Mambo ya kwa Babu LOLIONDO

Where is the government?, wapeleke JKT au waombe RED CROSS wajenge mabweni ya kujikinga na mvua.

Serikali inaona noma kumkubali Mchungaji wa Loliondo kuwa amewapiga bao watalaamu wao. Wana anza lingo longo eti wanataka waka prove dawa na mazingira ya upatikanaji wake.

Kwenye suala la maajabu ya Mungu, kuprove ni kupeleka wagojwa elfu waliothibitika kisha wapewe dawa kisha mkawapime tena na mue endelee kuwa monitor kwa kipindi maalumu kama wamepona.

Siyo waanze kuleta zengwe kwa mzee wa watu na kubuni mbinu za kufisadi ili wajinufaishe tofauti na malengo ya Babu!

Serikali chovu utaiona tu utendaji wake, hata kupeleka huduma muhimu kuhudumia raia, hawataki!
 
Mkuu.
Babu kapewa maono ya dawa hii na Mungu au Yesu?

Inaonekana Babu hakupewa amri au uono wa kuwa abague wagonjwa kulingana na imani zao za kidini.

Na Jee hao wagonjwa wamepewa sharti hilo la ku"kiri kuwa Yesu ni bwana"?

Hivi hapa Babu anafanya kazi ya uganga au uchungaji?

Jina Jipya la Mungu wangu ni Yesu; aliyejulikana zamani kwa majina mengi kama Yehova Yire (Mungu mponyaji), Yehove Nisi (Mungu ndiye bendera ya ushindi wangu) Jehova Shalom (Mungu wa Amani) Alfa na Omega (Yeye ni mwanzo na pia Mwisho), alionekana kwa Musa kama Yuko ambaye Yuko na kwa Wana wa Israel kama Mungu wa baba yao Ibrahimu Isac na Yakobo....So ukiniuliza kuhusu huyo Babu alioteshwa na nani na kama ni mganga au mchungaji; I cant say much he knows better than I do for he is the owner of the dream/vision....Sijawahi kumwona kumsikia yeye kama individual anadai nini hivyo nadhani I have no right to rule out who he is and kwa jina gani anafanya hayo anayofanya...

Kwakukusaidia mimi sina dini na wala siamini katika yeyote I am a christian by faith na ukristo tafsiri yake ni Outward working of Divinity in Humanbeings...The power that worketh is that of Holly spirit of God/Jesus hayo mengine ya dini niwaachie wanazozimiliki am out!
 
mti huo majani yake ni chakula cha twiga toka enzi hizo(nenda kwa michuzi kuna habari zaidi)

Loh twiga wamekula hasara masikini, watakosa chakula kabisa ikiwa majani yao yanakatwa kwa spidi hii.

Nilikuwa najaribu kupiga mahesabu ya haraka haraka. Ikiwa Babu anatibu watu 500 kwa siku x shilingi 500 ni sawa na 250,000 x siku 30 anajipatia Milioni zake 7.5 ambazo hazina kodi wala VAT.

Hongera Babu Mungu akupe nini tena?
 
Hizi zote ni ishara za watu waliokata tamaa na maisha! We fail to invest in better infrastructures, health services, education, roads...etc for our children..na tunaanza kukimbilia Loliondo kutafuta dawa za kututibu ukimwi na kansa! Ama kweli! Umasikini ni kitu kibaya. Lakini ni kibaya zaidi kama ni umasikini wa fikra. I only wish tungekwenda Loliondo kukomboa mbuga yetu aliyogawiwa yule mwaraabu...perhaps angetupa kodi zaidi tukajenga ile barabara ya Arusha-Loliondo!

