Manji tena !? - Zabuni ya Manji yaigawa Manispaa ya K`ndoni

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Zabuni ya Manji yaigawa Manispaa ya Kinondoni !
Na Richard Makore






  • Naibu Meya asema matrekta wameyapokea
  • Kauli yake yapingana na Kamati ya Uwekezaji
Jinamizi la ufisadi limeendelea kuinyemelea Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, baada ya kukubali kuuziwa matrekta 27 ya kuzoa takataka yasiyokuwa na viwango kutoka kwa mfanyabiashara, Yusuf Manji. Dalili za kuwepo vitendo vya ufisadi zimeonekana wazi baada ya Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo ambalo ndilo lililopitisha zabuni hiyo kugawanyika katika makundi mawili.
Upande mmoja unaoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Baraza hilo, Julian Bujugo, ulipinga waziwazi kuwa hawawezi kuyapokea matrekta ya Manji kutokana na kutokuwa na viwango vinavyotakiwa kwa kuwa, Manji alikiuka masharti ya tenda na yaliyotaka matrekta yanayokidhi viwango.
Bujugo alisema Manji alipewa zabuni ya kuagiza matrekta yenye matairi manane lakini yeye akawapelekea yenye matairi manne kinyume na walivyokubaliana.
Hata hivyo, kauli ya Bujugo jana ilipingwa vikali na Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Ibrahim Kisoki, baada ya kuibuka na kusema kuwa matrekta hayo yana viwango na wamekubali kuyapokea.
Kisoki aliiambia Nipashe kuwa wamemwagiza Manji kuongeza idadi ya matairi katika matrekta hayo hadi yafikie manane ili yafanane na maelekezo ya zabuni waliyompa.
Kauli hizo mbili kutoka ndani ya Baraza la Madiwani ambalo ndilo lililopitisha zabuni hiyo, zimezua mkanganyiko na kujenga dhana kuwa huenda kuna upande mmoja umepata ushawishi na kumlegezea masharti mfanyabiashara huyo ili kuweka mambo yake sawa.
Baada ya kukabidhiwa matrekta hayo, Bujugo alitangaza wazi kuwa madiwani wa Manispaa hiyo hawadanganyiki hata mtu akiwapa rushwa, lakini siku moja baadaye Naibu Meya, Kisoki aliibuka na kumtaka afute kauli yake.
Wakati Bujugo akitoa kauli hiyo, pia alimtaka Manji kuyaondoa matrekta hayo katika eneo la Manispaa hiyo ndani ya siku saba, lakini matrekta hayo bado yanahifadhiwa katika eneo la Manispaa ya Kinondoni licha ya muda huo kupita.
Kisoki jana aliliambia gazeti hili kuwa, Bujugo hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo na kwamba yeye (Kisoki) ndiye aliyetakiwa kusema kama matrekta hayo yalikuwa hayafai au la.
Alisema Manispaa imeamua kuyapokea matrekta hayo licha ya kuwa yana mapungufu na masharti ya zabuni yamekiukwa.
Aliongeza kuwa wamempa Manji miezi miwili ili ayafanyie marekebisho ya kiufundi, ikiwemo kuyaongezea matairi kutoka manne yaliyonayo hadi kufikia manane kwa kila trekta.
Kisoki alisema matrekta hayo kwa sasa yapo kwenye yadi ya magari ya magari ya Manispaa hiyo yakifanyiwa marekesho na kuongeza kuwa yatakuwa tayari baada ya miezi miwili.
Naibu Meya huyo alisisitiza kuwa licha ya baadhi ya madiwani katika Baraza hilo kukataa kupokea matrekta hayo lakini yeye ameyapokea na akadai kuwa haoni kama yana matatizo yoyote. Mbali na tenda hiyo ya Manji ambayo imezua utata na kuwagawa madiwani, pia hivi karibuni Manispaa hiyo ilituhumiwa kuuza eneo la kituo cha mabasi cha Makumbusho.
Kashfa nyingine zilizowahi kuikumba Manispaa hiyo ni pamoja na kuuza kiwanja cha shule ya Msingi Kawe kwa mwekezaji.


Manji, Patel, Rostamu, Somaiya n.k. Mapanya yaliyoshiba - kaazi kweli kweli !!
 
gademu! yaani hakuna hata mafisadi wapya... yaani watu wale wale tu? grrrrrr!
Kwanini tusianzishe timu mpya ya ufisadi mimi na wewe? Unajua mzee wewe ungekuwa enzi zile za kina Mkwawa na wewe kichwa chako leo tungelikuwa tunakitembelea makumbusho!Lol
 
Kwanini tusianzishe timu mpya ya ufisadi mimi na wewe? Unajua mzee wewe ungekuwa enzi zile za kina Mkwawa na wewe kichwa chako leo tungelikuwa tunakitembelea makumbusho!Lol


unajua sijui inaudhi au inafurahisha maana kila tukizunguka tunakutana na watu wale wale inakuwa kama ule wimbo wa 2Pac "everywhere I go, i see the same.. "
 
unajua sijui inaudhi au inafurahisha maana kila tukizunguka tunakutana na watu wale wale inakuwa kama ule wimbo wa 2Pac "everywhere I go, i see the same.. "
Identity yetu kama watanzania tumeipoteza baada ya kuridharau Azimio la Arusha. Imagine binadamu asiye na aina yoyote ya utambulisho!
 
