Tangazo na qualifications poa. Je hawajaweka mtu wao tayari na hii sio formality tu?
Mashirika mengine wanapewa kishkaji tu , mara Raisi kamteua fulani kuwa mkurugenzi shirika fulani .......na bla bla kibao.
Wakuu wa mashirika wanapaswa waombe kazi wafanyiwe interview na due diligence kabla ya kupewa ofisi. Waliopewa kishkaji ndio hao wameyaua yote. Kodemet
Ukweli ni kwamba Badra hakuwa anafahamu na si yeye tu kwani baadhi ya viongozi wa juu na wenyewe hawakuwa na taarifa kama vile Kiongozi wa chama cha wafanyakazi.Katika magazeti ya jana jioni Badra Masoud ambaye ni afisa uhusiano na habari wa Tanesco amesema hatambui hilo tangazo limetoka wapi na kuyatahadharisha magazeti yaliyotoa tangazo kuwa wasitegemee malipo kutoka tanesco.
Lakini tangazo lenyewe mbona limekaa ndivyo sivyo? linasema muombaji awe na digrii ya uhandisi AU utawala,hii imekaaje wadau,yaani inayumkinika umwambie mwombaji awe na digrii ya udaktari au sheria kwa kazi hiyo hiyo moja? inakuja kweli au iko namna ili xyz atengenezewe ulaji hata kama hana sifa? kwa nini wasiseme tu kwamba mwombazi awe na digrii ya uhandisi na shahada ya uzamili ya utawala (MBA au Msc Management)?
Sijapata maelezo ya kina kwamba nini kilimsibu Dr Idris huko TANESCO? Je ni majungu au kashindwa ku deliver?
Mkuu Jibu lako hili hapa chini na kwa wengine wenye utata na mabadiliko makubwa yanayokuja ndani ya shirika:Sijapata maelezo ya kina kwamba nini kilimsibu Dr Idris huko TANESCO? Je ni majungu au kashindwa ku deliver?