Manispaa ya Morogoro yaagizwa kulipa Bilioni 10 wanakijiji............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Bil 10/- kulipa fidia Moro

na Joseph Malembeka, Morogoro

amka2.gif
WANAKIJIJI zaidi ya 427 wa eneo la Mgulu wa Ndege, Lukobe na Mzembe Manispaaa ya Morogoro, wanatakiwa kulipwa fidia ya sh bilioni 10 na manispaa hiyo baada ya kushinda kesi ya ardhi namba 117 ya 2009.
Kesi hiyo ilitokana na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi hao na manispaa baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kudaiwa kulazimisha kupima na kugawa viwanja zaidi ya 4,000 katika maeneo hayo bila fidia kwa wananchi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa hukumu hyo, Jaji Longway wa Mahakama Kuu ya Ardhi, Kanda ya Dar es Salaam, alisema madai yaliyotolewa na wanakijiji hao ni ya msingi na manispaa wanapaswa kulipa fidia hiyo.
Katika madai yao tisa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wakili Pascal Gaspar Chuwa, wanakijiji hao waliitaka Manispaa kubatilisha hati za viwanja 4,000 vilivyopimwa katika eneo hilo.
Akizungumzia mgogoro huo, Mkurugenzi wa Halamashauri hiyo, Jolvis Simbeye, licha ya kukiri kuwepo kwa mgogoro huo alisema maeneo yanayogombewa ni mali ya serikali na wananchi walipewa kuyatumia kwa muda kwa ajili ya kilimo na uzalishaji wa mazao mbalimbali yasiyo ya kudumu.
Alisema kutokana na mpango huo, serikali imeamua kupanua makazi na mji katika maeneo hayo ili iweze kukabiliana na kasi ya ongezeko la watu mjini humo.
 
Kauli hii ya DED inaashiria ya kuwa mgogoro huu utatinga Mahakama ya Rufaa tu hakuna namna manispaa hiyo itatenga hayo mapesa siku za usoni........................
 
Back
Top Bottom