Mantiki inasema mwaka 2015 CCM kitashinda kwa 41% ya kura

chigwiye

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
352
59
Je fikra zile zile zilizokifikisha CCM kwenye asilimia 61 zilizotangazwa na TUME (toka 81% za 2005) bado zinaweza kukiwezesha kushinda mwaka 2015? CCM kinahitaji fikra mbadala ili kiishi au fikra zile zile kiondoke mwaka 2015 na asilimia 41 kama mantiki inavyobashiri.
 
Mabadiliko kidogo tuu, serikali iwatumikie wananchi; kwa sasa waajiriwa mfano halmashauri au mahospitali wako pale kama vile ni miradi yao binafsi na si kutoa huduma. Mfano mzuri ni mgawo wa viwanja Halmashauri ya Arusha vijijini
 
Huko si kushinda,ni kushindwa! halafu ccm itazikwa kabisa baada ya hapo
 
41% si kushinda ni kushindwa hakuna chama kingine kitakachoshindana na CCM zaidi ya CHADEMA, hivyo 41% itakuwa kifo cha CCM
 
Je fikra zile zile zilizokifikisha CCM kwenye asilimia 61 zilizotangazwa na TUME (toka 81% za 2005) bado zinaweza kukiwezesha kushinda mwaka 2015? CCM kinahitaji fikra mbadala ili kiishi au fikra zile zile kiondoke mwaka 2015 na asilimia 41 kama mantiki inavyobashiri.

Naamini, kura za CCM zitaongezeka kwani wamefanya mabadiliko makubwa ya kuweza kurudisha imani kwa wananchi, Kuna uwezekano mubwa sana wa CDM kusambaratika kabla hata ya 2014
 
Huko si kushinda,ni kushindwa! halafu ccm itazikwa kabisa baada ya hapo
Kinyume chake pia chaweza kuwa kweli, bado natafakari nitarudi kuuliza tena humu JF kama niliwahi kusema jambo kama hili.
 
41% si kushinda ni kushindwa hakuna chama kingine kitakachoshindana na CCM zaidi ya CHADEMA, hivyo 41% itakuwa kifo cha CCM

Kama CCM ni 41%, then CDM NI 25%, CUF - 20%, NCCR - 5%, TLP and others - 9%.

Mshindi ni......41% (CCM).
 
Naona umewapendelea kweli, matokeo yatakua kama ifuatavyo;
CDM=54%
CCM=31%
CUF=07%
NCCR=2%
TLP,ADC,...etc=1%
Na 5% zitaharibika.
Matokeo yatatangazwa kwa kuilazimisha tume.
 
Kama CCM ni 41%, then CDM NI 25%, CUF - 20%, NCCR - 5%, TLP and others - 9%.

Mshindi ni......41% (CCM).

Hata wakichakachua vp! Tume yao, polisi wao na tiss wao, bado hawapati hizo asilimia. Quote me!
 
Inawezekana kama katiba itabaki hiyohiyo, kwani hata matokeo ya 2010, yalilindwa na katiba. Mkuu wa kaya hawezi kukiri kwa kinywa, ingawa moyoni anafahamu ukuu wake watokana na mamlaka, nguvu na ukuu aliopewa na katiba. Ujanja ni kupata na wala si kuwahi.
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA
 
Kuwapa asilimia zote hizo ccm watanzania watakuwa wameshakuwa sugu wa kuibiwa.kwani ccm imeshapewa ridhaa mara nyingi tu ya kuongoza nchi lakini kila wanapopewa ridhaa hiyo wanaishia kuwaibia wananchi.wakishitukiwa wanavunja baraza la mawaziri, wanaleta hoja ya kujivua gamba ili waonekane safi.kumbe ni walewale wanao uma na kupuliza wakijuwa fika kuwa wanatuua taraaaaaaaaatibu.
 
Kama katiba mpya itaacha ujinga wa simple majority lolote laweza kuwa jibu. But kama itakuwa kwa 51% kama kwa wenzetu wenye akili basi mshindi anawezapatikana kwa kura ya pili.
 
Watatumia mbinu walizokuwa wanatumia kule Wanakochoma Makanisa, tume itatangaza Magamba kushinda kwa 51% na CDM 49% ili kuwatia matumaini waendelee kukaza mwendo uchaguzi mwingine!
 
Naamini, kura za CCM zitaongezeka kwani wamefanya mabadiliko makubwa ya kuweza kurudisha imani kwa wananchi, Kuna uwezekano mubwa sana wa CDM kusambaratika kabla hata ya 2014

Ndoto za mwendawazimu hizi.
 
ccm haitashinda, siwezi kutabiri CDM itashinda kwa asilimia ngapi, lakini ccm haiwezi kushinda uchaguzi wa rais katika nchi hii kwa miaka ijayo!!!
 
Back
Top Bottom