Yusuf Manji amshitaki Reginald Mengi, adai fidia Sh1/-

Je Mahakama ya Tanzania katika kufuata sheria za Tanzania kwenye kesi ya Madai (kama hii ya Manji Vs. Mengi) inaweza:

a. Kuita ushahidi
b. Kuita mashahidi
c. Ku compel both of them?
Labda Mengi hatokuwa na haja ya kuita mashahidi...
 
Mzee Mwanakijiji,

Na wewe kwa upotoshaji kweli umekubuhu, ukija pewa nafasi sitashangaa nikiona unakuwa worse kuliko hata hao akina Rweyemamu. Katika mjadala wote huu sijaona mahali popote palipokufanya uje na conclusion kama hiyo unless kama lengo ni ku SPIN.

Kama nilivyosema mimi sio mwanasheria ila nimeona cases nyingi tu ambazo mashahidi wanaotakiwa na upande mmoja au mwingine hawafiki mahakamani na case inaendelea.

Mfano juzi tu hapa case ya prof. Mahalu ambayo mashahidi mbalimbali wa serikali wameshindwa kwenda mahakani na hakimu akaamua case iendelee.

Angalia pia Milosovic naye alitaka mashahidi kibao lakini akaambiwa wao sio relevant kwenye cases husika.

Mimi nakumbuka hata wakati wa case ile ya wale waliotaka kumpindua Nyerere, mashahidi wengi ambao waliomba waje mahakamani, hawakwenda.

Sasa nitashangaa kweli kwenye case ya madai kama utaweza kumuita mtu yeyote unayemtaka bila kuonyesha sababu za msingi za kuwepo kwake. Kwa mfano ili uweze kusema Manji ndiye alirudisha pesa za Kagoda lazima uwe na ushahidi kuonyesha hivyo, ushahidi ambao umepatikana kwa njia halali. Hapo ni bank iliyopokea au wale waliokuwa wanapokea hizo pesa, vinginevyo mahakama itakataa kumwita shahidi huyo.

Case ya mafisadi ingekuwa na maana kama Mengi na wengine tunaopinga mafisadi ndio tungeifungua case na sio vinginevyo. Kwasasa kazi kubwa ya kuhakikisha madai ya ufisadi iko kwa Mengi na wala sio kwa hao mafisadi.

Pia Mengi ni wrong person kupigana hii vita ya ufisadi kwasababu ni rahisi sana kuonyesha kwamba kwa njia moja ama nyingine kuna ugomvi na wahusika hasa Manji. Huo ugomvi wao binafsi whether ni kwenye biashara au huko Yanga, sio tu unawagawa watu bali pia unashusha uzito wa case.

Hawa mafisadi ilitakiwa wafikishwe mahakamani na watu ambao wako clean kwenye suala zima.

Ninakuwa na wasiwasi kweli na hawa watu wanaowashauri viongozi wetu au wafanyabiashara maarufu. Huenda kwasababu hao viongozi wetu hawaambiliki au washauri wetu ni opportunists na wanaangalia boss anataka nini kisha kwenda na wazo kama hilo. Mshauri ambaye ni huru angeweza kabisa kumwambia Mengi timing sio nzuri.

Vinginevyo hata mimi nasubiri hiyo case. Tatizo tu Mengi akishindwa tayari atakuwa ameua case nzima na hawa mafisadi na itakuwa ngumu sana kwa mtu mwingine kuwavaa.

