Manispaa ilala siku maalum ya usafi muanzie ukonga mazizni

masharubu

Senior Member
May 5, 2010
155
10
Nimeona tangazo kutoka manispaa ya ilala ikiwahimiza wakazi wa manispaa hiyo kuwa kila jumamosi ya kwanza ya kila mwezi ni siku usafi ktk manispaa hiyo.

Ninachowaomba kwa hilo kwa kuwa mmekua mkichukua kodi kwa kila n'gombe anaechinjwa hapo lakini usafi hamsimamii wala hamuufanyi na machinjio yanatoa harufu hasa kipindi hiki cha mvua.

Barabara ya kuingia ndani ya machinjio ni chafu kupindukia kiasi kama wadau wa tv wakiwaonyesha jamii hali ya machinjio hawatakula nyama, sasa hiyo alfu kumi kwa kila n'gombe mnayochukua mnachukua kwa ajili ya matumbo yenu.

Hivi ilikuwaje waziri wa mifugo hakupitishwa ukonga mazizini angejionea balaa kushinda la vingunguti, na pia wamekua na ujanja wa kutotengeneza barabara ili watu wasiiende kujionea madudu yao.

Harufu ya damu inayopikwa haivumiliki kiukweli, halafu mnalaumu jamii forum wakati madudu mnayafanya wenyewe.

Meya wa jiji, na manispaa ya ilala mpoo!!!!!!!!!!!??????????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom