Senior Bachelor
Member
- Mar 23, 2011
- 86
- 32
Chombo kii baharini, mawimbi yasukasuka
Waloshika usukani, manahodha moja hulka
Walikitoa ufukweni, baharini 'kiingika
Abiria mehamaki, chombo chaenda mrama!
Ilipoanza safari, kutapika walihisi
Kwa woga wayo bahari, majiye kuyaakisi
Taratibu wakakiri, hawakuwa nayo jinsi
Nahodha kawatuliza, kuikabili safari.
Injiniye yachemka, nahodhaye chamshinda
Abiria wanamaka, wamehisi kinapinda
Tobo 'megundulika, 'lotoboa sio kinda
Manahodha moja hulka, chombo chenda mrama.
Aloshika usukani, Cheka Jino mpole
Litia na tumaini, chombo lipopokea
'Biria lipata amani, wakidhani si gobole
lo! Kama walotangulia, huyu pia limbukeni!
Limbukeni 'jisifia, ajigamba yu mweledi
Jama namhurumia, ajifanya maridadi
Chombo kinajinukia, hata akipiga dobi
Ukubwani kaingia, ndevuze hazichomozi!
Mashauriano afanya, ya akidi na unywaji
Kila wakiyamaliza, wajipamba kwa uaridi
Maji ya vikao vyao, machozi ya abiria
Ndio! chombo ki baharini, maji chumvi hayanyweki!
Vya wengine vyaelea, bahari haivitishi
Matobo meyamendea, maji hayawaangushi
Makasia 'jipigia, kama bwana maangushi
Chetu kinajizamia, manahodha tubadili.
Toka kiwe baharini, nchi kavu kijaona
Kama vile harusini, manahodha hawaj'ona
Wisiki wazitamani, wa'giza bila amana
Machoziye abiria, ni kinywaji chao bora!
Abiria amkeni, kusanyeni zana zenu
Machoziyo hayanyeshi, hata mchicha wa menge
Tafuteni nazo nyundo, zibeni hayo matobo
Manahodha fukuzeni, mchukue usukani.
Kwa majigu jifunzeni, na kwa nyuki vilevile
Nyuki wao wafaidi, kwa asali ya sukari
'Nyigu mwisho ni masega, hivi asali wawezi?
Lakini kiwasikia, wajiita nao nyuki!
Waloshika usukani, manahodha moja hulka
Walikitoa ufukweni, baharini 'kiingika
Abiria mehamaki, chombo chaenda mrama!
Ilipoanza safari, kutapika walihisi
Kwa woga wayo bahari, majiye kuyaakisi
Taratibu wakakiri, hawakuwa nayo jinsi
Nahodha kawatuliza, kuikabili safari.
Injiniye yachemka, nahodhaye chamshinda
Abiria wanamaka, wamehisi kinapinda
Tobo 'megundulika, 'lotoboa sio kinda
Manahodha moja hulka, chombo chenda mrama.
Aloshika usukani, Cheka Jino mpole
Litia na tumaini, chombo lipopokea
'Biria lipata amani, wakidhani si gobole
lo! Kama walotangulia, huyu pia limbukeni!
Limbukeni 'jisifia, ajigamba yu mweledi
Jama namhurumia, ajifanya maridadi
Chombo kinajinukia, hata akipiga dobi
Ukubwani kaingia, ndevuze hazichomozi!
Mashauriano afanya, ya akidi na unywaji
Kila wakiyamaliza, wajipamba kwa uaridi
Maji ya vikao vyao, machozi ya abiria
Ndio! chombo ki baharini, maji chumvi hayanyweki!
Vya wengine vyaelea, bahari haivitishi
Matobo meyamendea, maji hayawaangushi
Makasia 'jipigia, kama bwana maangushi
Chetu kinajizamia, manahodha tubadili.
Toka kiwe baharini, nchi kavu kijaona
Kama vile harusini, manahodha hawaj'ona
Wisiki wazitamani, wa'giza bila amana
Machoziye abiria, ni kinywaji chao bora!
Abiria amkeni, kusanyeni zana zenu
Machoziyo hayanyeshi, hata mchicha wa menge
Tafuteni nazo nyundo, zibeni hayo matobo
Manahodha fukuzeni, mchukue usukani.
Kwa majigu jifunzeni, na kwa nyuki vilevile
Nyuki wao wafaidi, kwa asali ya sukari
'Nyigu mwisho ni masega, hivi asali wawezi?
Lakini kiwasikia, wajiita nao nyuki!