Manusura wa Mafuriko waonesha hasira kwa JK - Dar

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Wananchi manusura wa mafuriko Dar waonesha hasira zao dhidi ya serikali ya CCM. Mmoja wa waathirika alikataa kuokolewa na waokozi wa kujitolea,baadb ya kukaa siku ya 2 na familia yake juu ya paa la nyumba,pasipo msaada toka serikalini. Hatimaye mtu huyo kafa maji.

Aidha,ktk eneo la shule ya Mchikichini,mama manusura amegoma kumjibu rais JK aliyemwuliza ilikuwaje. Alipofuatwa na wana habari waliotaka kujua kisa cha yeye kukataa kumjibu Jk amesema ameachwa siku 2 kwenye mafuriko na kitoto chake kichanga pasipo msaada wa serikali.

Hawa ni sampuli ndogo inayoonesha jinsi wananchi walivyojaa hasira dhidi ya serikali na ccm waendekeza ufisadi na anasa,na kusahau kuutumikia umma.

source: "Tuongee Asubuhi" Star tv na "Nipashe" 23-dec-11
 
serikali yetu huwa inafika kwa wakati kwenye matukio kama ya migomo na maandamano tena ikiwa na vitendea kazi vilivyokamilika.Lkn kwa issue kama hizi za majanga huwa inawachukua muda mrefu kujiandaa.Hao manusura wasilalamike sana kwani serikali ndivyo ilivyo.
 
Duh, siku mbili bila jitihada zozote za kuokoa manusura? Hii nchi inaelekea wapi?
 
Siku mbili mtu juu ya paa,tena bongo hapo hapo ambako tunaamini serikali ndio iko hapo na tz ndio hapo,sijui ingekuwa ni mikoani sithani kama kungefanyika jitihada zozote
 
Kweli inasikitisha sana kuona watu wanahangaika bila msaada. Majeshi yetu yanajua mbwembwe tu na ku respond haraka katika kudhibiti maandamano na sio katika kutoa misaada. Lakini inabidi na sie wananchi tupunguze ubishi.

Watu wakiambiwa wahame mabondeni wasikaidi ni kwa usalama wao. Pale darajani Tangi bovu nyumba zinaendelea kujengwa tena karibu kabisa na mto. Kama serikali imelala sijitahidi kujiweka sawa sie wenyewe.
 
Wangesikia kuwa kuna maandamano mahali karibia na yalipo mafuriko,hapo wangejitosa na virungu vyao.
 
Tatizo watu wanawaza siasa tu humu, hata mafuriko nayo serikali kwani ndo imeleta mvua? watu wanaishi mabondeni hawataki kuhama wafanyejwe? rais anakuuliza unakataa kumjibu kwani yeye ndo mmeo? vitu vingine tusiingize siasa ukisaidiwa kubali. Hata kama ingekuwa ni chadema au chama gani wangezuia hayo mafuliko? Jamani acheni siasa penye hakuna.
 
Watu walikuwa wakitembea kwa miguu makundi makubwa kuzidi wale waliokuwa wakitoka mahakamani arusha. nilitarajia tafsiri maandamano ya jeshi la polisi la mwema kuchukua hatua ya kuwakamata wote na kuwafungulia mashtaka kwa mujibu wa sheria baada ya gari kikojozi kutimiza wajibu wake!!!!
 
Tatizo watu wanawaza siasa tu humu, hata mafuriko nayo serikali kwani ndo imeleta mvua? watu wanaishi mabondeni hawataki kuhama wafanyejwe? rais anakuuliza unakataa kumjibu kwani yeye ndo mmeo? vitu vingine tusiingize siasa ukisaidiwa kubali. Hata kama ingekuwa ni chadema au chama gani wangezuia hayo mafuliko? Jamani acheni siasa penye hakuna.

Hata kuokoa watu hawawezi ndugu. Soma hoja za watu kwa makini, hawazungumzii kuzuia mvua.
 