Ahsante sana Mtanzania kwa analysis yako. Kusema kweli mimi nimefuatia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Dilunga na WoS. Ni wazi kabisa wawili hao walikuwa wanaeleza kitu ambacho wanakifahamu na si kubabaisha. Upande wa pili Mkjj ameonekana kupwaya katika kufanya arguments zake na sikushangaa sana badala ya kuwa muungwana na kuthamini muda na michango ya wawili hao, aliishia kupotosha kama kawaida yake.
Ni vema tukajifunza kuwa wakweli na kuthamini uwezo wa wenzetu katika fani zao. Si kila mtu anajua kila kitu (kama alivyo Mkjj), tukubali kuelimishwa pale ambapo hatuna utaalam na hii ndiyo njia bora ya binadamu kutawala mazingira yake. Kwa wataalam wa sheria kuijua sheria siyo kupata digrii pekee bali pia wanavyoshiriki katika shughuli mbalimbali za kila siku katika kazi zao. Sasa akina sisi sheria tunaisoma pale tunapokuwa na ishu, tena ishu yenyewe tunataka favor upande wetu, kwa hakika huwezi kuambua kitu ni sawasawa na kusoma JHC novels.
Pia nadhani ni vema tukajikumbusha kuwa nia ya kuwepo kwa JF si kutumikia au kupendelea kundi fulani, tujenge spirit ya kuangalia mustakabali wa nchi yetu katika misingi ya sheria, haki na usawa. Tukosoe pale ambapo ni lazima na sababu za kufanya hivyo zipo bila ya kumwonea mtu aibu, upendeleo au kumvunjia heshima na utu wake. Tusibebe ushabiki na kupotosha jamii kwa ajili ya ubinafsi wetu au kwa sababu tu unatakaku-take side.
Mwisho, ninalaani vikali wale wote ambao wanafanya mambo bila ya kufuata na kuzingatia taratibu za kisheria kwani wanaonesha kujijengea misingi ya maisha katika jamii hii kana kwamba sheria zilizopo haziwahusu wao.
 
Kwa kuwa mimi sio learned fellow hiyo ndio ilikuwa tafsiri yangu na nadhani itakuwa ya watu wengi zaidi. Naomba nisaidie hivi hizi gharama tunazozisikia huwa haziangalii uharibifu uliotokana na kashfa yenyewe? Kwa mfano iwapo aliyekashfiwa ni mfanyabiashara na pia anaheshima fulani katika jamii fidia yake haiangalii hili pia. Hivi ni kweli unaamini Manji anataka kutumia haki yake ya kisheria tu na si kunakubwa zaidi analotaka kutuambia kupitia kesi hii? Hii haki ya kisheria kuna wakati watu huitumia vibaya japo hawavunji sheria(mifano kibao ipo)

Mfano wakitu kingine anachotaka kueleza?
 
Pia nadhani ni vema tukajikumbusha kuwa nia ya kuwepo kwa JF si kutumikia au kupendelea kundi fulani, tujenge spirit ya kuangalia mustakabali wa nchi yetu katika misingi ya sheria, haki na usawa. Tukosoe pale ambapo ni lazima na sababu za kufanya hivyo zipo bila ya kumwonea mtu aibu, upendeleo au kumvunjia heshima na utu wake. Tusibebe ushabiki na kupotosha jamii kwa ajili ya ubinafsi wetu au kwa sababu tu unatakaku-take side

Support: 100%
 
Dah naona kizunguzungu kweli.
jeuri ya fedha ndo inatawala hapo. FIDIA YA SHs 1? what on earth? au ndo kuweka rekodi za guiness?
anyway mie nakodoa macho naagiza mahindi ya kuchoma kiloba na bilauri la maji.

I love the way Mengi alivyowafrem wezi wetu. na nimependa sana jinsi mheshimiwa Simba alivyomjibu kwani imeonesha nani yu upande wetu na nani anacheza ngoma yao iitwayo NGOMA YA KISHENZI (nukuhu: Mpoto - salam kwa mjomba)
 
Mimi nakerwa sana na wahalifu wanapotaka kutumia vyombo vya sheria (Law and Its due procedures) kujinufaisha na kuficha ukweli.
Nadhani wakati umefika wa kuchukua hatua:-
  • Wana JF nawahisi kwa nguvu na moyo kutumia "network na connections" zote kukusanya ushahidi utakao thibitisha madai ya R Mengi
  • Kushawishi watu Kujitoa na kuhudhuria hiyo kesi kwa wingi wetu
Wakati umefika kuonyesha kuwa TZ inawenyewe
 
Mimi nakerwa sana na wahalifu wanapotaka kutumia vyombo vya sheria (Law and Its due procedures) kujinufaisha na kuficha ukweli.

Nadhani wakati umefika wa kuchukua hatua:-
  • Wana JF nawahisi kwa nguvu na moyo kutumia "network na connections" zote kukusanya ushahidi utakao thibitisha madai ya R Mengi
  • Kushawishi watu Kujitoa na kuhudhuria hiyo kesi kwa wingi wetu
Wakati umefika kuonyesha kuwa TZ inawenyewe


Sidhani kama JF iko hapa kwa ajili ya kumfanyia mtu kazi.

