Maneno haya Jenerali kuhusu katiba nimeyapenda

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Mwanazuoni Jenerali Ulimwengu anawaasa wanasiasa anasema hivi...



Yapo mambo yanayowasumbua wanasiasa, ndani ya chama tawala na ndani ya vyama vya upinzani. Haya ni yale ya kiutawala zaidi ambayo ni tume huru ya uchaguzi; utaratibu wa uchaguzi; viwango vya asilimia katika uchaguzi; utaratibu wa uchaguzi; madaraka ya Rais; madaraka ya Bunge; kuwapo kwa waziri mkuu au la, na madaraka yake; uwakilishi wa uwiano (PR); ukomo wa mihula ya uongozi, na mambo mengine madogo madogo kama hayo.

Haya yote ni muhimu lakini hayana uzito kama ule ninaouona katika maeneo mengine mfano Kuwapo kwa Muungano na mgawanyo wa mamlaka na rasilimali baina ya Tanganyika na Zanzibar; mamlaka juu ya rasilimali za nchi kwa ujumla (ardhi, madini, maji, misitu); ugatuzi na mamlaka ya serikali za mitaa na mgawanyo wa madaraka baina ya serikali hizi na serikali kuu; mgawanyo wa rasilimali baina ya wakulima na wafugaji; utamaduni na lugha za asili mkabala na Kiswahili na Kiingereza; mfumo wa elimu utakaojenga Utanzania, na kadhalika.


"Narudia kusema kwamba tusifanye mambo kwa haraka kwani hatuna tunakoenda. Tupo hapa, na tunataraji kuwa hapa kwa miaka milioni ijayo, kama si zaidi. Kwa nini tunafanya mambo kama vile tuko transit tukienda mahali pengine?"- Jenerali Ulimwengu
 
general z r8 nd muungano plus hw we share th national cake ar sensitive matters 2 4rm part of th constitution.
 
jenerali ulimwengu kichwa halafu si mnafiki,ni bonge la hazina lakini serikali haitaki kumtumia,akifa tutajutia.anajua mambo mengi sana huyu mtu
 
Back
Top Bottom