Manji akumbwa na balaa

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,921
31,161
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, inatarajia kumfikisha mahakamani mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Manji, kwa kukabidhidhi matela ya kubebea takataka yaliyo chini ya kiwango.
Nia hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Manispaa hiyo na Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo, ambaye alibainisha kuwa, halmashauri hiyo ilimpatia zabuni ya kuagiza matela mfanyabiashara huyo, lakini ameshindwa kulinda makubaliano ya mkataba.
Alisema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Manji hana nia ya kupeleka matela yenye viwango vinavyohitajika au kurejesha kiasi cha shilingi milioni 324 alichopewa kwa ajili ya kazi hiyo.
Bujugo alisema matela 27 yalikusudiwa kusambazwa katika kata zote za wilaya hiyo ili kuiweka manispaa hiyo katika hali ya usafi.
Alisema Manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (Septemba – Desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi Novemba mwaka huu.
“Zabuni hiyo ilikuwa ni ya kipindi cha miezi mitatu, lakini Manji alikiuka utaratibu huo ambapo imepita zaidi ya mwaka ndiyo anatuletea matela hayo yasiyo na ubora,” alifafanua Bujugo.
Aidha, alisema halmashauri katika mkataba wake na Manji, ilitaka matela yenye matairi manane, lakini mfanyabiashara huyo aliwapelekea matela yenye matairi manne.
“Sisi tuna ushahidi wa kile tulichokiagiza katika makubaliano yetu. Tulihitaji kuletewa matela yenye matairi manane, amechukua muda mrefu anatuletea matela ya matairi manne, hatuyataki,” alieleza.
Alisisitiza kuwa, kamati yake na halmashauri haikuwa tayari kupokea matela hayo na kumshauri Manji kutimiza kile walichokubaliana katika mkataba husika.
Alisema hivi sasa kuna mbinu chafu na ushawishi unaofanywa na mfanyabiashara huyo kwa baadhi ya madiwani ili wakubali kuyapokea matela hayo.
Alibainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilitoa siku saba kwa Manji kuyaondoa katika eneo yalipowekwa matela hayo na kuleta yale yanayokidhi viwango.
Alidai kwamba pamoja na agizo hilo, mfanyabiashara huyo alishindwa kutimiza masharti aliyopewa, jambo lilioifanya manispaa kufikiria kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha jambo hilo linamalizika.
Tanzania Daima Jumatano lilijaribu kumtafuta Manji ili kuzungumzia sakata hilo, lakini simu yake ya mkononi ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake.
Msaidizi huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Manji hakuwepo ofisini huku akilitaka gazeti limuachie maagizo ili akirudi ampe.
“Ninaomba uniachie ujumbe nitamfikishia na kama atakuwa tayari najua lazima atakupigia,” alieleza msaidizi huyo.
Hata hivyo, msaidizi huyo alishindwa kutimiza ahadi hiyo ambapo hadi Tanzania Daima Jumatano linakwenda mtamboni, hakuna simu yoyote iliyopigwa na Manji.

Chanzo Tanzania Daima.
 
ujinga mtupu..mwaka mzima walikuwa wapi kumpeleka mahakamani?
 
ujinga mtupu..mwaka mzima walikuwa wapi kumpeleka mahakamani?

Mkuu, haya matatizo yapo sana kwenye procurement maana suppliers hulazimisha kukidhi viwango sometimes wakiwa hawana uhakika na source... asbabu nyingine ni corruption, unaweza kukuta mtu kashakula halafu kahamishwa... pia hii ya kuchukua muda kabla ya kwenda mahakamani, inategemea mlolongo wa mawasiliano

ila kwa kweli hii ni nyingie ya ufisadi uliopo karibu kila halmashauri hapa Tz, wanapewa pesa nyingi sana lakini efficiency na capacity ya kufuata taratibu ni questionable

ningekuwa na uweza ningebadili mfumo

Hivi hayo matela waliagiza mapya au used?
 
Ufisadi tu....mkataba ulikuwa ushavunjika pale Manji aliposhindwa ku-deliver matera hayo katika muda uliokubaliwa....!
 
Huwa najuuliza watu wanatoa wapi hizi pesa za kutanulia,magari ya bei mbaya kumbe ni tenda mbovu kama hizi ambazo mtu anachukua pesa anazizungusha then anarudisha kwa kuleta vitu ambavyo havifai.lkn bw baba akiwa mbovu na familia nayo huwa hovyo,hivi top meya ni msafi kweli?
 
Manjis wakati mwingine anashangaza kweli anatuibia fedha zetu halafu anakwenda Jangwani anatoa fedha kiduchu kwa Yanga kwania ya kujipatia ujiko kumbe ni lijizi tu.
 
