Mandamano ya kuonyesha hisia zao Wazanzibar kuchoshwa na Muungano

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Matembezi ya amani Zanzibar

Written by abdi | 26/05/2012

uamsho-564x272.jpg


Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
 
Mimi sioni sababu ya kuwanyima watu haki ya kujiamulia mambo yao wenyewe na mstakabari wa taifa lao.
 
waongee kwanza na viongozi wa ccm zanzibar.. Muungano upo mikononi mwa viongozi wa ccm . Tuliwapigia kura wenyewe ..
 
Hawa CCM sijui wanataka tufikishane wapi katika suala la muungano? Kwanini tusiitishe kura ya maoni dhidi ya muungano huu, maana sasa tunaelekea kubaya leo Wazinzibari wameandamana kesho watatumia nguvu na hapo ndipo watakapoona tia akili hawa CCM ya solve this tatizo au watakapokufa watu ndo wataamini kuwa muungano hautakiwi.
 
Kuvunja Muungano ni kuhatarisha maslahi ya akina Hussein Mwinyi, Vuai Nahodha na wengine wengi....ccm haipendi kuwaudhi watu hawa, na wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano, kutoka zanzibar wataenda wapi? Unafikiri ccm itakuwa tayari kupoteza ulaji wa watu hawa???? ccm haipendi kuwaudhi watu bwana....!!!!!!
 
Back
Top Bottom