Manji ajaribu kujisafisha Kashfa ya Kagoda; ajichongea!

Kumbe Manji anamjua mmiliki halisi wa Kagoda kwani alishafanya nae biashara, hivyo kama yeye si mtuhumiwa basi ni shahidi muhimu wa serikali.
 
Nchii hii sasa inapoelekea jela ni za maskini tu, katika hali ya kujibu tuhuma za Msemakweli za kuiba ela BOT kwa kusema eti nilirudisha, this is non-sense and against rule of law.Kubebeana hadi lini? ina tofauti gani na ya JAH- IROO alisafishwa eti hakuchangisha taasisi 20 bali nne tu na eti hakupata BILION 1 bali milion 570? YUPO WAPI DEREVA WA GARI LA TANZANIA? USALAMA JE? CIDs?. bora nmesema hasira imepungua na ctopata laana bali baraka
 
Sasa kaibe wewe kuku mtaani uone kama hujaozea jela,
Hii nchi tunaishi na wahalifu wengi sana mitaani,
Itafika kipindi tutaanza kuwasaidia mahakama kuwahukumu hawa watu kama mahakama zenyewe zimeshindwa!!
 
Ukombozi wa watu hutotokana na watu wenyewe. Sheria na taratibu zote zimewekwa ili kuisaidia jamii husika na wala siyo jamii kuwa watumwa wa sheria.
Inapotokea mfumo wa kutoa maamuzi ya kisheria unatoa upendeleo wa wazi kwa wateule wachache, ni muhimu kufanya mabadiliko makubwa kuanzia kwa watendaji ambao ndio chanzo cha tatizo.
Wananchi wanatakiwa kuelewa kwamba huwezi kuwashughulikia watuhumiwa wa ufisadi mkubwa kabla ya kupambana hadi uwashinde walinzi wao ambao ni watendaji katika taasisi za uma zinazohusika na utoaji haki.
Hali hii ikiachwa iendelee, wananchi watakosa imani na mfumo wa utoaji haki na matokeo yake ni kujichukulia sheria mkononi ikiwa ni pamoja na kuwahukumu watuhumiwa kwa kuwashambulia wao binafsi (hata kuwachoma moto ndani ya mashangingi au makasri yao), kushambulia mali zao kama kuchoma viwanda, majumba, magari, mashamba n.k.
Ni muhimu kwa watuhumiwa kuelewa kuwa wanategemea walinzi wajinga ambao ndio wanaofanya mambo kuwa magumu. Ikumbukwe kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwapeleka mahakamani na baadaye hao walinzi waovu (maadui wa uma) wakatoa ushahidi legelege, au hata hati ya kutoendeleza mashitaka kutoka kwa DPP na hata baada ya hukumu Rais akatoa Presidential Pardon, ili mradi tu sheria imechukua mkondo wake.
Kwa mustakabali mzuri wa watuhumiwa, ni bora wajiunge na uma kuwashughulikia walinzi wao ambao kwa ujinga wao wanazidi kuwasha moto wa maangamizi, ili baadaye wapate hukumu za haki ambao zitakuwa nafuu kuliko kiama wanachoandaliwa.
 
Kitu ambacho mleta habari kashindwa kukielewa ni kuwa kuna grace period ya lini uli lodge kampunimiwe incorporated na lini imekuwa incorporated. Licha ya hayo kuna intention, ambayo inaweza kuambatana na MoU kabla ya kampuni kuanzishwa. Na hapo hizo tarehe na kampuni vimekuwa leaked ili ukivipeleka mahakamani (mwanasheria mbumbu kama anaetajwa) vikugeukie. <br />
<br />
Kwa ufupi, kampuni inaweza kuwepo hata kama haijawa incorporated.
<br />
<br />
TAARIFA YA KAINERUGABA ERICK MSEMAKWELI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WIZI WA DOLA MILIONI 31 ZILIZOFANYA NA MAKAMPUNI YA KAGODA AGRICULTURE LIMITED NA QUALITY FINANCE CORPORATION LIMITED

Baada ya kusoma na kutafakari taarifa iliyotolewa na Yusuf Mehbub Manji kwa vyombo vya habari Septemba 8, 20011 nimebaini kwamba imejaa uongo na upotoshaji mwingi kiasi cha kunilazimu mimi kujibu kama ifuatavyo.

Matusi na kejeli dhidi yangu na hasa elimu yangu.

Taarifa ya Manji imejaa matusi na kejeli dhidi yangu kwamba mimi si chochote, nabangaiza, natumia vitisho ili kujipatia fedha (yaani blackmailer) na ni mtunzi wa vitabu vya kukashifu watu. Haya yote siyo kweli na ni dhahiri kwamba Manji amepatwa na hasira na jazba baada ya kuumbuka.

