Mantiki ya Mstari Mwembamba kati ya Penzi na Chuki/Logic of A Thin line between Love and Hate

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,605
1,704
- Mwanadamu anajipenda nafsi yake
- Mwanadamu anapompenda mwanadamu mwingine ni mwendelezo wa kujipenda nafsi yake mwenyewe
- Mwanadamu anapomwagwa, anapokataliwa ama anapoacha kupendwa na mwenzake huishia kujichukia
- Mwanadamu anapojichukua basi mwisho wake ni kuvuka mstari na kumchukia yule aliyekuwa anampenda

*Dhana ya kumpenda mwanadamu mwingine kama nafsi yako haipingani na hii mantiki ya mstari mwembamba

English translation to follow shortly, oops, I mean later!
 
Basi mimi l got it all wrong, maana nilifikiri wanaojipenda sana huwa wanawachukia wengine, maana huwa so selfish and unconsiderable.
 
lol, huwezi kumpenda binadamu mwingine kama hujipendi, tena watu wasiojipenda ni wagumu sana kwenye mahusiano maana wanajaribu kulazimisha wapendwe sana ili kufidia ombwe zito walilo nalo moyoni kwa kushindwa kujipenda nafsi.
 
- Mwanadamu anajipenda nafsi yake
- Mwanadamu anapompenda mwanadamu mwingine ni mwendelezo wa kujipenda nafsi yake mwenyewe
- Mwanadamu anapomwagwa, anapokataliwa ama anapoacha kupendwa na mwenzake huishia kujichukia
- Mwanadamu anapojichukua basi mwisho wake ni kuvuka mstari na kumchukia yule aliyekuwa anampenda

*Dhana ya kumpenda mwanadamu mwingine kama nafsi yako haipingani na hii mantiki ya mstari mwembamba

English translation to follow shortly, oops, I mean later!
And hence your question is??

Kwa jinsi ninavyoelewa mimi nashindwa kujua kama ni sawa au si sawa na wewe.
Ni kwamba altenate kati ya Love na Hate iko so frequent kiasi kwamba ni kama zinaungana kabisa!
Mfano, mtu unayemchukia sana inaweza kutokea ghafla ukampenda sana(Hii ina-apply zaidi kwa jinsia), na hatimaye ukaishia kumwuoa au kuolewa naye, na ni wengi wa hivyvo...anakusimulia kuwa huyu mume wangu nilikuwa namchukia sana kabla ya kunioa!!
Lakini pia the opposite applies as mtu unayempenda sana unaweza kumchukia kupindukia...mifano ni mingi mno kwa hilo.

A very thin Line between Love and Hate...they are almost joined!
 
lol, huwezi kumpenda binadamu mwingine kama hujipendi, tena watu wasiojipenda ni wagumu sana kwenye mahusiano maana wanajaribu kulazimisha wapendwe sana ili kufidia ombwe zito walilo nalo moyoni kwa kushindwa kujipenda nafsi.

Duh
Nafikiri inabidi tudefine huko kujipenda; maana inaweza ikawa hatuelewani.
Kwa mswahili mtu asiyejipenda ni yule ambaye uvaaji wake uko shabby, mchafu, kifupi asiyejijali. Anayejipenda ni yule ambaye yuko over-conscious kuhusu yeye mwenyewe na muonekano wake ni kama arrogant fulani hivi, anachokitaka lazima akipate bila kujali anamuumiza nani in the process.
 
Naunga mkono hoja 100% Ila naomba nisumarize tu hayo uliyoyaongea

UKIMPENDA MTU SANA MKIJA KUKOROFISHANA UTAMCHUKIA SANAAAAAAA! NA UKIWA UNAMCHUKIA MTU SANAAAA UJUE MKIPANA MTAKUWA MNAPENDANA SAAAAAA HENCE PROVED THERE IS A THIN LINE BTN LOVE N HATE!!!! BETTER BE NEUTRAL TO STAY SAFE IN THE MARGIN!!!! LOL!
 
Companero
Kuna simulizi maarufu sana ya MSAMARIA, nina uhakika unaielewa.

Tunasimuliwa kuwa Msamaria alimsaidia yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi, akamfanyia huduma ya kwanza na kumpeleka Hospitali na kumlipia gharama, na akaagiza kuwa kama kungekuwa na ziada basi angekuja ku-clear wakati akirudi toka huko alikokuwa akienda!

Huyu mtu kwa kitendo chake cha kumpenda mtu asiyemjua na kumsaidia, anaendelezaje himaya ya kujipenda mwenyewe?

Huoni kwamba hii inapinga dhana yako?
 
Last edited by a moderator:
PakaJimmy bado kuna upendo wa kristu hadi akakubali kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine. Sasa siamini mtu anayejipenda anawezaje kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine.