Kama mnabisha kwamba watanzania tumekata tamaa na maisha angalia vitu kama DECI vilipoingia hata wakubwa wa serikalini waliiba kodi zetu wakaenda 'kupanda mbegu' sijui leo DECI iko wapi...mifano ni mingi jamani

Ushauri wangu kwa watanzania wenzangu: Mafanikio hayana short cut. Huwezi kupata utajiri simply kwa kwenda kwa mganga! work hard and bit of 'luck' money will come. Ni kupenda hivi vitu vya mkato mkato ndo tunazidi kuwa masikini. Unalala..usiku asubuhi unataka uendeshe Lexus! Unless uibe utaipata wapi? Mwanafunzi anashindwa kusoma shule anataka mganga amsaidie kufaulu mtihani! Tunawanyima haki wanachi wetu na kupeleka hela zote uswisi huku wachache wakiishi maisha ya peponi...harafu unakuta hao hao wanasimama kwenye majukwaa wakitwambia twende kanisani kuombea amani ya nchi! Kuna watu wanatufanya tuone kwamba umasikini ni mapenzi ya Mungu kitu ambacho si kweli. Kikwete anaona kabisa DOWANS wanatuibia na wale wahusika kashindwa kuwawajibisha...they have swindled billions in our name....Kikwete huyo huyo anasimama mbele ya TV anatwambia kwamba matatizo ya umeme yanatokana na kazi ya 'Mungu' kwa sababu mvua haipatikani. Twende kanisani/msikitini tukaombe mvua inyeshe tupate umeme!

I Masanja, I refuse to believe in this! Hardwork, determination and discipline will liberate you! I say and I do! Amen!

Mbona unachoongea hakina uhusiano na hii mada mambo ya watu kuponywa yana uhusiano gani na umaskini wetu wewe umetokea wapi kila kitu unataka kuingiza siasa na umaskini wetu acha mambo hauna ndugu mgonjwa wewe eeeeeh?utajua umuhimu wa huyu babu. Kuna waarabu wanakwenda huko na wanakiri kwamba yesu ni bwana kabla ya kunywa dawa hao nao ni watanzania? shauri lako.
 
Jina Jipya la Mungu wangu ni Yesu; aliyejulikana zamani kwa majina mengi kama Yehova Yire (Mungu mponyaji), Yehove Nisi (Mungu ndiye bendera ya ushindi wangu) Jehova Shalom (Mungu wa Amani) Alfa na Omega (Yeye ni mwanzo na pia Mwisho), alionekana kwa Musa kama Yuko ambaye Yuko na kwa Wana wa Israel kama Mungu wa baba yao Ibrahimu Isac na Yakobo....So ukiniuliza kuhusu huyo Babu alioteshwa na nani na kama ni mganga au mchungaji; I cant say much he knows better than I do for he is the owner of the dream/vision....
Kwakukusaidia mimi sina dini na wala siamini katika yeyote I am a christian by faith na ukristo tafsiri yake ni Outward working of Divinity in Humanbeings...The power that worketh is that of Holly spirit of God/Jesus hayo mengine ya dini niwaachie wanazozimiliki am out!

Umenisaidia sana mkuu.
Asante sana.
 
kaambia na Mungu bei ni mia tano tu........ nimetoka huko majuzi ndugu zangu na shemeji yangu amepona kisukari....Makamba nae tulipishana wakati sie tunatoka yeye ndo anaingia....hata mkuu wenu alifika huko kwa kisingizio cha kwenda kufukua nyayo za kale ...na amepewa juice ya babu......huenda hata poromoka tena majukwaani

Edson, hebu nisimulie jinsi babu anavyotoa huduma yake; unajieleza kwanza tatizo lako, ndo anakuombea au unapewa tu hayo maji yenye dawa???
Najiuliza pia, kwa jinsi watu walivyo wengi kwa sasa hivi, anatoka kweli kwenda kutafuta hiyo dawa, au alishachimba ya kutosha???
 
... inasemekana!! Yawezekana ni kweli au ni uzushi mtupu. Ile kitu inaitwa placebo
huponyesha pia lakini at the end si dawa.
Hivi kweli karne hii watu wazima na akili zao wanywe dawa amabayo haina uthibitisho? Au eti, ...tiba aya magonjwa sugu yasiotibika kisayansi na siyo... tiba ya magonjwa sugu ambayo tiba yake haijapatikana? Kisukari? Hypertension?

21st century!! Au hawa ni wale waliodanganyika?

Usifikiri ho watu woote ni wajinga! Hebu fikiria kuna maganga na machawi yanajitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa yanatibu ukimwi na magonjwa sugu lakini watu hawaendi kama wanavyo kwenda kwa Babu!

Mtu ukiumwa kwelikweli hautahitaji mbwembwe za kitaalamu, hata ukiambiwa mkojo wa mama mkwe unaponyesha ugonjwa ulionao ulioshindikana, utamtuma mkeo akaulete! achana na ugonjwa!
 
