Mambo ya ndoa: Yawezekana naibiwa?

Mpe muda wa kulichunguza hili jambo, dalili zipo lakini sio strong enough to make conclusion. Mlie chabo hasa hizo simu, hasa ukipata muda muafaka jaribu kusoma txt zake au incoming and outgoing calls.

Unaweza hata ukaweka siku umfatilie nyenendo zako baada ya kazi.

Aisee kuna wengine kiboko wanachat sana na kupiga simu kibao na kupokea ukichek simu zao kila kitu kimefutwa si call log,inbox wala sent items na kila akiacha simu lazima afute kila kitu kwanza ndo simu iwekwe mezani
 
Mhhhhh! Yahitajika busara sana kutatua hilo jambo! Kwanza kabisa wewe usimuulize, mlie cobis tu, wala usioneshe kuwa una wasiwasi nae, ila kumuumiza roho na kumfanya roho imsute wewe mkumbushe jinsi gani unapenda sana na hutaki kumpoteza! Mweleze unavomthamini na alivo wa muhimu kwako kila mara. Ila at the same time fanya uchunguzi wa kina wa matukio yake, mpitie kazini bila taarifa mda kutoka mwambie muongozane home ( Kama ana kidate utaona atavojitahidi kukukwepa) chunguza chunguza tu taratibu kwa mda, ili upate uhakika na wkt huohuo umpe mda wa kutambua mistakes zake, huenda akajirudi. Unaweza kuta nae yamemkuta kama yangu ana crash kwa bosi wake mpya! LOL! Ila akizoea utakuta anajielewa na kurudisha heshima na upendo zaidi. Cheating inahitaji roho ya chuma! Wengi wanajaribu wanahcemsha!
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana maana wengine utadhani wana mioyo ya chuma au labda hawana kabisa yaani ni kama mawe. Ni muhimu kujiridhisha na mambo kama ni kweli au la kabla ya kuchukua uamuzi wowote. THANKS BWANA
 
Yeye sikisha kuwambia yeye msafi sana hana mambo ya kucheat, sasa yanini unataka kumlazimisha awe cheater.

Mwanamke hachungwi baba utajiumiza tu, na mwanaume yule mwanaume haswa, mara nyingi sana huwa hana wasi wasi na mke wake.

Sasa mwanamke kujipilizia perfumes na kupaka lipstick ndo lazima awe anagawa tunda lake tu nje, kazi unayo si mchezo.

Nimepata UJUMBE MURUA kuwa baadhi ya wanawake wanajichuklia kama wao wako sahihi kwa kila jambo na wanaume ndiyo wakosaji tu. Kwamba mke afanye visa halafu mume ajikaushe tu eti asiwe na wasi wasi. NAWE THANKS PIA KWA ELIMU YAKO
 
Nimepata UJUMBE MURUA kuwa baadhi ya wanawake wanajichuklia kama wao wako sahihi kwa kila jambo na wanaume ndiyo wakosaji tu. Kwamba mke afanye visa halafu mume ajikaushe tu eti asiwe na wasi wasi. NAWE THANKS PIA KWA ELIMU YAKO
Mimi nauliza hivi, we ulipo owa ulijiolea tu au ulimfatilia huyo mwanamke tabia yake kwanza.

Kama ulijiolea tu bila kuchunguza unapo owa, una haki ya kuwa na wasi wasi na mke wako, na kama uliowa na ulimuamini mke wako kama ni mwanamke aliye tulia vipi uwe na wasi wasi naye?

Je mwanamke ulie muowa kwanza alikuwa katulia na ana adabu zake, vipi abadilike ghafla? kosa liko kwa mme au wazazi wake....Ukiweza nijibu swali hilo nadhani utagundua mtego wa kumnasa...siku njema :yo:
 
We akili zako sometimes zinachekesha vipi ukae unamchunguza mke wako/mme wako kama humuamini unaishi naye ya nini....Pls refer Qur'an 49:12

Wakati mwingine tunaepuka kufanya maamuzi ya haraka bila kuwa na uhakika wa mambo. Uhakika ukiwepo hata mhusika atajilaumu mwenyewe tu
 
Hahaha! Sasa mie nnaeogaga jumapili kwa jumapili siku nikioga jumatano si talaka!
Sipati picha uzee huu unaamka asubuhi unanawa unaishia, mweeh!
loh yqani nyie mkishaoga usiku asubuhi mnanawa mnaenda kazini? Khaaaaaaaaaaaaaaaaa

mpe mkeo hongera kwa kujua kuwa mwanamke anapaswa awe msafi........
Mwanamke anukie......
Mwanamke asiwe na vichaka huko kunakofunikwa nguo
 
Habari wanajamii

Mwenzenu naleta hoja hii. Inanihusu mimi mwenyewe na simzungumzii mtu mwingine kama ilinavyofanywa na wengine.

Nina mke na watoto, kwa muda mrefu tuliishi vizuri japo mikorogano midogo midogo haikukosa. Lakini mwaka huu mwenzangu kabadilika sana na nimeingiwa na hisia kuwa huenda kuna mahali mama watoto ana-cheat.

Kwa kawaida tukishaoga usiku asubuhi yake huwa haogi mwili mzima lakini usiku wa juzi kwanza alijifanyia usafi akafyeka NYWELE ZAKE kila mahali zilipo ukiondoa za kichwani (NADHANI NAELEWEKA). Jana kaamka saa 10.00 alfajili akaenda nje kuchemsha maji ili aoge (hii siyo kawaida yake).