Tatizo watu wanawaza siasa tu humu, hata mafuriko nayo serikali kwani ndo imeleta mvua? watu wanaishi mabondeni hawataki kuhama wafanyejwe? rais anakuuliza unakataa kumjibu kwani yeye ndo mmeo? vitu vingine tusiingize siasa ukisaidiwa kubali. Hata kama ingekuwa ni chadema au chama gani wangezuia hayo mafuliko? Jamani acheni siasa penye hakuna.

Kuwaza siasa si tatizo, think twice before.....
 
serikali yetu huwa inafika kwa wakati kwenye matukio kama ya migomo na maandamano tena ikiwa na vitendea kazi vilivyokamilika.Lkn kwa issue kama hizi za majanga huwa inawachukua muda mrefu kujiandaa.Hao manusura wasilalamike sana kwani serikali ndivyo ilivyo.

Hivi ulikuwa hujui huu ndo wakati wa serikari kutoa kafara
 
Tatizo watu wanawaza siasa tu humu, hata mafuriko nayo serikali kwani ndo imeleta mvua? watu wanaishi mabondeni hawataki kuhama wafanyejwe? rais anakuuliza unakataa kumjibu kwani yeye ndo mmeo? vitu vingine tusiingize siasa ukisaidiwa kubali. Hata kama ingekuwa ni chadema au chama gani wangezuia hayo mafuliko? Jamani acheni siasa penye hakuna.
ALIYEWAUZIA VIWANJA NI NANI? KAMA HAPARUHUSIWI KUISH MTU ALIYEPELEKA HUDUMA ZA MAJI NA UMEME NI NANI? MWENYE MAMLAKA YA KUWAHAMISHA HUKO BONDENI NI NANI? Tafakari chukua hatua!
 
wahanga wanatakiwa kushtkiwa kwa kujenga mtoni.historia inaonyesha walishafukuzwa hapo si zaidi ya mara moja.serikali inakwambia toka hapo hapafai unakaa yakikukuta unamlaumu alikwamba usikae hapo.mvua ikiisha inabidi ipigwe bomobomoa kama ule ukuta wa palm beach au ghorofa la masaki.serikali inalijua hili ni kwamba kuna watu wamekaaa standby wafukuzwe mabondeni wao wakawape kadi za chama chao na kitangazia serikali mbaya haina utu
 
Alijokoa mwenyewe baada ya siku mbili? wacheni unafik.
Ww mama una matatizo ya akili..watu wengi wamejiokoa wenyewe na kwa kusaidiana baina yao. Hakuna mikakati wala jitahada zozote za uhakika zilizofanywa na serikali yenu kuokoa watu. Kwanza nakushangaa uko online badala ya kwenda kuwasiadia ndugu zako unawaita wa mjini, manake wengi wao ndo wanaosishi mabondeni. Sisi wakuja tuna afadhali!
 
JK alionyesha dharau alipotembelea walio athirika na mafuriko eneo la jangwani alisema hivi sasa inabidi hapa muhame, aiwezekani kila kipindi cha mvua muwe mnapata kero kama hizi; mtu mwenye akili timamu awezi kuishi hapa hapo kwenye red mi naona ni dharau inamaana wanao ishi pale hawana akili timamu au maisha magumu yaliyosababishwa na serikali yake
 
Ww mama una matatizo ya akili..watu wengi wamejiokoa wenyewe na kwa kusaidiana baina yao. Hakuna mikakati wala jitahada zozote za uhakika zilizofanywa na serikali yenu kuokoa watu. Kwanza nakushangaa uko online badala ya kwenda kuwasiadia ndugu zako unawaita wa mjini, manake wengi wao ndo wanaosishi mabondeni. Sisi wakuja tuna afadhali!

Achana nae.... ndo hao watu wa kubebwa ndo maana anatetea hata upuuzi.. yeye kazi yake kumlaumu Nyerere tu.
 
Back
Top Bottom