Manji aibuka sakata la UDA, azidi kumkaanga Masaburi

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group Yusuf Manji, amesema maombi ya kampuni yake kutaka kuingia ubia na Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa gharama ya sh bilioni 1.5 hayakujibiwa. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, alisema hadi sasa hajui sababu za kukataliwa kununua hisa 49 za UDA, licha ya kufanya juhudi za makusudi kujua kwa nini maombi hayo hayakujibiwa licha ya kuwa mwombaji pekee.

Amesema kuwa ukimya huo uliilazimu Quality Group kuandika barua kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi Abdallah Kigoda na ile Hesabu za Mashirika ya Umma Zitto Kabwe. “Barua yetu ilizingatia ukweli kwamba tulishiriki katika tenda mbili za UDA ile ya mwaka 2005 iliyoshirikisha kampuni tatu na nyingine ilirudiwa mwaka 2007 ambayo kampuni yetu pekee ilishiriki.

“Katika tenda ya mwaka 2007 tulieleza kuwa tupo tayari kuingia ubia wa UDA kwa gharama ya sh bilioni 1.50 kwa ununuzi wa hisa 49 pia tulieleza kwamba itakuwa ni uwekezaji wa dola milioni 10 za Marekani kwa ajili ya kurabati karakana. “Pia tulieleza kwamba tungeleta mabasi 150 chini ya utaratibu wa mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART)…tulifanya hivyo kwa kuzingatia kwamba tunao uzoefu wa miaka 30 katika sekta ya usafiri,” ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo ambayo nakala yake Tanzania Daima inayo.

Shirika la UDA kwa sasa linaendeshwa na kampuni ya Simon Group ambayo, umiliki wake umezua balaa kiasi cha kuamriwa kusimamishwa kwa muda kujihusisha na maamuzi makubwa ya uendeshaji. Katika hatua iliyozua tafrani, Simon Group hivi karibuni ilinunua mabasi mapya 30, kinyume na azimio la Baraza la Madiwani la jiji la Dar es Salaam.

Meya wa Jiji, Didas Masaburi, alionyesha kusikitishwa kwake na maamuzi ya kampuni hiyo ya kununua mabasi hayo, na kudai kuwa ni kuvunja amri na maelekezo halali ya madiwani na kwamba atachukua hatua madhubuti kufuatilia sakata hilo.



 
Back
Top Bottom