Mandhari ya Zuhura-Mwezi-Zohali Pembetatu Pacha Alfajiri Alhamisi

Unapendezwa na sayari na nyota angani, yaani astronomia?

  • Hapana

    Votes: 0 0.0%
  • Sielewi

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    9

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
279
202
Mandhari ya kuvutia sana itaoneka angani alfajiri ya Alhamisi hii tarehe 7 Januari, jirani na upeo wa mashariki kuanzia saa kumi na nusu alfajiri. (Angalia picha iliyoambatishwa)

Sayari mbili, Zuhura (Venus) na Zohali (Saturn) zitaonekana pamoja na hilali nyembamba ya Mwezi katika umbo la pembe tatu pacha iliyolala.

Hilali itakuwa upande wa kushoto wakati sayari mbili Zuhura na Zohali zitakuwa karibu yake kwa umbali sawa zikitengeneza pembetatu pacha iliyolala. Zuhura itakuwa juu ikin'gaa mno wakati Zohali itakuwa chini kidogo ikin'gaa kwa utulivu.

Sayari mbili zingine pia zitaonekana katika anga ya alfajiri siku ya Alhamisi. Mushtarii (Jupiter) au kwa jina lingine Sambulaa itaonekana karibu na utosini ikin'gaa kwa ukali sana.

Mirihi (Mars) itakuwa anga ya kati upande wa mashariki ikiwa na uekundu mwembamba.

Sayari zote nne zitakuwa katika mstari mmoja ikionesha kuwa mixing iko ya sayari zote zipo katika bapa moja
============
============

Mandhari ya Zuhura-Mwezi-Zohali.jpg
 
View attachment 315066
Mkuu
Huu mfuatano hautaathiri nguvu za mvutano kuelekea Mushtarii?
Hali ya hewa haitaathirika?

Ni tukio zuri kulishuhudia in lifetime
 
Hapo ndipo napowakubali NASA wao mda mwingi wanautumia kwenye sayansi ya anga wakati sie tunautumia kwa wizi na ngono(refer D.Trump)
 
Sijui ntakumbuka kuamka... mniamshee sawa. Kwani hiyo mandhari itadumu kwa muda gani wakuu??
 
Swadakta ..Allah ndo mjuzi wa mambo yote ambaye ametuamrisha tuelimike ili tuujue utukufu wake.
 
Sijui ntakumbuka kuamka... mniamshee sawa. Kwani hiyo mandhari itadumu kwa muda gani wakuu??

Mandhari ya pembetatu pacha itaonekana alfajiri ya kesho tu, kwa vile Mwezi utasogea upeoni, ila kwa siku chache sayari Zuhura na Zohali zitaendelea kuonekana karibu karibu kwa vile husogea polepole.
 
Mkuu
Huu mfuatano hautaathiri nguvu za mvutano kuelekea Mushtarii?
Hali ya hewa haitaathirika?

Ni tukio zuri kulishuhudia in lifetime

Hali ya hewa haitaathirika kwa vile nguvu za mvutani kati ya sayari ni ndogo mno ikilinganishwa na nguvu kati ya maada Duniani.
 
Huo ukaribu unakuwa wa umbali wa mile ngapi kutoka moja hadi nyingine na kikawaida inakuwaga ngapi zinapokuwa kwenye umbali mrefu ??????
 
Kuna umbali mrefu sana kati ya Mwezi na sayari. Ukaribu tunaozungumzia ni katika muono angani ya vitu hivyo kutoka kwetu Duniani.

Huwa tunaziona zikikaribuana na kupishana angani kwa vile zina zunguka katika mizingo yake.
 
Back
Top Bottom