Manispaa Moshi kuwalipia ada wanafunzi wote

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Manispaa Moshi kuwalipia ada wanafunzi wote


na Grace Macha na Rodrick Mushi, Moshi


amka2.gif
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi limeanza kazi kwa kufanya mapinduzi makubwa kwenye bajeti yake ikiwamo kupunguza matumizi kwenye mambo yasiyo ya lazima huku ikiazimia kuwalipia ada wanafunzi wote wa shule za sekondari za kutwa.
Matumizi yaliyopunguzwa ni yale ya ofisi ya meya kutoka shilingi milioni 16 zilizotengwa kwenye bajeti ya mwaka 2010/11 hadi shilingi milioni 4.7 kwenye bajeti ya mwaka 2011/12.
Katika bajeti hiyo, kiasi kikubwa cha fedha kimepunguzwa kwenye fungu la chai na vitafunwa kutoka shilingi milioni 10.3 mwaka 2010/11 hadi kufikia milioni 1.8 kwa mwaka 2011/12.
Hayo yalifikiwa jana wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo cha kujadili na kupitisha maazimio ya makisio ya bajeti ya halmashauri hiyo kwa ajili ya mwaka 2011/12. Halmashauri hiyo inaundwa na madiwani wengi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Wanafunzi wa sekondari 8,528 watalipiwa ada ya shilingi 20,000 kila mmoja itakayogharimu halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 170.5 huku wazazi wao wakitakiwa kulipia michango mingine ya shule ikiwamo kulipia wapishi, walinzi na huduma nyingine zinazotolewa kwenye shule hizo.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa manispaa hiyo Bernadette Kinabo, alipingana na uamuzi wa madiwani hao juu ya kuwalipia ada wanafunzi kwa madai kuwa inapingana na sera ya serikali inayowataka wazazi kuwalipia wanafunzi wao ada ili wajisikie wana uchungu na elimu ya watoto wao.
Meya wa manispaa hiyo, Jafar Michael, alisema kutokana na tatizo la ugumu wa maisha wazazi wengi wamekuwa wakishindwa kuwalipia watoto wao ada hali inayoziweka shule katika wakati mgumu wa uendeshaji wa shughuli zake.
Alisema hali hiyo huwasababisha walimu kuwarudisha wanafunzi nyumbani mara kwa mara na hivyo kuchangia kuporomosha maendeleo ya elimu ya wanafunzi hao ambapo alisisitiza kuwa wanafunzi 1,200 wanaoishi kwenye mazingira magumu na yatima wataendelea kulipiwa ada yote ya shilingi 237,000 kwa mwaka.
Meya Jafar alisema wamefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 351 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani ya halmashauri hiyo na kwamba sehemu ya fedha hizo zitatumika kuwalipia ada wanafunzi wote na kuongeza matundu ya vyoo katika baadhi ya shule za sekondari zinazokabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo.
Kikao hicho kinatarajiwa kuendelea leo kwa ajili ya kujadili bajeti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
 
Sidhani kama ni wanafunzi wote kujumuisha hata wale wa private....................................hii sera ya Chadema ninaiunga mkono kabisa................................karo ya shule imefukarisha familia nyingi......................ili kuwatandea haki wale walioko kwenye private skuli yabidi nao wapewe vocha zenye thamani ileile ya skuli fees wanazolipiwa wale walioko shule za serikali ili kuondoa ubaguzi wa kimapato.........................
 
safi sana chadema waonesheni njia wa magamba kwamba inawezekana ukiwa na nia, huyu mkurugenzi wa moshi huwa ni waajabu sana.
walipiwe watoto wa shule za serikali hapa ndio kuna watoto wa wakulima, private wanakwenda kwa mapenzi yao na urefu wa mifuko yao.

mkuu hii si uilete jukwaa la siasa, hapa huwa ni kituo kidogo cha polisi
 
Aliyeenda Private kwa sababu tu serikalini hakufai maana yake anaweza kujisomesha
 
hahaaa CCM si walisema elimu bure haiwezekani au nakosea??? Wazee wa kujivua gamba...budget ya kupioga chai na maandazi 10m...mwaka huu mtatoka na maandazi na uji wa ulezi nyumbani kwenu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom