Mamluki/wahuni wa chadema ndio hawa tulionao jamvini?

Ziada Mwana

JF-Expert Member
May 20, 2011
201
22
Kumbe kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea wa BAVICHA kumetupa mwanga sana wa kutambua kuwa baadhi ya hawa wanaojifanya wafurukutwa/wakereketwa/walalahoi wa chadema ni mamluki. Kama kweli hata wakadiriki kuingia na visu, misumari, bisibisi na kila aina ya silaha ili kuwakabili "wapinzani" wao.

Tunao humuhumu JF na Dr Slaa amewasitiri kwa kuwaambia tu wameenguliwa kwa kukiuka maadili, ni yepi hayo? Kama sio hivyo visu? Wengine waliingia kichwakichwa kule Nyamongo na hata kudiriki kuvunja miiko ya kazi zao.

Kumbe ni "mamluki", mbona basi kupatikana na silaha kinyume cha sheria ni kosa la jinai na wala wasichukuliwe hatua za kisheria? Kama si ni watu wao CHADEMA? Na kwamba tu wanafunika kombe? Haya Dr Slaa endelea kuwatema hao akina ............

sikuelewielewi,.unalaumu,unatufahamisha,unatoa ushauri???kwani ulitaka waachwe hata kama walikiuka maadili ili kusionekane chadema kuna watu wanaokiuka maadili au vipi??mimi naona kilichofanyika ni kitu sahihi..kuwa kiongozi cdm lazima uwe msafi especially financialwise
 
Kuwaengua peke yake hakutoshi. Kitendo walichokifanya ni cha jinai na kama kweli Chadema ni watu wanaoheshimu utawala wa sheria, tukio hili linapaswa kuripotiwa katika vyombo vya dola na wahusika kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao. Tukio hili limetufungua macho na kujua sasa kwamba kumbe hawa walioenguliwa ndiyo vinara wa vurugu katika matukio yaliyopita huko nyuma and the leadership must come clean on this!
 
sikuelewielewi,.unalaumu,unatufahamisha,unatoa ushauri???kwani ulitaka waachwe hata kama walikiuka maadili ili kusionekane chadema kuna watu wanaokiuka maadili au vipi??mimi naona kilichofanyika ni kitu sahihi..kuwa kiongozi cdm lazima uwe msafi especially financialwise

Nimeelezea mambo mengi kwa wakati mmoja,hivyo ni juu yako kuchambua, kwanza nimesema (kukuhabarisha) kuwa hao wahuni wa chadema tunao humu jamvini tena wanajifanya wana siasa kali. pili nikashangaa kuona watu hao (mamluki) hawajachukuliwa hatua za kisheria kwa kupatikana na silaha kinyume cha sheria.na pia nikaonesha wasiwasi wangu kuwa watu hao si mamluki bali ni wana CDM ambao ni wajeuri,watukutu na hawafai kuwepo CDM ila Dr Slaa hataki kuweka wazi hilo na anatafuta mchawi nje ya CDM ili abebe mikoba.
 
Dikteta Saanane kaondolewa kabla ya kuingia kwenye kura.tumekaa tukafurahi,AENDE AKAGOMBEE UENYEKITI WA VIJANA WA ODM KENYA.AKAMSAIDIE KIPENZI CHAKE RAILA ODINGA.HECHE KUWA MAKINI NA HUYU ATAKUPINDUA.Hakikisha mnamdhibiti kweli kweli​
 
Acheni kujidanganya na mamuluki mwaka ule mlisema makam katibu mkuu ni mamuluki. Nyie semeni uchaguzi hamumwezi. Hata wabunge wa viti maalum nao ilishindikana. Hili neno limekuwa ngao kwenu kupangana madarakani kama mnavyopenda.
 
Kumbe kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea wa BAVICHA kumetupa mwanga sana wa kutambua kuwa baadhi ya hawa wanaojifanya wafurukutwa/wakereketwa/walalahoi wa chadema ni mamluki.(kama kweli) hata wakadiriki kuingia na visu,misumari,bisibisi na kila aina ya silaha ili kuwakabili "wapinzani" wao.tunao humuhumu JF na Dr Slaa amewasitiri kwa kuwaambia tu wameenguliwa kwa kukiuka maadili. ni yepi hayo?kama sio hivyo visu?wengine waliingia kichwakichwa kule nyamongo na hata kudiriki kuvunja miiko ya kazi zao,kumbe ni "mamluki", mbona basi kupatikana na silaha kinyume cha sheria ni kosa la jinai na wala wasichukuliwe hatua za kisheria? kama si ni watu wao (chadema)? na kwamba tu wanafunika kombe? haya Dr Slaa endelea kuwatema hao akina ............

" BARAZA la Vijana la Chadema (Bavicha), limepata viongozi wapya katika uchaguzi uliotawaliwa na mizengwe na vurugu zilizotishia usalama wa wapigakura.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa, vurugu hizo zilichochewa na kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa kuonyesha visu alivyodai kuwa vilikamatwa na walinzi wa chama hicho jana asubuhi. Mbali na kuonyesha visu kadhaa, Dk Slaa alitangaza kuenguliwa kwa wagombea watatu wa nafasi ya uenyekiti; Bernard Saanane, Greyson Nyakarungu na Mtela Mwampamba kwa madai ya ukiukaji wa maadili.

