Maneno 4 Muhimu Kwa kupata Penzi la Mwanamke

Huuu ndio ukweli mtupu

Hayo maneno siku hizi hayana nguvu sana kama zamani, siku hizi wanawake wanaangalia zaidi ni kitu gani mwanaume anamiliki au future ya mwanaume huyo ikoje, inalipa au hailipi....
Hujawasikia wakisema kwamba mwanaume asiye na kitu ana kasoro?

Ndio maana wale wanaume wanamudu kujikweza huwabamba sana wadada...

Kizazi hiki sio cha maneno matupu ndugu yangu....
 
BADILI TABIA usijifanye hujui, naomba uwe mkweli wa nafsi yako, hivi unadhani watoto wetu hawa tuliozaa bado wanafuta nyayo za wazazi wao katika kupenda?
Siku hizi maisha yamebadilika sana, hizi tamthilia na mitandao ya kijamii imewafanya mabinti wetu akili zao kupogoka linapokuja suala la kupenda, ni binti gani siku hizi asiyependa mwanaume mwenye gari..?

Kama mwanaume hana kitu ana mtihani mgumu sana pale linapokuja suala la kutafuta mwenza.....

neno hilo! Kuntu
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi kuna asilimia kubwa ya ukweli ktk ulichosema, mwanamke anahitaji security zote; financial, emotion, social etc. Lkn napingana na hiyo ya 'wanawake wa siku hizi'.

Mama yangu aliyeolewa Mwaka 1961, kabla hajaolewa alikuwa anasali apate mchumba au mwalimu au bwana mganga, mchumba wa kwanza alikuwa mwalimu (but it didn't work out), wa pili na wa mwisho was daktari (ambaye alimuoa).
So sijui tunavyosema siku hizi labda tuinclude miaka ya 1950s, maana mtu kutaka muajiriwa nafikiri alitaka pamoja na status lkn financil security (uhakika wa mshahara mwisho wa mwezi). Otherwise nakubaliana nawe hayo Maneno manne hayajitoshelezi siku hizi, kuna pia Dini ambayo wewe ulishaizungumzia; wengi sana wameshindwa kuwa na wapenzi wao kwa kuwa wanaimani tofauti.
Kaunga, niliwahi kuandika kuhusu jambo hilo, na wewe ulichangia kwa mkukubaliana na kile nilichosema, hedu fungua huu uzi na pia soma maoni yako, ulisema nini kuhusu jambo hilo?

https://www.jamiiforums.com/mahusia...nafuata-asili-katika-kupenda%85%85%85%85.html

Ni kweli, unajua kwa mvivu siku zote njaa ni sehemu ya maisha. Lakini, jasiri hata kama kaajiriwa na muhindi kama anavyosema Scofield bado atakuwa na shamba; na si ajabu jioni atakuwa anafua hata vyuma.

So hata kibarua kikiota nyasi; bado ugali wa kila siku utapatikana, wagonjwa watapata matibabu n.k
 
Last edited by a moderator:
Kaunga, niliwahi kuandika kuhusu jambo hilo, na wewe ulichangia kwa mkukubaliana na kile nilichosema, hedu fungua huu uzi na pia soma maoni yako, ulisema nini kuhusu jambo hilo?
https://www.jamiiforums.com/mahusia...nafuata-asili-katika-kupenda%85%85%85%85.html

Nimejikumbusha, kweli tulikubaliana kuwa it is a natural instict so si kitu kipya na si sahihi kusema wadada wa siku hizi; ni wa siku zote.

Nafikiri hata wanyama ni the same, sema report za tafiti za behaviour za wanyama haziko accessible sana.
 
Last edited by a moderator:
Maneno 4 NAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE Kumpata Mwanamke kimapenzi.

Imebainika kwamba, wanaume wanaposaka wapenzi, huwa tayari kutii masharti wanayopewa na upande wa pili. Utii huu ndiyo unaotajwa kumvutia mwanawake kiasi cha kumfanya aamini kirahisi kuwa mwanaume wa maisha yake ni huyo anayemtongoza wakati huo.


Hakuna shaka kwamba, katika mazungumzo ya awali ya mwanaume anayemteka mwanamke kimahaba, kinywa chake huwa hakikauki maneno haya manne zenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambazo ni NAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE.


Ni wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno hao wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi wao. Binafsi nathibitisha hili kwa kuwa nimeshafanya uchunguzi kupitia wanaume wanaonijia kutaka majibu ya kwa nini wapenzi wao wamewageuka na kutokuwapenda kama awali.


Kabla ya kuwashauri nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambua kuwa waliacha kutumia maneno hayo mara tu walipoona amefanikiwa walichokuwa wanakitafuta.

Kama nilivyosema neno la kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni NAKUPENDA. Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke ajiamini.

Neno la pili, NAKUHITAJI. Kama inavyokuwa wakati wa kutongoza, mwanamke anapenda kuambiwa neno hilo

na kufanyiwa vitendo inavyoonesha kuhitajika kwake katika maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa

kimaisha. Sambamba na hilo mwanamke anapenda sana kupewa ASANTE katika yale anayofanya.

Jambo la mwisho kabisa ni SAMAHANI. Ndugu zangu kuna wanaume ambao hawako tayari kuomba msamaha

kabisa hata kama wamekosa kosa kubwa na la wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi. Ni busara kwa

mwanaume kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni mwenye mamlaka na hivyo kuzidisha upendo na uangalizi wa tabia mbaya za mwanaume.


Hakuna neno la tano la POLE?
 
Back
Top Bottom