Mantiki ya kuhairishwa kuwashwa kwa mwenge wa uhuru Mbeya inashangaza

nyandulu

Member
Jan 5, 2011
14
0
Jamani watanzania hii nayo yashangaza, kama inavyo eleweka kuwa shughuli za mwenge wa uhuru huratibiwa na wizara ya kazi na maendeleo ya vijana, na kwa mwaka huu ilipangwa mwenge huo ungewashwa katika mkoa wa Mbeya na katika wilaya ya Mbeya na ilitarajiwa kuwashwa kati ya tarehe 27 mei 2011 hapa mkoani na maandalizi yote yalisha fanyika ikiwemo kukusanya michango kwa wananchi wote hapa mkoani.

Ajabu ni kwamba taarifa hivi karibuni na mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndg John Mwakipesile kwa waandishi wa habari ni kuwa shughuli hiyo imehairishwa na sasa Mwenge huo wa Uhuru utawashwa mwezi Oktoba huko Butiama mkoani Mara sababu ya kumbukumbu ya mwasisi wa taifa hili.

Vilevile kusherekea miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika, sina sababu ya kuhoji sababu hizo nazikubali sana, hoja zangu na haya kila mtanzania lazima ahoji

- Je wizara inayoratibu mbio za mwenge haikuzijua sababu hizo mapema kabla ya hawajapanga mwenge kuwashiwa mbeya?

-Je kwanini mkoa uruhusiwe kufanya maandalizi hadi mwisho ndo watoe taarifa ya hairisho?

_Kama kuna sababu nyingine ambayo wizara haijasema ni vema iweke wazi maana kuna taarifa zinazo dai kuwa ni hali ya kisiasa hapa mkoani ndo iliyofanya kuhairishwa( Chadema ina nguvu hapa mkoani ) kwa maana mwenge ungewashwa hapa mkoani na ungezimwa butiama desemba, ingekuwa ni vema pia.

- Wizara hiyo ni vema iwajibike kwa kutokuwa makini,

-Ufisadi mwingine ni huu hapa, katika maandalizi ya kuwashwa mwenge mbeya wananchi walilazimishwa kuchangia, kila kaya Tsh 500, gari zote binafsi
na za biashara hapa mkoani Tsh 10,000. wafanyabiashara Tsh 10,000, wafanyakazi Tsh 2000.

Katika taarifa ya kuhairishwa kuwasha mwenge mkuu wa mkoa alitamka kuwa fedha hizo zitawekwa katika akaunti maalum bila kutaja kiasi cha fedha iliyokusanywa.hizi ni dalili za ufisadi hiyo fedha italiwa bila taarifa.

Hivyo watanzania tuamke tudai hiyo pesa au irudishiwe waliochanga maana lazima kuna orodha ya majina au badala ya kuwekwa katika hiyo akaunti maalumu ipelekwe kusaidia mradi wa shule au zahanati hapa mkoani na ilezwe kabisa katika fedha kiasi kilichopatikana na ni mradi gani utapewa fedha hizo, ninavyo elewa viongozi wa Tanzania wanasubiri tusahau wagawane.

Tuchangamke.
 
hapo kwenye red, ina maana na michango hiyo itarudishwa kwa wananchi au itapelekwa huko Butiama?
 
JK ana alergy na MBEYA, wananchi wa mkoa wa mbeya watayasikia matukio ya kitaifa kwenye redio tu.Ni aibu
kuwatenga watu eti kisa waliinyima ccm kura,shame to you JK!
 
Mambo ya mwenge ni uchawi mtupu, ningekuwepo Mbeya kwanza nisingechangia, maana mwenge unadidimiza uchumi na kuchochea umaskini.
 
Back
Top Bottom