Niko tayari kwa matusi, kejeli na vitisho na sitorudi nyuma. Lakini angetumia akili yake vizuri angegundua kwamba mimi nina shahada ya sheria ambayo nilitunukiwa 2008.

Kwamba ninatumiwa.

Hii siyo kweli; historia yangu inajieleza. Ari yangu ni uchungu na nchi yangu ambapo watu wanaweza kuiba mabilioni ya pesa wakajulikana na wasichukuliwe hatua. Nilipokuwa naingia kwenye harakati hizi nilijua wapo watu wenye nia mbaya ambao wangenituhumu natumiwa. Manji ni miongoni mwa watu hawa. Lakini watambue kamwe hawatanirudisha nyuma.

Ushaidi wangu kwa DPP. Katika taarifa ya Manji amejaribu kuuaminisha umma kwamba mimi ni muongo na kwamba eti kampuni ya Quality Finance Corporation Limited ambayo anakiri ni yake imetapeliwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited. Huu ni uongo wa wazi.

Manji yuko nyuma ya makampuni yote mawili na kama kawaida yake anataka kuchezea akili za Watanzania. Kwanza kwanini alidhamini Kagoda kufungua akaunti Benki ya CRDB? Kwa nini aliingiza fedha dola milioni 2 katika akaunti ya Kagoda na makubaliano ya fedha hizi yako wapi?

Ilikuwaje aingie mkataba na kampuni ambayo haijasajiliwa? Nyaraka zinaonyesha Kagoda ilisajiliwa na Msajili wa Makampuni Septemba 29, 2005 wakati mkataba wa kukopeshana ambao Manji anataka tuuamini umesainiwa Septemba 12, 2005. Manji anatakiwa kufahamu kwamba kurejesha mali ya wizi ni wajibu na siyo fadhila kwa maana ukisharejesha hauwezi kushatikiwa.

Tanzania bila ufisadi inawezekana. Watanzania tuthubutu kuwafichua na kuwaanika mafisadi. Ningependa kuwashauri Watanzania wote wenye ushahidi au taarifa za ufisadi wazipeleke kwenye vyombo vya sheria kama nilivyofanya mimi.


Kainerugaba Erick Msemakweli

Dar es Salaam

Septemba 9, 2011
 
Kitu ambacho mleta habari kashindwa kukielewa ni kuwa kuna grace period ya lini uli lodge kampunimiwe incorporated na lini imekuwa incorporated. Licha ya hayo kuna intention, ambayo inaweza kuambatana na MoU kabla ya kampuni kuanzishwa. Na hapo hizo tarehe na kampuni vimekuwa leaked ili ukivipeleka mahakamani (mwanasheria mbumbu kama anaetajwa) vikugeukie.

Kwa ufupi, kampuni inaweza kuwepo hata kama haijawa incorporated.

Siamini kuna mtanzania yoyote mwenye kumtetea Manji katika hili; labda iwe ni wakili aliyelipwa kufanya hivyo. Kwa maana hiyo basi, kwa namna unavyomtetea huyu jamaa, hata akinya utadaka kinyesi chake na kusema kinatoa harufu ya manukato.......
 
Kudeal na ufisadi Tanzania ni zaidi ya kupita kwenye tundu la sindano. Ukisoma hii thread utaona unafiki wa kiwango cha kutisha cha the so called waTanzania wazalendo!
Thank you,unafiki wa hali ya juu, thread kama hivi wanazipita kimya kimya kwa aibu
 
Siamini kuna mtanzania yoyote mwenye kumtetea Manji katika hili; labda iwe ni wakili aliyelipwa kufanya hivyo. Kwa maana hiyo basi, kwa namna unavyomtetea huyu jamaa, hata akinya utadaka kinyesi chake na kusema kinatoa harufu ya manukato.......
Tatizo lako ni elimu tu. Ni mahaka gani imemtia hatiani?
 
Kuna watu tunawapa madaraka wanafanya mambo ya ajabu hadi aibu. Halafu huyu mama mtaalamu wa kurekebisha istilahi za kiswahili mbona anawatetea sana wapiga will.

Ili ufungue akaunti benki wadhamini/mdhamini ni wakurugenzi /mkurugenzi wa benki. Aliedhamini kagoda kama kweli ndio mmiliki

Ila BOT kuna ukwasi sana maana white elephant project zote hizi bado wako kimya
 
Back
Top Bottom