NSSF, tanesco, jiji kila sehemu ni yeye halafu ni bomu.
who is this manji???? na kwanini ana kiburi hivi???
 



Manji, Patel, Rostamu, Somaiya n.k. Mapanya yaliyoshiba - kaazi kweli kweli !!

More like yasioshiba na alafu asipotimiza hiyo ahadi sijui ndio inakuaje? watampeleka mahakamani kudai hela yao kwa kuvunja terms of his contract? na achukue matrekta yake. harudishe posho yao au la ndio ushakuwa uporaji mwingine wa mchana mchana.
 
unajua sijui inaudhi au inafurahisha maana kila tukizunguka tunakutana na watu wale wale inakuwa kama ule wimbo wa 2Pac "everywhere I go, i see the same.. "


Kuna yule mfanya biashara maarufu aliwahi kusema mafisadi Tanzania hawazidi wangapi vile? 10 sio...mlidhani alikuwa anatania.
 
Haya mambo ndiyo yanazidi kutupa sura sahihi ya CCM. HAwawezi kubisha kabisa ndio wanaowaweka madarakani, wako kazini kukusanya pesa za uchaguzi wa 2010
 
Hivi huyu naibu meya amekwenda hata shule ya vidudu au anaongea utumbo tu??

Yaani gari kutoka specification ya matairi manne mpaka manane, ni suala dogo tu la kurekebisha kama kuchange rangi ya gari, au ni suala zito la mfumo mzima wa engine, chasis, weight capacity, axle blah blah???

Ama kweli Tanzania tunawazimu sisi wote na viongozi wetu!!!
 
Hivi huyu naibu meya amekwenda hata shule ya vidudu au anaongea utumbo tu??

Yaani gari kutoka specification ya matairi manne mpaka manane, ni suala dogo tu la kurekebisha kama kuchange rangi ya gari, au ni suala zito la mfumo mzima wa engine, chasis, weight capacity, axle blah blah???

Ama kweli Tanzania tunawazimu sisi wote na viongozi wetu!!!

...sijui hata kama alishawahi kutengeneza gari la maboksi. maana hata hilo nalo inabidi ujue sehemu utakapotoboa ili kuweka chelea kama axle kwa ajili ya matairi ya ndala au visoda!!!!
 
Kubadilisha trekta ambalo limeundwa kutumia tairi nne na kulifanya litumie tairi nane sio kazi rahisi kama madiwani hao wanavyofikiria. Tungekuwa na kiwanda cha kutengeneza trekta ha Tz ningeweza kuwaelewa. Hawa madiwani wajaribu kufikiria kuijeuza Hiace ambayo ina tairi moja moja nyuma na kuzifanya ziwe mbili mbili! Kitakachotakiwa kwanza ni kutoa differential housing yote na kuweka nyingine ambayo sehemu za kufunga tairi zitakuwa ni pana ili kuweza kubeba tairi mbili. Na ili kufanya hivyo, itabidi kufanya modification ya vitu vingi na hata jinsi ya kuifunga differential hiyo mpya. Sijui kama Manispaa hiyo ina wahandisi Mchundo (Mechanical Engineers) la sivyo waombe ushauri. Kwa kifupi sio rahisi kuzifanya trekta hizo zifunge tairi nane badala ya nne. Ama kweli hii ni Bongo
 
Mhindi ametuingizia miti nyuma ya miili yetu.tumekuwa speechless,stupid

Rekebisha kauli yako la sivyo mimi nakuruka,kwani mimi ni mkristo kamili hivyo kuingizwa kitu nyuma ya mwili ni dhambi kubwa ambayo sitoweza kuikabili.Inawezekana wewe na wenzio ndio mnao.....miti.Mimi simo!
 
Hivi kuna kampuni hata moja linamilikiwa na manji lime-be-registered MANJI? maana naona sasa tunaandika kama hatujaenda shule why do you address an entity which has not done any business with u?
 

Manji, Patel, Rostamu, Somaiya n.k. Mapanya yaliyoshiba - kaazi kweli kweli !!


Mag3 umemsahau Jitu (Jeetu) aliyepewa zabuni ya matrekta ya kilimo kwanza nayo bila ya shaka yakiwasili yatakuwa hayana viwango vya kutumika kwenye kilimo. Mapanya yaliyoshiba ambayo bado yanawatafuna walipa kodi wa Tanzania kwa kasi ya ajabu.
 
Back
Top Bottom