Maneno ya Baba

Heri waliokuwa wanakaa na baba zao wakiongea. Mimi ilikuwa nkitoka shuleni tu nafukuzwa kwenda madrasa kusoma QurAan na Fiqhi. Hadi anafariki hatujawahi kukaa kuzungumza ya kidunya. Lakini kwa hili namshukuru na kumkumbuka sana. That is what has made what I am now. Allah Amweke mahali pema peponi.
 
Yafanyie kazi ,utafanikiwa,
mi huwa natumia yale ya Marijani Rajab ya wimbo wa ''wosia wa Baba''
 
Asante kwa pole, Husn but kwa leo na kwa furaha uliyonayo kwa result unatakiwa upumzike.
Fanya ulale hii mida sio mizuri, ndiyo mida ya Popobawa kuamka na kuanza kuvinjari jukwaa hadi jukwaa, usije ukakumbana nae usiku huu hafai kabisa ukutanenae.

ndio nimeamka sasa. Halafu nafurahi kuona unayafanyia kazi maneno ya baba. Kijana mzuri, sio mkorofi, mcheshi na mstaarabu. Mungu akuongoze.
 
Hongera Judgement kwa kupata malezi ya baba na kikubwa zaidi alikupa usia, binafsi sikujaaliwa bahati hiyo
 
Leonard ! Hakuna mtu wa karibu kwa Mume kama Mke .
Na kwa Mke ni Mume, each other ni ritehand wa mwenzake.
But , But, But !
Pakijatokea ugomvi wa balaa na divorce ikawa establish !
Na kila mmoja akashika njia yake, viumbe hawa hutokea wakawa maadui kiasi kufika hata mmojawao akisikia ex- mwenza kafa hahudhurii hata mazishi ! Ndiyo kwanza anashukuru.
Lakini nduguyo hata mgombanaje undugu haufi wala hauna subsitute (instead of )
Undugu ni kama kabila (tribe) haubadilishiki !.
Mke anabadilishika !
Dini
inabadilishika.
Mke sio nduguyo.

umenigusa sana nimesha shuhudia sakata kama hili.si ndugu hata kidogo ni lafiki tu wa kawaida.
 
Wanawake wote mwalimu wao kipofu ishi nao kwa akili sana hayo ndio maneno aliyoniambia baba ambaye bado nipo nae kwenye uso wa dunia
 
Nianze kwa kumtakia RIP, kwani hatunae katika uso wa ardhi.
Si mara moja au mbili, ni mara nyingi Baba yangu nikiwa tumekaa nae zama za uhai wake, alikua akiyarejelea maneno haya :-
(Nikimnukuu)
Baba > Mwanangu mimi Baba yako nimekua, na nimekutana na mengi.
Katika dunia hii mwanangu ukitaka ufanikiwe kimaisha , ishi na watu vizuri.
Na uweke taswira usoni kwako kua watu ndiyo mtaji wako, na wewe ni mtaji kwa watu wengine.
Hakikisha usibweteke na mali za ndugu zako na ukazitegemea, nenda juu chini umiliki za kwako.
Ishi na familia yako kwa mapenzi, lakini usisahau kua mkeo si ndugu yako.
Na katika dunia hii mwanangu unapokutana na watu (binadamu) ukawasikia mtu anakwambia
"Mimi sipendi wizi kwelikweli "
"Mimi sipendi uongo"
"Mimi sipendi uzinzi"
Basi mwanangu uwasikiapo watu wakijinadi kwa kauli hizo , waangalie kwa macho mawili , kwani hua wanakua ni kinyume na kauli zao.
Anaejinadi hapendi uzinzi basi ndiyo mzinzi nambari one !
Mwanangu wale wenye tabia na mienendo yao mema hua hawajinadi , huvaa silka ya tabia zao kimyakimya na jamii ndiyo huwatambua.
(mwisho wa kunukuu)
Binafsi yangu maneno haya ya Baba yote ninayaona ukweli wake.

Hap kwenye red Marehemu baba sijui alikuwa anamaanisha nini Judgement.

Nadhani kwa mabinti zake wa kike alikuwa anawaambia wanangu mme sio ndugu yako.
 
siku zote mkeo ni rafiki yako wa ndani na mwenzako, katika muungano wa hiyari, na una weza kuwa na mwisho wake ikiwa yatakiukwa masharti ya mkataba huo, hapo sasa maana ya baba utaipata KUWA MKEO SI NDUGU YAKO, kwani baada ya kuundoka kwako atarudi kwa ndugu zake na wewe utabaki na ndugu zako hata kama hamuongei miaka, kwa hiyo hata siku moja mkeo hawezi kuwa ndugu yako MANENO YA BABA NI MSWKI WA MTI HAYITAJI DAWA, ILA FIRSTLADY, MTOTO NA BABA YAKE NI NDUGU WA KIBAOROJIA NA UBINI (utambulisho) na hili kwa wenye akali halina shaka hata kidogo, ila baba amekufa huku akimpenda mke wake inavyoonekana, mungu ndiye anajua baba atalipwa nini kesho akhera , kwa huruma zake na maombi yetu amwingize peponi ,amin
 
Hap kwenye red Marehemu baba sijui alikuwa anamaanisha nini Judgement.

Nadhani kwa mabinti zake wa kike alikuwa anawaambia wanangu mme sio ndugu yako.
hapa ndo napopata picha kweli nyie wanawake sio watu kabisa, hata kuitwa sio ndugu mnapendelewa mngepaswa kuitwa viumbe wa ajabu wa porini tena nyoka.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom