Manusura mwingine aokolewa Haiti

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,706
155,275
Manusura mwingine aokolewa Haiti

Kijana wa kike ameokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo moja katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince , -siku kumi na tano baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi.
Tetemeko hilo liliharibu sehemu kubwa ya mji huo na kusababisha hasara kubwa.
Kijana huyo amefutwa kutoka vifusi hivyo na maafisa wa uokozi kutoka Ufaransa.
Waokozi hao wanasema alikuwa amekwama kwenye bafu ambako aliishi kwa kunywa maji.
Wamesema licha ya kuwa na mshangao na kupata jeraha la mguu alijawa na furaha.
Ameokolewa siku tano baada ya serikali ya Haiti kusimamisha rasmi shughuli zote za kuwasaka na kuwaokoa walionusurika.
Yamkini watu laki mbili walifariki katika tetemeko hili lilotokea Januari 12 na wengine 130 wakiokolewa kutoka vifusi vya majengo yalioharibika.
Wakati huo huo rais wa nchi hii Rene Preval ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge ambao ulipangwa kufanyika mnamo Februar 28.
 
Yaani, Mungu ni mkubwa. Yamkini kutakuwepo na watu wengi ambao bado wako hai na Serikali kwa kusitisha uokoaji ina maanisha imewapa "death penalty". Mungu wanusuru wote ambao bado wameshikiliwa na vifusi na wako hai kwa uweza wako. Amen.
 
Miraculous! How can s.o survive on bath water! Unbeleaveable pple.
Hebu kunywa wewe km hatujakuzka sasa ivi.
 
Back
Top Bottom