Mamlaka ya Rais

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,601
338
Utaratibu huu wa uteuzi wa makatibu wakuu wa wizara na viongozi wengine wa serikali uliopo sasa hivi unaturudisha nyuma sana. Yahani jinsi ilivyo sasa kila kitu kinasubiri maamuzi ya rais, kweli ni haki hii? kila kitu rais tu jamani? Ah amejirudinkia madaraka makubwa mno na hapo kweli kunahaja ya kurekebisha katiba yetu ili japo bunge ama waziri mkuu wawe na mamlaka zaidi ya rais hasa ktk uteuzi wa watendaji mbalimbali wa serikali. WanaJF mnasemaje hapo? Mnasadiki?
 
Naunga mkono hoja..,rais wetu amerundikiwa madaraka kupita....,ila hili ccm wataliona baada ya kuanguka
 
Dawa ipo tunayo, ni kuandika katiba mpya, tena wala tusione aibu just copy and paste katiba ya Kenya na kurekebisha mambo kidogo tu, hivyo kilichokuwa kinatakiwa sasa hivi ni kuipitia katiba ya kenya na kuchukua yote yanayotufaa na kuyaacha yasiyotufaa au kuongezea yaliyopungua. Hapo tutaepuka gharama na mda, hawa waliopo madarakani sasa hivi wanachofanya ni delaying tacts kwa ajili ya manufaa yao na siyo kwa manufaa ya Watanzania, tuamke jamanai tumwombe MUNGU atusaidie nchi itoke mikononi mwa wa koloni wazawa.
 
Back
Top Bottom