Biblia inaassume kila mtu ni selfish Fulani (anayejipenda) na ndio maana inawashawishi watu wawapende wenzao kwa kipimo hicho hicho wanachojipenda. Sasa kama kweli kila mtu anajipenda, basi hakuna mtu angemchukia mwenzake kwakuwa kigezo cha kumpenda mtu ni kuweza kujipenda wewe.

Mimi ninafikiri wanaojipenda wenyewe sana, they are very weak n insecure inside au wanakosa upendo ndio maana wanatumia nguvu nyingi sana kujipenda.
 
Last edited by a moderator:
nakubaliana na Kaunga ,watu wanaojipenda sana huwa selfish na hawawezi kutoa upendo huohuo kwa wenzao,instead inakuwa its all about wao yan wao wanaona wanastahil kupendwa ila hawapaswi kutoa kwa kipimo kilekile!
 
havipingani, aliyesimulia kisa mkasa hicho ndiye alisema mpende jirani yako kama nafsi yako - hakusema mpenda zaidi ya nafsi yako, alisema kama nafsi yako, yaani sawa sawa na nafsi yako.

ukimpenda mtu kama nafsi yako chochote ambacho uko tayari kukifanya tayari kwa nafsi yako utamfanyia, na kwa kuwa unampenda kama nafsi yako utakuwa tayari kutoa nafsi yako kwa ajili yake kwa kuwa unaipenda kama yako.
 
nakubaliana na Kaunga ,watu wanaojipenda sana huwa selfish na hawawezi kutoa upendo huohuo kwa wenzao,instead inakuwa its all about wao yan wao wanaona wanastahil kupendwa ila hawapaswi kutoa kwa kipimo kilekile!

wewe na kaunga mna maana tofauti, hapa tunaongelea kujipenda kwa maana ya kutojichukia - mtu anayejichukia hawezi kumpenda mtu mwingine, atampendaje wakati hajui kupenda, yaani, hajui hata kujipenda yeye mwenyewe.
 
PakaJimmy bado kuna upendo wa kristu hadi akakubali kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine. Sasa siamini mtu anayejipenda anawezaje kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine.

Biblia inaassume kila mtu ni selfish Fulani (anayejipenda) na ndio maana inawashawishi watu wawapende wenzao kwa kipimo hicho hicho wanachojipenda. Sasa kama kweli kila mtu anajipenda, basi hakuna mtu angemchukia mwenzake kwakuwa kigezo cha kumpenda mtu ni kuweza kujipenda wewe.

Mimi ninafikiri wanaojipenda wenyewe sana, they are very weak n insecure inside au wanakosa upendo ndio maana wanatumia nguvu nyingi sana kujipenda.

nimeshalijibu hilo ila ngoja niliweke katika mahesabu labda litaeleweza zaidi

kumpenda mtu kama nafsi yako ina maana:

nafsi yako = nafsi yake

kukiwa na ajali ya meli na imebakia boya moja tu la kuvaa unakuwa tayari kumuachia mwenzake alivaa, apone wewe ufe kwa sababu kwako hakuna tofauti kati ya kuokoa nafsi yake na kuokoa nafsi yako mwenyewe, unazipenda zote.

yesu alitoa nafsi yake kwa ajili ya nafsi zetu kwa kuwa alitupenda kama anavyojipenda yeye - upendo wake ulikuwa ni mwendelezo wa upendo alio nao kwa nafsi yake.
 
Compareno,

Hii mada yako inanirudisha moja kwa moja katika makala ya juzi ya BBC kuhusu "Narcissism" iliyozungumzia Freud "His Majesty The Baby" concept, mythology ya Kigiriki ya Narcissus na kanuni ya kwenye biblia ya "Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako"

Kuna uhusiano wowote au ni coincidence tu inayotokana na ile dhana ya "great minds think alike"?

Kama ni katika kuwasilisha dhana ile ile ya kwenye makala, basi lazima ikuwie vigumu kwa sababu hatuna neno linalofanana kimaana na narcissist kwa kuanzia
 
lol, ni coincidence tu. hiyo programu ya bbc sijaiona.freud nimemsoma zamani sana.na biblia sijaifungua kwa muda (niombee kuhusu hilo).hizi ni tafakuri zangu za alfajiri nikiwa kitandani baada ya kuamka.
 
Good for you @ tafakari za alfajiri.

Lazima mapinduzi ya fikira yapatikane kwenye jamii ya Kitanzania mwaka huu, manake alfajiri tu tafakuri hizi, jee ikifika jioni?!

*Kwani na programu yake ilitoka? Mie nilikuwa nazungumzia makala :)
 
nilikuwa namaanisha makala sio programu, sijui chochote kuhusu bbc - huku ni mambo ya fox na cnn tu!

lol, poa, karibu kwenye tafakuri za asubuhi - it is great for great mind to think alike early in the morning!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom