga kura ili kuwatia hofu wote wenye mipango miovu ya kuiba kura na hivyo kuwadhihaki watanzania. Mungu nchi yetu imekuwa kituko katika nyanja zote elimu, afya, michezo, miundo mbinu nk. Mungu inatosha tunataka ukurasa mpya. Wakumbuke watanzania kwa kuwapa akili na utashi mwema ili kesho wasifanye makosa, watumie akili zao njema na ufahamu kuchagua viongozi watakao livusha taifa hili liondokane na umaskini wa akili. Muumba mbingu ikumbuke Tanzania, kwa kuwa wakati wa mabadiliko ni sasa na hasa hiyo kesho 31/10/201.:israel:
Ahsante kwa kiutakabali sala hii.
Mungu ibariki Tanzania! AMINA!!!!!!!
 
Back
Top Bottom