Mandela na Lema wafanya uamuzi unaofanana - kwenda mahabusu kwa hiari

Matukio hayafanani kati ya lema na mandela,mandela alikuwa anadai uhuru na haki za weusi kwa mikutano na migomo.maandamano ya lema yanadai nini?

Mandela alipewa ofa,afutiwe mashtaka na aache harakati lema hajapewa ofa hiyo kesi bado ipo. Kama mandela angapewa dhamana angetoka kosa lake lilikua halidhaminiki,lema linadhaminika.ni umbumbumbu wa lema na anaowahadaa
Naomba nikusamehe kwa kuwa ni wewe ndiyo huelewi. Swala lakudai haki halina tofouti maana ni uhuru ule ule. Enzi za akina mandela kulikuwa na ukandamizaji wa wageni. Enzi za akina Lema ni ukandamizaji wa ndugu zetu wenyewe waliovaa mavazi ya wakoloni. Ndiyo maana ninasema madai na hali ya lema hayanatofouti na ya mandela.
 
CCM wanajichimbia kabuli kwa kutumia vyombo vya dola kukabiliana na upinzani, wanawapa promo bila CCM kujua.
 
Aweda today, based on this analysis have prove yourself to be a great thinker.
 
Tuwekeni ushabiki kando unawezaje kufananisha kesi ya mandela na lema? Umetumia vigezo gani?
This is crap, wewe msifie lema kwa alichofanya na si kulinganisha na mandela ili kuipa sapoti hoja yako.
Kimsingi hizo ni issue mbili tofauti kabisa, think again
 
Excellent Aweda, kweli ccm wana kazi, kama nyinyi ndo mnajiandaa kujinga na akina lema huko mbeleni magamba wataponaje?
 
Wewe unaota, huwezi kufananisha mchicha na Mbuyu.

MY FRIEND EVERY LEGEND DEAD AND ALIVE THEY STARTED LIKE MCHICHA HALAFU WANAKUWA MBUYU, PIA ULIZA WAKUU WOTE, WANAANZIA PALE WAKUU WENGINE WALIPOISHIA, SOMA KUHUSU BILLGATE ALIANZIA PALE MITS Altair 8800 WALIPO ISHIA YEYE NA ALEN WAKAENDELEZA WAKAPOLISHI WAKAPATA MICROSOFT,
JE UNAJUA TOYOTA WAMEBORESHA MAMBO YA FORD SO POSSIBLE HUYU KIJANA ANAKO KWENDA ANATISHA NA WANAMPA UMAARUFU WA CHEEEEEE
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Serikali nyingi za Afrika zinazima haki kwa wananchi wao kwa kutumia nyezo dhaifu, kama polisi,jeshi, mahakama,udini,kudhuru wanaowapinga au hata kuwaua na kulindana kirafiki. Hizi ndizo nyenzo ambazo ccm na serikali yake inazitumia kuzima harakati za kudai haki kwa watanzania. Wanashidwa kujifunza yanayotokea nchi nyingine mpaka yawakute wao na wanadhani hivyo vitawalinda milele. Ila mimi naamini kwenye ukweli Uongo hujitenga ngoja tuone hii jaja ya serikali dhalimu ya ccm itawafikisha wapi.
 
Some of Mandela and Lema similarities;

Nelson Rolihlahla Mandela
"During my lifetime I have dedicated myself to this struggle of the African people. I have fought against white domination, and I have fought against black domination. I have cherished the ideal of a democratic and free society in which all persons live together in harmony and with equal opportunities. It is an ideal which I hope to live for and to achieve. But if needs be, it is an ideal for which I am prepared to die."
"As violence in this country was inevitable, it would be wrong and unrealistic for African leaders to continue preaching peace and nonviolence at a time when the government met our peaceful demands with force," he says.
"The idea in my mind was not that we were going to win, but that we were going to focus the attention of the world on our demands. "

God Bless Lema

Nilipoona wenzangu hawawezi kupata matibabu nikasema mimi sio mgonjwa, nilipopata taarifa za rafiki zangu kufungwa kwa makosa yasiyo yao, nilipoona watoto wa mitaani wanaomba chakula, nilipoona wazee wamepoteza matumaini ya kuishi katika uzee wao, nilipoona vijana hawana ajira, nilipoona mabinti wasichana wadogo wameamua kufanya biashara ya ukahaba, NIKATAFAKARI,TENA NIKATAFAKARI.

Nimetafakari sana na nikatambua kuwa sababu ni mimi pale nilipokuwa kimya wakati wajane na wanyonge wanaonewa.

Wanafikiri wataendelea kutuogopesha kwa sababu wana jela na silaha, wanafikiri tutaendelea kuabudu uoga, wanafikiri wataendela kutunyanyasabila sababu ya msingi LAKINI SISI TUNAJUA TUTASHINDA KWA SABABU HAKI TUNAYOIPIGANIA NI MAKUSUDI YA MWENYEZI MUNGU.

Leo nitakwenda jela kwa hiari yangu binafsi kwa siku kadhaa na si kwa NIA YA KUJITAFUTIA UTUKUFU WANGU bali ,” JELA NI MAHALI PA KUISHI KAMA SABABU YA KWENDA HUKO NI VITA DHIDI YA UONEVU, UKANDAMIZAJI WA HAKI NA UTU WA BINADAMU.
 