Tuhimize rule of law kwani nchi hii si ya wana-JF bali ni ya watanzania wote.

Tujenge mawazo ya kuifanya hii ni nchi bora kwa watoto wetu watakaozaliwa kesho.

Kukumbusha, utawala wa sheria unamlinda kila mtu hata yule ambaye tayari ametiwa hatiani.

Kwa kumalizia everyone is innocent until proven guilty in the competent court of law.

Mwisho kabisa, tujifunze kufanya mambo kwa kufuata na kuzingatia sheria na taratibu na wala si jazba

kwaheri!!!!
 
Nilivyo na chuki na hawa wahindi mafisadi, hata mimi niko tayari kupanda kizimbani. Nitaomba nafasi kwenye chombo kimojawapo nibomoke kuhusu ufisadi wao. Tena kwa kuwataja kwa majina pamoja na washiriki wao, nione kama na mimi wataniongezakwenye list yao ya madai ya sh.1.
Basi watushitaki sisi hapa jf kwanza maana kama kuchafua si tumewachafua sana?

Kisha wamshitaki na Dr Slaa. Kwani wamesahau kwamba aliwataja kule Mwembechai? Hii ya kutishana kila siku na mahakama wakati ni wezi wa mchana hatuiogopi tena. Inahitaji spirit ya tofauti kupambana na ufisadi. Yaani uwe tayari si kufilisika na kufungwa bali hata kufa.
 
well well well;




na hapa anazungumza mwanasheria?



sheria gani inafuatwa wakati nimesema sheria inayofuatwa ni ipi.. sijui ni kitu gani kinawafanya mfikiri sheria ya Tanzania haipi nguvu mahakama kwenye kesi za madai kuita mashahidi au kuitisha ushahidi.. somebody show me mtu ambaye siyo mwanasheria. Naomba mwanasheria anioneshe please.


Wala usisumbuane nao badala ya kuangalia attachment ya hivyo vifungu wao wanakalia kuw haiwezekani. Your comments should base on the articles in previous pages not what u think. Ili kama hizo article siyo zenyewe tujue au kama aziapply tujue...
 
Napata hisia hili suala la mafisadi papa linatavalishwa sura ya kibaguzi/kidini ili kuupotosha umma wa watanzania, ni bahati mbaya sana watu wengi waliopata fursa ya kuzungumza na vyombo vya habari (redio na tv) mfano Mh. Simba na ile mizee ya Yanga hawakuzungumzia mada iliyomezani (ufisadi) bali waliwazungumzia watu. Tusubiri tuone.
 
Sidhani kama JF iko hapa kwa ajili ya kumfanyia mtu kazi.

Tuhimize rule of law kwani nchi hii si ya wana-JF bali ni ya watanzania wote.

Tujenge mawazo ya kuifanya hii ni nchi bora kwa watoto wetu watakaozaliwa kesho.

Kukumbusha, utawala wa sheria unamlinda kila mtu hata yule ambaye tayari ametiwa hatiani.

Kwa kumalizia everyone is innocent until proven guilty in the competent court of law.

Mwisho kabisa, tujifunze kufanya mambo kwa kufuata na kuzingatia sheria na taratibu na wala si jazba

kwaheri!!!!

JF haimfanyii mtu kazi bali tupo hapa kutoa changamoto kuakikisha what is right is done! Kama kuna watu wapo tayari kutoa ushaidi wa ufisadi then kwanini wasitoe ushirikiano kwa mengi? Au yoyote ambaye atafunguliwa kesi na who we believe are fisadi? Tanzania inaitaji ushirikiano kama tunataka kweli kesi za ufisadi zimaliziwe mahakamani kwa haki. We all know Tanzanian judiciary system is corrupted and hence we should start be realistic and realize that ‘everyone is innocent before court’ say applies only in the countries where the judiciary system are not corrupted and play fair game.

So it is up to sisi wanaJF kufikiria njia za kukusanya evidence na kuzitoa kwa mtu ambaye huyo tayari kufungua ( au amefunguliwa) kesi kuhusu hawa mafisadi. JF iwe ni chombo cha kuhamashishana.
 
