Manji anakwepa hukumu ya EPA?

Kama ni kweli poleni wafiwa wote na hasa Watanzania wenzetu wenye ajira kwenye kampuni zake.
 
Manji yu mahututi arejeshwa hospitali

na Dina Ismail
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MFADHILI wa klabu ya Yanga na mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji, amerejeshwa hospitali na hali yake ni mbaya.

Manji, Jumatatu wiki hii, alianguka ghafla nyumbani kwake, Upanga, akisumbuliwa na malaria iliyopanda kichwani, alipelekwa katika Hospitali ya Aga Khan kwa uchunguzi na juzi asubuhi aliruhusiwa, baada ya kupata nafuu.

Kwa mujibu wa taarifa za kitabibu zilizokuwa zimepatikana, Manji anasumbuliwa na malaria iliyokuwa imepanda kichwani, ikiambatana na msongo wa mawazo na kufanya kazi muda mrefu pasipo kupumzika.

Hata hivyo, juzi majira ya saa 4 usiku, akiwa nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam, mfadhili huyo wa Yanga, hali yake ilibadilika ghafla, hivyo kurejeshwa hospitalini Aga Khan.

Baada ya Tanzania Daima kupata taarifa za kurejeshwa kwa Manji hospitalini, ilifika hospitalini hapo na wauguzi kuthibitisha suala hilo.

Habari kutoka kwa mmoja wa wauguzi, ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini, alisema Manji alifikishwa hospitalini hapo huku hali yake ikiwa mbaya.

Alisema, kutokana na hali kubadilika mara kwa mara, baada ya kurejeshwa, alipumzishwa kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU), ambako alipumzishwa huko hadi jana mchana alipotolewa ICU.

Hata hivyo, Manji bado yu hospitalini akiendelea kupatiwa matibabu katika wodi namba 3 chini ya uangalizi maalumu wa madaktari.

Kutokana na hali yake, tangu aliporejeshwa hospitalini hapo juzi usiku, amekuwa akila kwa kutumia mpira huku kukiwa na ulinzi mkali kutokana na daktari wake kuzuia watu kumuona, isipokuwa familia yake na wasaidizi wake wa karibu.

"Kutokana na tatizo linalomkabili, ni kama mtu aliyechanganyikiwa, hivyo yuko katika uangalizi wa hali ya juu, ndiyo maana amehifadhiwa katika chumba maalumu," alisema mmoja wa wauguzi.

Habari za kuugua ghafla kwa Manji, zimewatia simanzi kubwa wadau wa Yanga ambao jana walikuwa katika hali ya taharuki.

Akithibitisha kurejeshwa hospitalini kwa Manji, Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega, alisema, ni baada ya hali ya mfadhili huyo kubadilika.

Aidha, Madega amezidi kuwasihi wanachama wa Yanga, kutokuwa na hofu zaidi, ingawa wako katika wakati mgumu kutokana na kuuguliwa na mfadhili huyo.

"Ninapenda kuwatoa hofu Wanayanga wenzangu kwamba taarifa hizi zisiwashitue, kwani kuna watu wanazisambaza isivyo, kwa mitazamo wanayoijua wao, Manji anaendelea kupatiwa matibabu, tumuombee kwa Mwenyezi Mungu apate nafuu haraka," alisema Madega.

Mbali ya kuwa mfadhili wa Yanga na kada wa CCM, Manji ni Mkurugenzi wa kampuni za Quality Group, aliyewahi kuwania ubunge katika Jimbo la Kigamboni na kushinda kwenye kura za maoni, ingawa alienguliwa na vikao vya juu vya CCM.

Tangu aingine mkataba wa kuifadhili Yanga, Manji amekuwa msaada mkubwa kwa klabu hiyo kutokana na kujitolea mamilioni ya fedha hata zaidi ya mkataba. Habari ambazo zilitufikia wakati tunakwenda mitamboni, zilisema kuwa, mfadhili huyo wa Yanga, alisafirishwa kwenda mjini Nairobi, Kenya kwa matibabu zaidi.
 
Manji ni Mzima na yupo Nairobi na anazungumza. Jambo la ajabu, ametokea ICU na hawezi kuzungumza lakini leo ameongea na mtu kwa simu akiwa MZIMA WA AFYAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!! Wajinga ndio waliwaaaaoooo!!!!!!!!!!!! Mwanyika, Mwema, Hosea.... Kalabahooooo!!!
 
Manji ni Mzima na yupo Nairobi na anazungumza. Jambo la ajabu, ametokea ICU na hawezi kuzungumza lakini leo ameongea na mtu kwa simu akiwa MZIMA WA AFYAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!! Wajinga ndio waliwaaaaoooo!!!!!!!!!!!! Mwanyika, Mwema, Hosea.... Kalabahooooo!!!

Ina maana hii ni danganya toto ili aepuke tuhuma mbali mbali za kifisadi zinazomkabili?

Kama kweli amefariki basi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi na awape wafiwa subira na faraja wakati huu mgumu kwao.
 
Mhh jamaa akifa itakuwaje ukarabati wa uwanja wetu wa Kaunda? Jengo la klabu yetu? Madega itakuwaje???
 
manji haumwi maleria wala nini...habari za uhakika kuwa alikunywa sumu akitaka kujiua.. more details to come. na sababu za kunywa sumu zinafahamika tayari
 
....kama kweli amefufa YANGA watakuwa wamelipa kafara kubwa sana kwa ushindi wao wa kupanga...maana wamezoea kina mzimba kutoa kafara walalahoi.....kama hajafa ...Mungu amjalie maisha marefu.....aache kufuru!....

uwezekano kuwa anakimbia pia its another option...
 
