Mambo ya muungano na yasiyo ya muungano

Shoo Gap

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
246
71
Nimesikia mara nyingi kauli hii "kuna mambo yasiyo ya Muungano na yaliyo ya Muungano",. Kwa uelewa wangu Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tz walipaswa kushughulikia yale mambo ya Muungano tu, wakati ambao Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipaswa kushughulikia mambo ya yasiyo ya Muungano kwa upande wao tu. SWALI: Mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika chombo gani kinayashughulikia?



ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANO
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo.
ONGEZA MENGINE KAMA YAPO
 
Aisee mengi nilikuwa siyajui....

Nimeuchoka wimbo wa muungano ambao sioni faida yake kama Mtanzania...!
 
sioni uhusiano wowote na kuchoma makanisa nikisoma baadhi ya hayo mambo ya Muungano na nikilinganisha na kero za muungano.
 
Zanzibar imeshakiuka nyingi kama sio vyote kwa mtindo kujaribisha kidole kwanza
 
una uhakika hayo mambo ndo nyerere na karume walikubaliana?ebu tupe hiyo hati ya muungano kama ina hiyo orodha...HAMNA MUUNGANO HAPO MKUU ni kufaamiana tu na urafiki...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom