Mambo ya ndoa (swali)

Pole sana!

Huyo simkeo tena, chunguza kwa makini, bilashaka Mchungaji Slaa ameshaingilia ndoa yako, pole !!!!
 
Siyo lazima ratiba zifanane. Kwa mfano, wote Ni marubani hamuwezi rusha ndege moja kila siku! Kuna kitu zaidi ya hicho anacholalamikia huyu jamaa. Nina wasi wasi kapoteza control ya familia....... na njia rahisi ni kupiga chini mke kama hakuna suluhu.
Nashukuru Malafyale, ni kweli si lazima zifanane nilichokuwa na maanisha hapa ni kuwa huyu bwana lazima kama ndivyo anayajua mahitaji ya kazi ya Wife wake. Kwa mfano kama mimi ni daktari na wife ni daktari nikiwa kama daktari najua kuna siku nakuwa na night shift vivyo hivyo na wife pia so hakuna shaka ktk hili likiwepo basi utakuwa ni wivu wa kijinga.

Lakini pia nikiwa kama Daktari najua si kuwa kila siku ntakuwa night so najua ratiba na mwenendo wa kazi ya udaktari mke wangu hawezi kuwa anarudi kila siku late na kusema ni kazi sbb nami naijua.

Anyway nadhani huyu jamaa awe muwazi zaidi NI NINI SBB ALIZOZITOA HUYU SHEMEJI KTK HICHO KIKAO? Then from there twawezapata picha halisi na kumsaidia kimawazo.
 
Ndoa ni mapatano au mkataba wa pande mbili, hivyo kwenye mkataba kabla haujasainiwa lazima kila mtu aridhike na masharti ya mkataba,inavyo onekana wewe na mkeo mliingia ndani ya ndoa kwa kudanganyana na i love u i love u mkasahau kuwekeana masharti kabla ya kuoana.

Na hili ndilo tatizo kubwa la ndoa za leo wanaenda kwa msukumo wa ngono na si kuzingatia vigezo na masharti. Hivyo basi kwa wewe hapo huna la kufanya ni kuachia ngazi na kujipanga upya, inawezekana akawa huyo huyo kama atakubaliana na masharti utakayo weka.

Ushauri kwa vijana msiingie kwenye ndoa kabla ya kuwekeana masharti na kila mmoja aridhike nayo ili mwisho wa siku likitokea la kutokea ujue pakuanzia.
 
Pole sana!

Huyo simkeo tena, chunguza kwa makini, bilashaka Mchungaji Slaa ameshaingilia ndoa yako, pole !!!!

Jamani sina imani sana kama unafit ktk hili jukwaaa..... Siyolazima kuchangia mada ikiwa uwezo wako wa kufikiri ni mdogo ki-hivo!

Ningekuwa na mamlaka ninge kupiga BAN kabisa.
 
tatizo kubwa lipo kwa huyu mwanaume .mama amzae mtoo wake mwenyewe asimnyonyeshe haikuji hata kidogo ..........think twice.........
 
Kunawaziri mmoja mwanamke mwenye familia nchi fulani aliamua kujiuzuru uwaziri ili apate kuwa na muda mwingi wa kukaa na watoto wake kwani aliona hawatendei haki watoto wake katika swala la malezi.
 
Pole sana Mnyalu, Ewe mke wa mnyalu wawezaje kumtesa mtoto uliyembeba kwenye tumbo lako mwenyewe.
Mama sikia sauti hii katoto kachanga kanakuita mamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa eyaa! eyaa! eyaa! eyaa!

Mama ndo mtetezi wa watoto jamani hata kama mwanaume huyo anakukera kiasi gani ukiwatesa watoto bado hujamkomoa yeye.

Unajua mama watoto watakutetea ktk mengi,watu au mwanaume anaweza akakutesa akakunyanyasa, ukaitwa majina mabaya lkn watoto wako uliowazaa mwenyewe ukiwalea vizuri watakuja kusema huyu ni mama yetu, hata kama dunia nzima inamkataa lakini ashukuriwe Mungu kwa sababu alitupenda akakubali kutuzaa na kututunza. WALEE WATOTO WAKO MAMA.

Na wewe Mnyalu anza darasa upya, si bure jamani. Tabia unayoitaka kwa mkeo kagua kama unayo.
 
Sikiza udugu wa Mke na Mume ni Kama nyanya mnakutana kwenye tenga na dunia ni soko itafikia kipindi kila mtu anakwenda kivyake. Kwani Unakipata kikubwa kipi kutoka kwa huyo Mwanamke zaidi ya jasho na shombo la kizinifu analokuletea Nyumbani

Huo ni Uzembe, milango ipo wazi suala la kuwa na Mtoto mchanga wa miezi minne halina uhusiano na yeye kumuacha kwa maana hata hivi yupo hana habari na Nyumba wala huyo Kichanga sasa kwa nini unaendelea kubeba gunia la Misumari wakati una uwezo wa kulitua?

UBWEGE mwingine una kera sana mambo kama haya msiwe mnayalete kwenye forum mnatuaibisha wanaume kama humuwezi pengine MZEE KWENYE 6 X 6 wewe ni dhaifu sasa kampata anayejua kweli kweli kuichakachua 6x6 mpaka inakuwa ni KUDADADEKI:

Acha uvivu sk akirudi mchakachue hadi kesho ashindwe kusimama kesho asubuhi iwe

Yaani asikie kama ndo viazi vinaanza kuchimbwa vile.
 
Ikiwa mke wako wa ndoa anayefanya kazi inayofanana na yako anatoka saa kumi na mbili asubuhi kuelekea kazini na kurudi mara saa tatu, saa nne, saa tano na wakati mwingine saa saba za usiku na hana hata muda wa kuangalia watoto, nyumba na hata kuchangia financially mahitaji ya hapo nyumbani. Utamfanya nini?

Assume umeshawahi kuitisha kikao cha wandugu wa pande zote mkajadili suala hilo lakini ameshindwa kubadilika na mmezaa watoto wamili .

Mmoja anakaribia miaka minne na wa pili ana miezi minne tu ila amegoma kunyonya maziwa ya mama yake hivyo anaishi kwa uji, maziwa ya kopo na maji, sometimes mnampa juisi ya embe na papai.

Utafanya nini kwa mke kama huyo?

nafikiri watu wengi hukosea wanapooa, badala ya kuoa wanawake wanaoa kazi zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom