Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
Mohammed Dewji Blog » Blog Archive » MHUBIRI ALIYEFUNGWA KWA KULAWITI AONGEZEWA KIFUNGO KWA KUJARIBU KUTOROKA…!!!
Wadau mnadhani nini kinawakumba hawa viongozi wetu wa kiroho hadi wanafikia hatua kama hii ??
Je wadau kwani utumishi wa Mungu unamaslahi yeyote ??
Mhubiri mmoja nchini Kenya anayetumikia adhabu ya kifungo cha miaka 21 katika gereza la Kitui kwa kosa la kulawiti ameongezewa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu zaidi baada ya kujaribu kutoroka akiwa mikononi mwa sheria.
Mhubiri huyo ambaye kwa sasa ni mfungwa Jeremiah Munyoki wa Kanisa la Jesus Worship Centre lililopo Mathulini huko Kitui, alitoroka akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kitui alikokuwa amelazwa kwa kipindi cha wiki moja akiugua Malaria.
Mwendesha mashtaka Inspekta Kenndy Apidi ameiambia mahakama kuwa mfungwa huyo alimtoroka askari magereza aliyekuwa akimlinda hospitalini hapo na kuruka fensi ya hospitali na kukimbia hadi katika kichaka kilichokuwa karibu.
Hata hivyo maafisa wa polisi jamii wa mji wa Kitui walimuona na kumtilia shaka kutokana na kuvaa sare za wafungwa, hivyo kumkimbiza na hadi kumkamata na kumkabidhi kwa wahusika.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya Kitui Beatrice Kimemia, ambaye hapo awali alimhukumu mhubiri huyo kifungo cha miaka 21 kwa kosa la kumlawiti mvulana wa miaka 13, amemuelezea mtuhumiwa huyo kama mtu asiyejutia makosa yake.
MO BLOG kwa mara nyingine inakemea tabia kama za mhubiri huyu, ambaye alipaswa kuwafundisha maadili watu ikiwa ni pamoja na watoto wanaokuwa akiwaonyesha njia iliyosahihi, lakini kinyume chake ndiye amekuwa baradhuli wa kuharibu vijana.
Wadau mnadhani nini kinawakumba hawa viongozi wetu wa kiroho hadi wanafikia hatua kama hii ??
Maana tunaamini ukiwa mcha Mungu toka moyoni huwezi kufanya kitendo kama hicho, au siku hizi wengi wanakuwa watumishi wa kiroho kwa sababu ya maslahi ??
Je wadau kwani utumishi wa Mungu unamaslahi yeyote ??
Maana inaonekana wengi hawana wito
.Tusaidieni hili jamani
!!!!