Manji ajaribu kujisafisha Kashfa ya Kagoda; ajichongea!

Yusuf Manji, jamaa katajirika kwa mipesa yetu wenyewe, nashangaa wanaomsifia eti anatumia walizoacha babu zake.
Mzee Mahboob kafia Marekani, nasikia alikimbia moto hapa, si ajabu hata mwane naye akaanza.
 
Aaaah Bossi, vipi tena mkuu??? Active members zaidi ya 15,000 kati ya members 47,000 tushindwe kuzipelekesha hizi thread sambamba??!!

Unaogopa sauti za "man on, man on" uwanjani, utaweza kweli kubutua mpira walau nje ya goli??!! lol

mkuu
actually nilichotaka tutumie nguvu pia kujadili wizi wake unaondelea now
sisemi tusijadili kabisa ya kagoda..
yuko behind karibu kila kitu cha dili za halmashauri ya jiji
why?kwa sababu kawachagua yeye hao madiwani na meya wao...
umenipata?
 
To be honest ya manji na kagoda naona ni old news kwangu.

tukiendelea kujadili wizi wa 2005 wakati kuna wizi mwingine unaendelea ni busara kweli?
?

Yote yatajadilika tu mkuu, but we have to start somewhere as in 2005?
 
Hawa wahindi zamani walijifanya wajuvi sana sasa mambo yao yanazidi kuwekwa hadharani ona anavyojibu utadhani mtoto wa darasa la pili barua nzima imejaa maneno ya hasira utafikiri anamjibu mpenzi wake.
 
mkuu
actually nilichotaka tutumie nguvu pia kujadili wizi wake unaondelea now
sisemi tusijadili kabisa ya kagoda..
yuko behind karibu kila kitu cha dili za halmashauri ya jiji
why?kwa sababu kawachagua yeye hao madiwani na meya wao...
umenipata?

mkuu weka thread yenye data hapa uone kama hatapona, kuna neno anapenda sana kuchafuliwa
kila kitu kuchafuliwa, hali anafanya biashara na wachafu halafu yeye tu ndio msafi, mmmmmmmmmmm
 
Mkuu! toka liniFISADI akawa SMART? ama mkweli akapindisha? unakumbuka tume ya uchaguzi na takwimu za wapigakura? TISS huwa hakuna u-smart kwenye uongo o ufisadi. DAIMA UTAJICHANGANYA
 
Well,

Barua haiko signed basi ni CHAKA... Umeangalia tarehe za registration ya Kagoda na ukaangalia makubaliano ya mkopo toka Kagoda kwenda Quality Finance? Do you see my concern? Wala mi sina shida na yeye kupinga, ana haki na si vema kuchafuliwa kama anajua yeye ni msafi. Tatizo langu ni ninapoangalia hizi TAREHE mkuu wangu

Hawa watu inaonyesha wazi kabisa kwamba wamekuwa wakicheza hii michezo michafu kwa muda mrefu na hawakuwahi kufikiria kwamba iko siku mambo yatafumuka, as long wana deal na wakubwa wa serikali kwahiyo walikuwa wanajifanyia mambo tu kiholela bila kuweka umakini.

Labda usikute hata huo usajili wa brela umefojiwa tu ili ku cover irregularities ambazo "zingewafunga" kama wangeonekana kufanya biashara huku wakiwa hawana uhalali wa kisheria wa kufanya shughuli.

Kwahiyo utaona kwamba mkataba kati ya kagoda na quality finance umemchoma kisu cha moyo ze alwatan yusuf manji.
 
Wakifikishwa mahakamani ndo watasema ukweli. Sasa hivi wanatapatapa tu. Hawajui hata ku-forge documents
 
Wakuu,

Yusufu Manji katoa taarifa yake kama inavyoonekana chini hapa... Huenda vyombo vya habari nyumbani vikatumia taarifa hii lakini ieleweke kuwa haijasainiwa, tarehe za usajili Kagoda, tarehe za usajili Quality Finance na tarehe za mikopo zimejichanganya mno... You need to be smart when playing such games!

Sasa ndugu yangu Manji, hivi Kagoda na loan kipi kilitangulia? Mkopo kabla ya kampuni au kampuni kabla ya mkopo?

Hapa umejichanganya mkuu wangu, mnaweza kuangalia namna ya kuiweka sawa hii?

Asante Invi, wee ni mwisho!. Hawa jamaa kwa kawaida wako very smart in paperwork and playing with peoples mind, sijui this time walibugi step vipi?!.