Manji ni Mzima na yupo Nairobi na anazungumza. Jambo la ajabu, ametokea ICU na hawezi kuzungumza lakini leo ameongea na mtu kwa simu akiwa MZIMA WA AFYAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!! Wajinga ndio waliwaaaaoooo!!!!!!!!!!!! Mwanyika, Mwema, Hosea.... Kalabahooooo!!!

Mkuu Halisi kwa hili umeniacha hoiiiiiiii maana sijambulia kitu, unamaana gani mkuu?
 
Mkuu Halisi kwa hili umeniacha hoiiiiiiii maana sijambulia kitu, unamaana gani mkuu?

KAGODA=MANJI+ROSTAM AZIZ

EPA KAMATI=MWEMA+HOSEA+MWANYIKA

EPA KAMATI-KAGODA=MANJI MAHAKAMANI

MANJI MAHAKAMANI+USANII WA KIKWETE=MAHABUSU

MAHABUSU*MADAWA YA KULEVYA=MANJI KUTOROKA

Asha
 
Kwani ilikuwaje, Muungwana si alisema jamaa wamepokwa pasi zao za kusafiria?
 
Kifupi Manji yu hai, Period! Yaliyobaki ni uchimvi.

Mod badilisha title ya hii thread au iondoe kabisa kwani inadanganya.

NN
 
Kama yupo hai inabidi arudi na kutubu pamoja na kuwarudishia watanzania vile alivyowadhulumu.

Pia inabidi ajue sasa wananchi wamefikia hatua ya kukosa hata ule moyo wa huruma kwake.Hisia zilizoonyeshwa na baadhi ya wachangiaji wa huu mjadala hapo juu bila shaka ni reflection ya hisia za watanzania walio wengi kama hii habari ni ya kweli au kama kifo chake kingetokea wakati wowote.

Pia inabidi mafisadi wengine pia wajionee na wajisahihishe kabla nao hawajafikia huko.


Pia,sijui waliosambaza hizi habari kama ni za uzushi walikua wanamaanisha nini hasa.Watanzania inabidi tufike mahali tubadilike sasa.


Kama ni kweli basi Mungu amlipe kadiri ya matendo yake.Amen
 
manji haumwi maleria wala nini...habari za uhakika kuwa alikunywa sumu akitaka kujiua.. more details to come. na sababu za kunywa sumu zinafahamika tayari

Mkuu kama umezifahamu hizo sababu zilizopelekea Manji kunywa sumu si uziweke hapa hadharani.........
 
Kwani ilikuwaje, Muungwana si alisema jamaa wamepokwa pasi zao za kusafiria?

Kwahiyo wewe uliamini hivyo? Pole ndugu yangu,Manji ni mzima hii ni kutupoteza[distraction].Kuna watu wenye msimamo kama Mugabe alipoulizwa na viongozi wa SADC kwanini Tvangirai hana paspoti akajibu hamna karatasi za kutengenezea paspoti Zimbabwe hahaha!
 
Mkuu kama umezifahamu hizo sababu zilizopelekea Manji kunywa sumu si uziweke hapa hadharani.........

kwa taarifa fupi kwa kati ya mengi yanayo msibu ni kuwa jamaa ana madeni ya million of dollars and sehemu alipokuwa anategemea azilipie pameguma...
 
Hata mimi nimesikia kutoka kwa watu wa Gymkana na watu wa Yanga, tena wote viongozi waandamizi wanaoheshimika. Si jambo jema la kufurahia lakini tuangalie haya madawa, sheria inasemaje?

wamiliki na waagizaji ndo haohao... wanawatuma vijana wetu wayalete, sasa na wao yanawaathiri
 
Kifupi Manji yu hai, Period! Yaliyobaki ni uchimvi.

Mod badilisha title ya hii thread au iondoe kabisa kwani inadanganya.

NN

Heshima mbele mkuu, kwani huoni heading ya hii thread? kuna message inayosambazwa kwenye mitandao mbali mbali kuhusu swala hili na ndo maana nikapost hii thread kwa heading ya tetesi na kuomba kama kuna mwenye ukweli atuwekee hapa tupate kujua nini kinaendelea sasa kama wew euna uhakika kuwa yupo hai ni vyema ukatueleza kinaga ubaga kama umewasiliana na mtu wa karibu na Manji au wewe ni mmoja wa wafanyakazi wake au wewe ni mmoja wa ndugu zake lakini si kwa kuchimba mikwara kuwa thread inapotosha.........

kama itathibitika kuwa hakuna ukweli juu ya hili MODS ruksa kuiondoa
Hope u understand
 
Kifupi Manji yu hai, Period! Yaliyobaki ni uchimvi.

Mod badilisha title ya hii thread au iondoe kabisa kwani inadanganya.

NN

Heshima mbele mkuu NN, kwani huoni heading ya hii thread? kuna message inayosambazwa kwenye mitandao mbali mbali kuhusu swala hili na ndo maana nikapost hii thread kwa heading ya tetesi na kuomba kama kuna mwenye ukweli atuwekee hapa tupate kujua nini kinaendelea sasa kama wew euna uhakika kuwa yupo hai ni vyema ukatueleza kinaga ubaga kama umewasiliana na mtu wa karibu na Manji au wewe ni mmoja wa wafanyakazi wake au wewe ni mmoja wa ndugu zake lakini si kwa kuchimba mikwara kuwa thread inapotosha.........

kama itathibitika kuwa hakuna ukweli juu ya hili MODS ruksa kuiondoa
Hope u understand
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom