WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Kama watu wetu wanalalamika hawana mikate, kwa nini wasile keki?
MKuu WoS, mtu akilalamika anapata shuruba na minyanyaso lukuki kazini huwezi kukimbilia suluhisho la kusema aacha kazi! Hiyo ni kuwa out of touch. Kuna shutuma za mazingira hatari ya kazi, kusafisha $#@& za wagonjwa bila gloves, mishahara inayoendana na kabila, kataka kulalamika hajakaa sawa wamem fire, wewe unamwambia atafute kazi pengine. Kuna haki za mfanyakazi ambazo anajaribu kuzitafuta ndugu yangu.
Kwanza hujui ugumu wa kupata hizo kazi. Pili, hata akiacha kazi, halafu mazingira ya kazi yakabaki hivyo hivyo ni kwamba miaka ya mbele ndugu yako au mtoto wako WoS na wangu wanaweza kuja kufanya kazi hapo. Tutafute haki za wafanyakazi wa nchi yetu, tusiwe out of touch kwa kuwaambia wasio na mikate wakale keki.
1. Naona quotation ya Mke wa King Louis wa Ufaransa kabla ya French Revolution...Marie Anttoinette!
Mimi ni mbangaizaji .. Quotation yako therefore hainihusu maana siko kwenye rulling class ndugu yangu.
2.Ugumu wa kupata kazi naujua sana..na vilevile kwa vile najua ndio maana nikipata kibarua sioni tija kubabaishana na kubishana na mwajiri.Vikinishinda huwa naanza!
3. Haki za mfanyakazi - kuna taratibu zake - akalalamike kuanzia ngazi ya Trade Unions na Labour..kwa kuja hapa wewe Dilunga umemsaidia nini mpaka sasa hivi? Hata mawazo tu hujampa.Bora hata mie nimempa ushauri hata kama kwako wewe na wengine haufai!