Heri wanaoudhiwa kwa sababu ya Haki maana.................................................
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tuwekeni ushabiki kando unawezaje kufananisha kesi ya mandela na lema? Umetumia vigezo gani?
This is crap, wewe msifie lema kwa alichofanya na si kulinganisha na mandela ili kuipa sapoti hoja yako.
Kimsingi hizo ni issue mbili tofauti kabisa, think again

Kwani Mandela alienda jela kwa sababu aliiba? Ni kwa sababu ya kupinga mambo ya kikoloni yanayochagizwa na vyombo vya dola. Vipi uko chekechea nini?
 
Tuwekeni ushabiki kando unawezaje kufananisha kesi ya mandela na lema? Umetumia vigezo gani?
This is crap, wewe msifie lema kwa alichofanya na si kulinganisha na mandela ili kuipa sapoti hoja yako.
Kimsingi hizo ni issue mbili tofauti kabisa, think again

Dhulma ni dhulma tu, iwe inafanywa na kaburu, ifanywe na ccm, ifanywe na polisi wa arusha, jina lake ni lile lile tu dhulma.

Mandela alipigania kuondoa ukandamizaji uliokuwa ukifanywa na makaburu dhidi ya waafrika wenzake. Lema anapigania kuuondoa ukandamizaji na unyanyasaji unaofanywa na polisi dhidi ya wapiga kura wake wa arusha kuwakilisha unyanyasaji unaofanywa dhidi ya watanzania maeneo mbalimbali, wewe huwezi ku-connect dots mwenyewe? Kwamba uvccm wamefanya maandamanbo na mikutano bila kibali lakini wakapewa ulinzi na polisi. Baada ya hiyo mikutano hakuna kiongozi yeyote wa ucvccm aliyeshitakiwa ukiachilia mbali kuhojiwa kwa milya. Kwanini polisi wanakuwa na double standards? kwani wafuasi wa chadema si watanzania kama wanaccm?

Kama ni ushabiki, basi wewe ndiye unapaswa kuuvua kwanza ili uzungumze jambo la kueleweka.
 
Mkuu hapo kwenye Red,
Ni vizuri ulianza na neno nafikiri, Ukweli ni kwamba, Mandela alipewa chaguo la kuwa huru kwa sharti moja tu la kusitisha mapambano ili asirudi mahabusu - akakataa. Bila kujali ni uhaini au la, angekubali kusitisha mapambano, yangeisha - yeye alikataa. Unadhani Lema angekubaliana na matakwa ya ccm na polisi haya yote yangempata?

Kamanda wangu !!!

Wajua humu watu wengine wao sijui hawajui wajibu wao ulio waleta hapa duniani au rahaaaaa!!

Swala linalo itwa mapambano wanalichukulia kwa uzito mdogo sana kwa hili la lema ni mwanzo na watakuja kujua mbele ya safari.
Mwl. Nyerere alijitoa kwenye serikali ya mkoloni kwa sababu yale aliyokuwa akiyapigania wakoloni walikuwa hawayatimizi akajitoa na kupigania haki na uhuru wa watanganyika akiwa nje ya serikali ya wakoloni na ndivyo hivyo sasa kuna mijitu mingine inasema huyo lema anafanya maaamuzi ya kujipa masifa na ndivyo hivyo wakati wa Mwl.Nyerere kulikuwa na watu kama hao na hata wakati wa Mandela kulikuwa na watu kama hao hao.

Katika lika hili la sisi vijana ambao tunaupeo kabisa wa sisi kwa sisi tunashindwa tambua HAKI zetu za KIRAIA na kukubali kuburuzwa na Dola kwa manufaaa ya Viongozi tulio wapigia kura kweli nasi twaona ni sawa tu acheni watunyanyase its Outrageous ideas or thinking
 
good move mpambanaji. jela sio mwisho wa maisha au ukombozi. walipomwingiza mandela jela alikuwa mdogoo very insignificant. walivyomtoa jela alishakuwa giant wa kutisha. watawala wajitazame upya. wasidhani kwa kumpeleka jamaa rumande ndo itamfanya asahaulike. inamjenga zaidi kisiasa na watajikuta hawana jinsi bali kuporomoka madarakani....
 
I have stupendous respect for Godbless Lema's boldness but I am not so sure if he's already in a position to be compared to Nelson Mandela's intrepidness. You have inordinately exaggerated the eclats and some may deem the remarks to be rather an insult to Mandela more than an accreditation to Lema.

But the undisputed fact is that the ruling part is using government apparatus to unfairly suppress opposition leaders. As an objective thinker, go through the lines and highlight the obvious double standard behaviour being used by Police forces and Judiciary to mistreat/frustrate CHADEMA so as to serve interest of CCM who were defeated in the last General Elections.

As a response to these mistreatments Hon. Lema has the point to tell Tanzanians and the world that CCM is basically wrong, powermonger and ant-democratic party. In fact, he has the support of many hearts and time will definitely prove that.
 
You are not serious!

"Mandela kama Lema" na sio walau "Lema kama Mandela"??

Labda niamini ni ukosefu wa kutoelewa lugha ya Kiswahili vizuri
Gaijin siyo kila thread ni lazima uchangie, au ndiyo nyie mnao fight uwe wa kwanza kuchangia? Hebu isome vizuri title yake uone kama coment yako ina hold water
 
Back
Top Bottom