Manesi kuanza mgomo leo

Salas

JF-Expert Member
Feb 15, 2009
382
82
Manesi wafunguka, watatangaza mgomo nchi nzima kuunga mkono madaktari vikao vinaendelea
 
Jamani hii sasa ishakuwa hatari...
Kwani raisi anashindwa kuona faida na hasara za kuwalinda hao watu wawili tu?
 
Na mgomo usambae hata na polisi wajiunge na mgomo..........................
 
Sasa hivi utasikia na polisi wamegoma maana swala la afya halina mwenyewe
 
manesi automatically lazima waingie katika mgomo maana wenyewe huwa wanapewa maelekezo na madaktari...sasa bila daktari nesi atafanyaje kazi yake? kikwete analo...!
 
Wakigoma madaktari obviously NA manesi wamegoma, ni sawa na mdomo ukigoma so does the kolomeo,
 
Mbona hili lilikuwa wazi kabisa! Na kama rais atatatoa hotuba sawa na ile ya mbayuwayu leo kwenye mkutano wake na wazee wa Dar basi tujiandae kuona sekta ya afya inakufa kabisa. Mpaka wapishi watagoma!
 
Ninasubiri jambo hili kwa hamu kubwa....manesi wagome rasmi, hata hivyo daktari akigoma automatically nesi hana njia nyingine ni kugoma....maelekezo juu ya tiba ya mgonjwa hutolewa na daktari, ripoti ya maendeleo ya mgonjwa kutoka kwa nesi hupewa daktari. Ni mgomo tu utakaorejesha muunganiko huu.
 
Goosh!
Mke wangu ni Nesi!
Haya mambo taratibu yanajicustomize mitaani na kutuhusu zaidi kila kukicha!...huh!
RIP my wife's profession!
 
Mbona nasikia mahakama itaka mgomo usitishwe?
Au ni propa-gamba?!
 
Mtoto wa mkulima kawazidi ujanja madokta kwa kupeleke ombi mahakamani na shauri kusikilzwa upande mmoja! Sijui kama hiyo ni sawa ila ndo amri imetolewa na lazima drs. Waitekeleze la watashitakiwa kwa kosa la kukaidi amri halali ya mahakama na kufungwa gerezani au kupigwa faini! Ila nadhani gvt wamepata temporary breathing space kwani tatizo liko palepale!
 
Back
Top Bottom