Mimi nilibaki ndani kwa muda lakini alipoingia ndani akakuta najiandaa kutoka nje akasema nibaki ndani kwanza yeye atakuja kunistua muda mwafaka ukifika - huenda alitaka aoge na kujufuta maji mwilini huko huko nje bila mimi kujua. Alioga hivyo hivyo na kujipuliza pafyumu nzuri nzuri, kajivika cheni za dhahabu, lipstick, nk tofauti na nilivyomzoea. Kama kawaida tuliongozana kwenda kazini japo hatufanyi kazi sehemu moja.

Jana jioni au tuseme usiku kuna shughuli nilikuwa naifanya nje, akaja kuniuliza eti nafanya nini kwa kuwa yeye alitaka kulala, hapo chakula cha usiku (dinner) hakijaliwa bado. Lakini nilipoenda dinning yeye alikuwa anahangaika na simu yake tu.

Wazoefu wa mambo haya mnijuze tafadhalini. Je kwa mazingira hayo yawezekana tayari kuna mahali amepata 3rd party?

KILA MARA MWENYEWE HUDAI KUWA YEYE NI MSAFI SANA NA KWAMBA KAMA NI KUCHEAT LABDA ITAKUWA MIMI NDIYE NAMCHEAT NA SIYO YEYE, LAKINI NYENDO ZAKE ZINATIA WALAKINI.

Kaka what mind can conceive can be achieved. Kwanini usifikirie anatafuta hela za kujenga maghorofa? Bila kuwa na uhakika na anachokifanya, you guesses might be wrong....na unatafuta presha for no reason.
 
Hivi hujui kwamba na waganga wa kienyeji wateja wao wakubwa ni wanawake? kama amepewa dawa za kuoga kwa masharti wewe utajuwaje? leave her alone, mke ni wa kukupa kampani tu ya kimaisha na sio something to take so serious. ndio maana wanaitwa HAWA.
 
Pole sana mkuu, ila ushauri wangu ni kuwa mchunguze kwanza na usimuhukumu mapema, bado dalili ni changa sana na naupaswi kumuhukumu mapema hivyo. Kama umampenda kwa dhati, jaribu pia kuepuka hiyo migogoro midogo midogo (ata ukishindwa kuiondoa ipunguze tu) ili muweze kuwa na amani na muishi kwa upendo. Pia kuwa makini unapomchunguza maana wengi hawapendi wachunguzwe (ataona kama humuamini).
Kila la kheri ndugu.
 


Wakati mwingine tunaepuka kufanya maamuzi ya haraka bila kuwa na uhakika wa mambo. Uhakika ukiwepo hata mhusika atajilaumu mwenyewe tu
Wanasema shaka shaka hazileti uhakika wa kweli, mke wako kama anacheat lazima alikuwa kicheche tu toka mwanzo, au wewe ndo umefanya awe vile kwa kumshakia shakia :bounce:
 
Kijana usiishi kwa wasi wasi kama wewe msafi mwenzako akichapuka utajua. Hamna tatizo hapo bado.
 
Hivi hujui kwamba na waganga wa kienyeji wateja wao wakubwa ni wanawake? kama amepewa dawa za kuoga kwa masharti wewe utajuwaje? leave her alone, mke ni wa kukupa kampani tu ya kimaisha na sio something to take so serious. ndio maana wanaitwa HAWA.


Bwana mdogo sijakusoma kabisa.
 
Jifanya boya usimuulize Wala usi Doubt choChote mbele ya macho yake...ipo siku atapitiliza ndipo utampatia hiyo DoCumentAry yake ...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
...Sipati picha uzee huu unaamka asubuhi unanawa unaishia, mweeh!
Nadhani wengi tunaongea kutokea DSM. Kwa maeneo ya baridi hili suala la kuoga (hasa kwa watu wa maisha ya kawaida au chini), huwa ni tete sana..si wanaume si wanawake!
 
Rafiki, usafi ni tabia! Mie ninmekulia sehemu za baridi lakini kuoga asubuhi na jioni ilikuwa lazima. Nimeshaoga maji ya baridi saa kumi za alfajiri nikiwa Moshi, Lushoto, Mbeya, na Arusha manake hupenda kuanza safari alfajiri. Nimejiwekea akilini siwezi kuamka kitandani nikatoka bila kuoga mwili mzima! Seuze mwanamke alieolewa kabisa, mweh!
Nadhani wengi tunaongea kutokea DSM. Kwa maeneo ya baridi hili suala la kuoga (hasa kwa watu wa maisha ya kawaida au chini), huwa ni tete sana..si wanaume si wanawake!
 
Rafiki, usafi ni tabia! Mie ninmekulia sehemu za baridi lakini kuoga asubuhi na jioni ilikuwa lazima. Nimeshaoga maji ya baridi saa kumi za alfajiri nikiwa Moshi, Lushoto, Mbeya, na Arusha manake hupenda kuanza safari alfajiri. Nimejiwekea akilini siwezi kuamka kitandani nikatoka bila kuoga mwili mzima! Seuze mwanamke alieolewa kabisa, mweh!
Wapo wachache sana wa aina yako au yangu (siogopi maji ya baridi!). Ni vema umetaja maeneo hayo ambayo kwa bahati na mimi pia nimewahi kupita/ishi na ningeongeza na njombe,makambako, mufindi/mgololo kule, ifunda na hata iringa na kwa watani zangu kule pare. Kwa maeneo hayo ni nadra sana kwa watu kuoga mara mbili kwa siku (I would bet not more that 20% would take bath twice per day!). Naturally, wengi hawapo confortabe kuoga maji ya baridi na hivyo hupendelea kuchemsha kwanza au kuoga mchana (kama kuna jua).
 
Back
Top Bottom