Mkuu, haya matatizo yapo sana kwenye procurement maana suppliers hulazimisha kukidhi viwango sometimes wakiwa hawana uhakika na source... asbabu nyingine ni corruption, unaweza kukuta mtu kashakula halafu kahamishwa... pia hii ya kuchukua muda kabla ya kwenda mahakamani, inategemea mlolongo wa mawasiliano

ila kwa kweli hii ni nyingie ya ufisadi uliopo karibu kila halmashauri hapa Tz, wanapewa pesa nyingi sana lakini efficiency na capacity ya kufuata taratibu ni questionable

ningekuwa na uweza ningebadili mfumo

Hivi hayo matela waliagiza mapya au used?

maneno yako yamenigusa sana kaka..hii nchi bana we acha tu unaweza ukalia
 
Manjis wakati mwingine anashangaza kweli anatuibia fedha zetu halafu anakwenda Jangwani anatoa fedha kiduchu kwa Yanga kwania ya kujipatia ujiko kumbe ni lijizi tu.

sasa mbona wanazipokea hizo hela za uwizi.na wao majizi
 
Huyu manji ni mtu hatari sana, yaani anaharibu kila mahali na bado wazidi kumpa tenda kwa fedha za walipa kodi. Kuna haja ya ku-blacklist watu kama hawa kwenye manunuzi.:mad:
 
Huyu manji ni mtu hatari sana, yaani anaharibu kila mahali na bado wazidi kumpa tenda kwa fedha za walipa kodi. Kuna haja ya ku-blacklist watu kama hawa kwenye manunuzi.:mad:

Mkuu ndiko anakoelekea, blacklisting on the way!!! BTW, kwanini tunasema blacklisted why cant we say whitelisted??
 
Ufisadi tu....mkataba ulikuwa ushavunjika pale Manji aliposhindwa ku-deliver matera hayo katika muda uliokubaliwa....!

Kwani walimlipa kabla hajaleta hayo matreiler? Kama bado si wakanunue sehemu nyingine na wasipokee hayo yake.
 
Mkuu ndiko anakoelekea, blacklisting on the way!!! BTW, kwanini tunasema blacklisted why cant we say whitelisted??

We are taking too long. Kaanzia NSSF kachota, PSPF n.k tulisikia habari za billion 90. Bado tu still on the way mkuu?

Naona hapa amekua whitelisted.
 
Nadhani atakwenda nunua difu za ziada aje afunge hapo kwenye tela kisha anaya mwagia rangi na kuwafisadi madiwani ili ngoma zinafanye kazi Manispalia kama kawaida..!!
 
Maneno mirefu mitendo hamuna - Give us the court summons and not these blaa bla za kuuza magazeti. Where were they all those 11 months? Why now? Dont they have meetings/forums to discuss this? Is this guy represent Mayor or Director?

Muda wa maneno uliisha - show us something different.
 
Nadhani mkataba hapa haupo! Hata hayo matela aliyoleta kimsingi yameletwa kukiwa hakuna mkataba! Kama alipewa pesa in advance, arejeshe na utaratibu wa kumpata mzabuni mwingine ufuatwe!
Failure to deliver within specified time in the contract is a bleach of contract and there should be a penalty that has been clearly stipulated in this contract (They should refer to their Special Conditions of Contract/Contract Data and Conditions of Contract for this particular supply contract)
 
Manjis wakati mwingine anashangaza kweli anatuibia fedha zetu halafu anakwenda Jangwani anatoa fedha kiduchu kwa Yanga kwania ya kujipatia ujiko kumbe ni lijizi tu.

Kwenye hili usiseme mkuu. Mashabiki wa Yanga hawaoni wala kusikia lolote kuhusu Manji. Ziwe ni pesa za wizi au dhuluma mradi ni pesa. It is a pity! Vichwa vyetu wadanganyika inabidi vifanyiwe uchunguzi.
 
Nadhani mkataba hapa haupo! Hata hayo matela aliyoleta kimsingi yameletwa kukiwa hakuna mkataba! Kama alipewa pesa in advance, arejeshe na utaratibu wa kumpata mzabuni mwingine ufuatwe!
Failure to deliver within specified time in the contract is a bleach of contract and there should be a penalty that has been clearly stipulated in this contract (They should refer to their Special Conditions of Contract/Contract Data and Conditions of Contract for this particular supply contract)

wewe unaongea nadharia ndugu yangu, hali haipo hivyo kwenye baadhi ya taasisi zetu, kwenye papers tuko poa sana tatizo ni context nzima humo... hapa inaonekana jamaa alitii mkataba akaleta vitu lakini kumbe ni feki kulinganisha na products specifications alizotoa mwanzo, yes ni breach lakini hapo ni a whole new ball game aisee, hasa kwenye corrupt legal system kama yetu... miaka itaenda taka zinajaa watu wako mahakamani, huyo ndio mpenda nchi anavyotufanya
 
Back
Top Bottom