JF haimfanyii mtu kazi bali tupo hapa kutoa changamoto kuakikisha what is right is done! Kama kuna watu wapo tayari kutoa ushaidi wa ufisadi then kwanini wasitoe ushirikiano kwa mengi? Au yoyote ambaye atafunguliwa kesi na who we believe are fisadi? Tanzania inaitaji ushirikiano kama tunataka kweli kesi za ufisadi zimaliziwe mahakamani kwa haki. We all know Tanzanian judiciary system is corrupted and hence we should start be realistic and realize that ‘everyone is innocent before court’ say applies only in the countries where the judiciary system are not corrupted and play fair game.

So it is up to sisi wanaJF kufikiria njia za kukusanya evidence na kuzitoa kwa mtu ambaye huyo tayari kufungua ( au amefunguliwa) kesi kuhusu hawa mafisadi. JF iwe ni chombo cha kuhamashishana.

"We all know Tanzanian judiciary system is corrupted and hence we should start be realistic and realize that ‘everyone is innocent before court’ say applies only in the countries where the judiciary system are not corrupted and play fair game."

Very contradictory statement, if you don't have faith with judiciary system why do you wanna go before it? Nadhani ungeweka statement nzito ya kukataa kwenda mahakamani, na hapo ndipo ningekushangaa kabisa...as I said before, tunatumia jazba zaidi kuliko kuangalia taratibu zilizopo.
Mwisho sahihisha hiyo statement yako uliyoanza 'We all know...' kwani ninaimani huna hoja ya kuweza kuitetea popote pale.
 
Hapa patamu! Mengi kawapiga mkwara alijua hawawezi kwenda mahakamani wataogopa mambo kufichuka, sasa wao wameenda!!!
Mengi's move now!
 
kwi kwi comedi drama... tusubiri kesi... hii itatuchekesha wengi.

Maybe Mr Mengi ana evidence kwi kwi
madai ya namna hiyoo yapo ila hapa kwetu ni mapya...kudai fidia shs 1.

manji jamani hivi wao na mengi sasa bifu lao ni zaidi tujuavyooooo?????

naona ana mawakili tena wenzetuu wanamtetea kweli!! ni biashara au kukosa uzalendo?? nina taarifa ile kesi ya ulipuaji wa marriot hotel india yule gaidi aliyepona kupata WAKILI ILI TABUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU....
 
Kisha wamshitaki na Dr Slaa. Kwani wamesahau kwamba aliwataja kule Mwembechai? Hii ya kutishana kila siku na mahakama wakati ni wezi wa mchana hatuiogopi tena. Inahitaji spirit ya tofauti kupambana na ufisadi. Yaani uwe tayari si kufilisika na kufungwa bali hata kufa.

Hawawezi kumpeleka Slaa mahakamani au kumdai fidia ,ndugu napenda uelewe kuwa kinachotokea hapa ni mapambano ya kambi ndani ya CCM na si kingine chochote kile ,na wala si kwamba wanaupigania ufisadi ,hio ni tiketi tu ya kugandamizana ndani ya chama chao ,au kwa zaidi ni amjungu ya wao kwa wao ,hivi unataka kutuambia Mengi alikuwa hawafahamu hao mafisadi tokea walipokuwa hawajatajwa na walipotajwa na akina Slaa ? Na kwa nini alikuwa Bubu mida yote hiyo mpaka juzi na jana jambo ambalo limeshapigiwa makelele zaidi ya mwaka sasa na kesi za rangi za kinyonga na miondoko yakobe zipo mahakamni.

Kitu kimoja ambacho inabidi mukielewe ikiwa mpo WaTz mnaofuatilia siasa za Tanzania ,Hamasi ni chama kilichoasisiwa na Wayahudi(Kama mnaifuatilia) ili kujipenyeza ndani ya kambi za wapelestina kwa kasi na kujua mambo ya ndani ya Wapalestina lakini baada ya kupenyeshwa kikageuka na kugeuza kibao ingawa bado kuna majasusi wanatumika wakiwemo ndani ya Hamasi lakini sehemu kubwa imebadilika na kuwa na itikadi za Kipalestina na hivyo kuwapa tabu wayahudi.

