Man with 39 wives, 94 children wants to have more

Safi sana,anajali kama vyumba mia sio mbaya bado anakiwanja upstairs.
 
mmmh!huyu ni zaidi ya noma,halafu hapo sijaona dogo aliyekatatamaa na malezi ya dingi aiseee
 
Wake 39 inabidi wake wengine anaweza kukaa mwezi asikutane nae kimwili ukichukulia zamu ya siku moja moja,,,lazima wamsaidie tu!!


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
huyu anataka kuvunja recoki ya dunia

huyu mbona cha mtoto? kuna muha mmoja kibondo kavunja rekodi hiyo kitambo sema tzania hatuna utamaduni wa ku publish vya kwetu na tunaona upuuzi.

muha huyo anayeishi kilomita chache toka mji wa kibondo, ambaye pia ni sangoma, ana wake zaidi ya hao, watoto zaidi na wajukuu zaidi. maana kudhihirisha umahir wake, taarifa zinasema alijenga shule akapewa walimu kufundisha tu hapo familia yake elimu msingi.
 
huyu mbona cha mtoto? kuna muha mmoja kibondo kavunja rekodi hiyo kitambo sema tzania hatuna utamaduni wa ku publish vya kwetu na tunaona upuuzi.

muha huyo anayeishi kilomita chache toka mji wa kibondo, ambaye pia ni sangoma, ana wake zaidi ya hao, watoto zaidi na wajukuu zaidi. maana kudhihirisha umahir wake, taarifa zinasema alijenga shule akapewa walimu kufundisha tu hapo familia yake elimu msingi.

ndiyo data zako hizo!!
 
Amani iwe kwenu,

Kama wewe ni mwanaume labda mwenye familia ya watoto watatu na mke mmoja na huwa unalalamika maisha magumu sababu ya jukumu ulilonalo la kulea watoto na familia kwa ujumla. Kwa wale mliobahatika kupata watoto mtakubaliana nami kulea watoto hata mmoja ni shughuli pevu . Sasa hebu piga 'picha ' kulea watoto 30 inakuwaje? kabla hata 'flash' ya picha haijawaka, hebu vuta taswira ya familia yenye jumla ya wanafamilia 181 kwenye nyumba moja.
1458916646182.jpg

Hii ni familia ya Mzee Ziona Chana 72 ya huko India yenye
Watoto 94
Wake wa mzee Chana 39
Wajukuu 33
Wakwe 14 na wote wanaishi katika nyumba moja.
1458916926252.jpg

Mzee Chana akiwa na wake zake 39.
1458916988738.jpg

Jumba analoishi na familia yake, ndio nyumba kubwa kuliko zote kijijini kwao. Familia hiyo inaishi pamoja kwenye jengo moja kubwa mithili ya hoteli lenye ghorofa 4 na vyumba 100.
Mr chana hula katika chumba chake mwenyewe chenye kitanda kikubwa na wake zake 33, wale wadogo kiumri ndio wamepewa vyumba vya karibu na chumba chake na wale ambao wanakaribia kuingia kijiji cha 'mvi' wanalala vyumba vya mbali kabisa.
Anasema hakuna kuoneana wivu sababu kuna ratiba ya mzunguko wa yupi alale chumba cha 'mfalme '
1458917497354.jpg

Moja ya vyumba wanavyolala wake zake mithili ya bweni la wanafunzi.
Pia kuhusu mlo Chana anasema mlo mmoja wa jioni kwa familia hiyo inaweza kuteketeza kuku 30 kilo 132 za viazi , kilo 220 za mchele na hapo hatujazungumzia mlo wa mchana.
1458917709610.jpg

Wanafamilia ya mzee chana wakiandaa moja ya milo ya siku.
Mzee Chana anasema familia yake ina nidhamu mithili ya Jeshi kila mmoja anatimiza wajibu wake pia anasema hajachoka kuoa na ana mpango wa kwenda Marekani kutafuta Wake zaidi wa kuoa sababu zoezi hilo bado ni endelevu.
Angalizo: Habari hii nilipoikuta ni ya 2013 Mzee chana alikuwa na Miaka 69. Hivyo hatujui kama amesha ongeza wake wengine.
 
Back
Top Bottom