Dk Slaa aliwaeleza wapigakura kuwa kamati ya ulinzi ya chama hicho pia ilibaini kuwapo kwa mabaunsa waliodaiwa kupandikizwa katika mkutano huo kwa lengo la kuuvuruga.Alisema watu hao waliletwa na baadhi ya wagombea wa nafasi za uongozi ambao kimsingi chama hicho kilikuwa kimebaini kuwa ni mamluki waliopandikizwa kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo. Kuhusu wagombea walioenguliwa, Dk Slaa alidai kuwa kuondolewa kwao kumetokana na kukiuka maadili."
(soure JF - DJ CHOKA FREDY)

Ngoja niende toilet kwanza
 
hueleweki...what i can c una jaribu kuhochea vurugu ndani ya chadema..you cant nenda magamba kafanye upuuzi wako CDM hakuna nafasi..
 
Wana-CDM kuweni macho uchaguzi usiwagawe na hatimaye chama kikayumba, wabaya wenu waka-take advantage.
 
Nimeelezea mambo mengi kwa wakati mmoja,hivyo ni juu yako kuchambua, kwanza nimesema (kukuhabarisha) kuwa hao wahuni wa chadema tunao humu jamvini tena wanajifanya wana siasa kali. pili nikashangaa kuona watu hao (mamluki) hawajachukuliwa hatua za kisheria kwa kupatikana na silaha kinyume cha sheria.na pia nikaonesha wasiwasi wangu kuwa watu hao si mamluki bali ni wana CDM ambao ni wajeuri,watukutu na hawafai kuwepo CDM ila Dr Slaa hataki kuweka wazi hilo na anatafuta mchawi nje ya CDM ili abebe mikoba.

Vyombo gani vya sheria unavyovizungumzia? ni hivi vinavyouwa watu! au ni hivi vianavyoshindwa kuishtaki kagoda?
 
Kijana toka humu haustahili sio mahali pa utoto wa kufikiri,hakuna atakae nunua na kuukubalh ujinga wako!
 
Nafasi zilikua ni chache na wagombea walijitokeza kibao.

Kwa kitendo hicho pekee yake i nzuri sana kuonyesha imani yao kwa CHADEMA. Viongozi waliobahatika kuchaguliwa BAVICHA sasa muanze kazi mara moja. Na wale ambao hamkubahatika leo hebu jibidisheni zaidi kuimarisha CHADEMA ili kesho tuweze kupata sababu murua wa kuwafikirieni.

Kazi namba moja mbele yetu sasa hivi ni BAVICHA kuzunguka nchi nzima na kutumia mbinu zooooooooooote zinazowezekana kuhakikisha ya kwamba MWEZI JUNI HII BUNGE LETU LINAANZISHA MCHAKATO WA KUPATIKANA KATIBA MPYA YA WANANCHI bila kuingiliwa na watawala.

Kipimo chetu kwenu pa kwanza ni hapa sambamba na kufungua matawi na kuimarisha zilizopo kote nchini.

Kumbe kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea wa BAVICHA kumetupa mwanga sana wa kutambua kuwa baadhi ya hawa wanaojifanya wafurukutwa/wakereketwa/walalahoi wa chadema ni mamluki.(kama kweli) hata wakadiriki kuingia na visu,misumari,bisibisi na kila aina ya silaha ili kuwakabili "wapinzani" wao.tunao humuhumu JF na Dr Slaa amewasitiri kwa kuwaambia tu wameenguliwa kwa kukiuka maadili. ni yepi hayo?kama sio hivyo visu?wengine waliingia kichwakichwa kule nyamongo na hata kudiriki kuvunja miiko ya kazi zao,kumbe ni "mamluki", mbona basi kupatikana na silaha kinyume cha sheria ni kosa la jinai na wala wasichukuliwe hatua za kisheria? kama si ni watu wao (chadema)? na kwamba tu wanafunika kombe? haya Dr Slaa endelea kuwatema hao akina ............

" BARAZA la Vijana la Chadema (Bavicha), limepata viongozi wapya katika uchaguzi uliotawaliwa na mizengwe na vurugu zilizotishia usalama wa wapigakura.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa, vurugu hizo zilichochewa na kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa kuonyesha visu alivyodai kuwa vilikamatwa na walinzi wa chama hicho jana asubuhi. Mbali na kuonyesha visu kadhaa, Dk Slaa alitangaza kuenguliwa kwa wagombea watatu wa nafasi ya uenyekiti; Bernard Saanane, Greyson Nyakarungu na Mtela Mwampamba kwa madai ya ukiukaji wa maadili.

Dk Slaa aliwaeleza wapigakura kuwa kamati ya ulinzi ya chama hicho pia ilibaini kuwapo kwa mabaunsa waliodaiwa kupandikizwa katika mkutano huo kwa lengo la kuuvuruga.Alisema watu hao waliletwa na baadhi ya wagombea wa nafasi za uongozi ambao kimsingi chama hicho kilikuwa kimebaini kuwa ni mamluki waliopandikizwa kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo.
Kuhusu wagombea walioenguliwa, Dk Slaa alidai kuwa kuondolewa kwao kumetokana na kukiuka maadili."
(soure JF - DJ CHOKA FREDY)
 
Back
Top Bottom