Tena ukifuatilia zile transfer pesa ikichotwa BOT, ni siku hiyo hiyo inahamishwa, hailali benki na ikilala ni siku moja!.

Njia ya mwongo ni fupi!
 
mkuu
actually nilichotaka tutumie nguvu pia kujadili wizi wake unaondelea now
sisemi tusijadili kabisa ya kagoda..
yuko behind karibu kila kitu cha dili za halmashauri ya jiji
why?kwa sababu kawachagua yeye hao madiwani na meya wao...
umenipata?

Isiwe nongwa mkuu, kama una data za kutosha ama kama hazitoshi kama una kianzio we anzisha thread tu uone wenye nondo watakavyoishukia.

Tusipende kujenga tabia ya kutaka kuibua mambo mapya tu kila siku wakati yale ya zamani bado hayajakamilika.

As long yusuf manji ameshiriki kutuhujumu na serikali haijamchukulia hatua stahiki, ataendelea kukumbushwa ufisadi wake mwaka baada ya mwaka hadi pale tutakapojiridhisha kwamba kimeeleweka.
 
Itajulikana tu kama yumo au hayumo, anyway sio lazima yeye awepo anawatumwa wake wanamjulisha.

Huu mchezo wa kukanusha vitu bora kukanusha na kuweka personal attack ndani yake bila ushahidi kutawamaliza wengi.

Again kwa huu utumbo ni wazi kabisa Manji ni fisadi, ina maana anataka kusema ana ugomvi na KAGODA, kwa sababu alirudisha hiyo hela serikalini?

Ni nani huyo Kagoda anayemzungumzia Manji maana kaweka kama mzimu flani tu kwa sababu yeye anawajua awaweke hadharani anaogopa nini?

Manji hawezi kukana tuhuma za Msemakweli kirahisi hivyo; kwanza kama Msemakweli anakutishia kukulipua kisha ukampa hela ina maana alichokutishia ni cha kweli, hii ina kuhusu wewe wala usiseme ni watu.

Mwisho, uhusiano wake na KAGODA uko wazi na ameukiri sasa Msemakweli kakosea wapi? Hakuna aliyekuwa anajua kwamba Manji alikuwa ni mdhamini wa KAGODA yaani mafisadi, na kwa kutumia mwanya huo alifungua kesi kumshitaki Mengi, sasa hapa hatajibu vipi hizo tuhuma kwamba yeye sio part ya mafisadi.

Ni kwa biashara zipi za mabilioni KAGODA walimwambia wanafanya hapa nchi na yeye kuingia nao mkataba na kupokea hela bila kujua zinatoka wapi?

Cha kuongezea mkuu,
Yeye Manji alijuaje kuwa kuna kampuni inaitwa Kagoda na kwenda kukopa ili hali kampuni haikuwepo? Pili kwa nini hakuenda kukopa benki na badala yake akakope kampuni ambayo haipo. Nani aliyemwambia kuwa kagoda wana pesa za kukopesha makampuni au kagoda ilikuwa Benki?
 
Mdogo wake atakuja na majibu sasa hivi. Kaeni mkao wa kula

Lahaullah!! Naona wana JF tumejitahidi kumrudisha kundini huyu muasi.

Ninalo moja kuhusu hili: Ukiona kila mtu anapayuka na ukweli hata akitokea anayepinga huwa hana nguvu wala hasikilizwi. Usemi wa busara Mwita 'even if you do not like us, but atleast do not hurt us' na mwisho 'kama huna pointi basi jaribu hata kuungana nasi, tunapigania uzalendo na sio chama kama wewe, liangalie uso mbayaaa....
 
Kitu ambacho mleta habari kashindwa kukielewa ni kuwa kuna grace period ya lini uli lodge kampunimiwe incorporated na lini imekuwa incorporated. Licha ya hayo kuna intention, ambayo inaweza kuambatana na MoU kabla ya kampuni kuanzishwa. Na hapo hizo tarehe na kampuni vimekuwa leaked ili ukivipeleka mahakamani (mwanasheria mbumbu kama anaetajwa) vikugeukie.

Kwa ufupi, kampuni inaweza kuwepo hata kama haijawa incorporated.
 
manji anajua kiswahili?
Anakijua sana akishikwa pabaya hata kizaramo atazungumza, wanazuga tu! Kuna GM wangu wkt napiga mzigo Oceanic Bay alikuwa anatuzuga hajui swahili! Akawa akituudhi tunatukana matusi!we utastukia anakuita ofsini umuelezee kwanini ulimtukana na mambo meengi kama hayo, wanazuga tu wanajua vizuri!
 
Back
Top Bottom