Sasa Hapa petu moja ya ujasusi uliopenyezwa ni hiki CHADEMA ,hiki kinasemekana ni pandikizi la CCM katika vyama vya Upinzani ,hapo awali yake lakini katika kutamukiwa kumetokea mapinduzi na kuibadili nia iliyokusudiwa na Chama Tawala kusoma harakati za vyama vya upinzani lakini ndani yake humo Chadema kuna waliowatiifu na kwa za CCM kwa maana wamebaki na nia ile ile japo huwezi kuwaelewa kwa kuwa dili limebadilika inabidi wajifiche na kuonekaana ni CHadema damdamu .

Sasa kumetokea mpasuko ndani ya CCM (Kambi za ndani ya CCM) ,hapa wale majasusi inabidi waonyeshe ni upande gani walioko ambao kusaidia kwao kambi hiyo ndiko kunakojitokeza hivi sasa ,hivyo angalieni sana mtaona kuwa maficho na rangi ya CHADEMA huwa inajitokeza tokeza na kufifia kwa maana WACHADEMA wamechanganyikiwa hawajui wapi pa kushika ila inaonekana kuwa CHADEMA wapo upande wa mafisadi kila awapo Kikwete na Chadema unaikuta kuwepo huko ,Zitto alikubali mitambo inunuliwe ,hapa palitokea kutofahamiana na Slaa ,Mengi nae anawapinga mafisadi na kumuunga mkono Kikwete Slaa anaonekana kumuunga mkono Mengi ,hivyo utaona migongano hii inatokana na kuwepo majasusi ndani ya Chadema ambao wanatoa sapoti kwa kiasi fulani pale mambo yanapoonekna yanataka kuingia doa ,tutaona makubwa tu maana ,kuna watu wamekaa pembeni wanaangalia miondoko ya Chadema na kumsifia pamoja na kumkingia kifua Mengi CCM nambari one.
 
mbona mnaoneklana kama hamna habari huku ndani wakati ilitoka kwenye taarifa ya habari chanell ten na aliyeongea alikuwa wakili wa manji akasema eti manji ni mtu mwenye utu sana ndio maana anadai sh moja lakini wakili wake naye alikuwa anaongea kwa uoga na kutokujiamini hata alikuwa haeleweki mi nilifikiri anatania nikasubiri kuona kama taarifa ya habari ya asubuhi habari hiyo itarudiwa haikutoka tena maana nilifikiri naangali ze comed wakati jamaa aasema hivyo

habari ndio hiyo
 
mbona mnaoneklana kama hamna habari huku ndani wakati ilitoka kwenye taarifa ya habari chanell ten na aliyeongea alikuwa wakili wa manji akasema eti manji ni mtu mwenye utu sana ndio maana anadai sh moja lakini wakili wake naye alikuwa anaongea kwa uoga na kutokujiamini hata alikuwa haeleweki mi nilifikiri anatania nikasubiri kuona kama taarifa ya habari ya asubuhi habari hiyo itarudiwa haikutoka tena maana nilifikiri naangali ze comed wakati jamaa aasema hivyo

habari ndio hiyo

Kita, uoga wa wakili ni aibu, kwasababu anajua ukweli asilimia miamoja ukweli ni kwamba mteja wake ni papa la mafisadi, na uthibitisho upo wa kurejesha hela za Kagoda! nidhamira tu mkuu ilikuwa ina msuta!
 
Manji leo amefungua kesi mahakama ya kisutu akidai amekashifiwa na Mengi. Anamtaka Mengi amlipe fidia ya sh1 kwa kumkashifu na kuandaa kipindu maalum cha kumuomba radhi ambacho atakuwa akikirusha (Mengi) mfululizo kwa siku saba

Wakuu hiyo shilingi moja ni symbolic, issue ni kuwa anataka eti 'asafishwe' na Mahakama.
Hapo ndipo mazee inatakiwa kuwa makini sana na proceedings kwani zile issue za NSSF na PSPF zilishawahi kuwa kwenye media.

Wajua ni raha tu wakipelekana Mahakamani kwani kila kitu sasa (ikiwemo na uozo) vitaanikwa.

Tukae mkao wa kula!
 
Back
Top Bottom