Mamia wa wamzika mama wa Ufoo Saro

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Hai/Dar es Salaam. Kijiji cha Uraa Machame kilichoko wilayani Hai mkoani Kilimanjaro jana kilifurika mamia ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali walioshiriki mazishi ya Anastazia Saro ambaye ni mama mzazi wa mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro.

Vilio na simanzi vilitawala katika mazishi hayo hasa kutokana na mazingira ya kifo cha Anastazia (56), aliyekatishiwa uhai wake kwa kupigwa risasi na mkwewe Anthery Mushi, Jumapili jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, Ufoo alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi kifuani na tumboni na Mushi na matokeo yake kukosa mazishi ya mama yake kutokana na kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Baadhi ya waombolezaji walishindwa kujizuia kutokana na simanzi walizokuwanazo na waombolezaji watatu walizimia mara baada ya kuuona mwili wa marehemu wakati wakitoa heshima za mwisho.

Waombolezaji walianza kutoa heshima za mwisho kuanzia saa 6:00 mchana na baadaye ibada ya mazishi kuanza na kisha mazishi kufanyika eneo la makaburi la Kanisa la Uraa.

Akizungumza katika ibada ya mazishi, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wa Jimbo la Hadi, Aminiraab Swai alisema pamoja na yote yaliyotokea Mungu atabaki kuwa Mungu.

Mchungaji Swai alisema mwanadamu anayeishi anatisha kuliko mfu kutokana na wanadamu kuasi sheria za Mungu na kufanya mambo na matukio yasiyompendeza Mungu.

Alisema ni jambo la kushangaza kwani kwa sasa kila mmoja analia na hali ngumu ya maisha iliyopo na hata aliyepewa dhamana ya kuongoza naye analia kutokana na hali ngumu iliyopo.

Akitoa salamu za rambirambi, Mkuu wa Wilaya ya Hai ambaye aliwahi kufanya kazi na marehemu kama mtangazaji wa ITV, Novatus Makunga alisema kifo cha mama yake Ufoo kimemshitua sana. Hata hivyo, aliwataka Watanzania kuzidi kuiombea familia ya marehemu.

Mushi kuzikwa kesho

Mwili wa Mushi, aliyekuwa mchumba wa Ufoo, umefanyiwa uchunguzi jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na unatarajiwa kuagwa leo katika hospitali hiyo kabla ya kusafirishwa kwenda Uru mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

Akizungumza na gazeti hili, kaka wa marehemu, Silva Mushi alisema uchunguzi wa mwili huo ulifanyika na shughuli za kuaga zitakuwa leo kuanzia saa tano asubuhi hospitalini hapo na baadaye itaanza safari ya kuelekea kuelekea Uru mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
 
Ndugu yangu usikae uhukumu maana wewe hujui ukweli uko wapi..dont do this agai.hebu chukulia km wewe ni mama yako??na watu wanaakusema hivi not goood
 
Waandishi wa habari tumieni weledi wenu kuandika habari sahihi na zinazoeleweka
 
Ikiwa kumbukumbu zangu ziko sahihi Askofu mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini ni Dr Martin Shao.
 
Back
Top Bottom