Usifikiri ho watu woote ni wajinga!
Mtu ukiumwa kwelikweli hautahitaji mbwembwe za kitaalamu, hata ukiambiwa mkojo wa mama mkwe unaponyesha ugonjwa ulionao ulioshindikana, utamtuma mkeo akaulete! achana na ugonjwa!
Anko Sam

Mfamaji ...haachi kutapatapa
au Mfamaji hukamata maji?

Nimependa mfano wako wa "mkojo wa mama mkwe".
Vipi ukiwa mkojo wa baba mkwe? Mtu huenda mwenyewe kuuchukua au anamtuma mke pia?
 
agggrrrr! nimemkumbuka yule mganga kule zimbabwe akadai amegundua kuwa kuna mafuta...mungu tusaidie!
 
Nadhani hujaelewa huyu jamaa anatibu nini habari zinasema hahusiani na haya uliyo comment
Mkuu

Masanja has a good point. Mimi nadhani wewe ndio hujaelewa.

Anachofanya Babu ni kutuliza tu hali za watu walioelemewa na maradhi au pengine kukata tamaa ya maisha. It's a psychological healing in the wake of traumatic experience, the problem is not going to go away, no. People only get relief and you know what happens they stop prior medication, so when the disease hits back it's a one way go. Babu has already said you can't take it twice, as is not going to help. Not good news but that's where we are.

The reasons how we got there is what Masanja tries to discuss.
 
Jifunze kusoma kitu kukielewa kabla hujajibu,

Siyo VVU tu magonjwa sugu, kisukari, kansa nk.
Joyceline perception ni ngumu kweli kweli. Mhafidhina na pengine wengineo hawakuelewa kuwa tiba hiyo ni kwa ajili ya magonjwa sugu kama ulivyoyataja(kisukari,cancer, figo n.k) ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Ieleweke pia kuwa na VVU siyo lazima upate UKIMWI. Kisukari, cancer, figo, ini kwa sasa hivi ni hatari kuliko hata VVU.
 
Hizi zote ni ishara za watu waliokata tamaa na maisha! We fail to invest in better infrastructures, health services, education, roads...etc for our children..na tunaanza kukimbilia Loliondo kutafuta dawa za kututibu ukimwi na kansa! Ama kweli! Umasikini ni kitu kibaya. Lakini ni kibaya zaidi kama ni umasikini wa fikra. I only wish tungekwenda Loliondo kukomboa mbuga yetu aliyogawiwa yule mwaraabu...perhaps angetupa kodi zaidi tukajenga ile barabara ya Arusha-Loliondo!

Kama mnabisha kwamba watanzania tumekata tamaa na maisha angalia vitu kama DECI vilipoingia hata wakubwa wa serikalini waliiba kodi zetu wakaenda 'kupanda mbegu' sijui leo DECI iko wapi...mifano ni mingi jamani

Ushauri wangu kwa watanzania wenzangu: Mafanikio hayana short cut. Huwezi kupata utajiri simply kwa kwenda kwa mganga! work hard and bit of 'luck' money will come. Ni kupenda hivi vitu vya mkato mkato ndo tunazidi kuwa masikini. Unalala..usiku asubuhi unataka uendeshe Lexus! Unless uibe utaipata wapi? Mwanafunzi anashindwa kusoma shule anataka mganga amsaidie kufaulu mtihani! Tunawanyima haki wanachi wetu na kupeleka hela zote uswisi huku wachache wakiishi maisha ya peponi...harafu unakuta hao hao wanasimama kwenye majukwaa wakitwambia twende kanisani kuombea amani ya nchi! Kuna watu wanatufanya tuone kwamba umasikini ni mapenzi ya Mungu kitu ambacho si kweli. Kikwete anaona kabisa DOWANS wanatuibia na wale wahusika kashindwa kuwawajibisha...they have swindled billions in our name....Kikwete huyo huyo anasimama mbele ya TV anatwambia kwamba matatizo ya umeme yanatokana na kazi ya 'Mungu' kwa sababu mvua haipatikani. Twende kanisani/msikitini tukaombe mvua inyeshe tupate umeme!

I Masanja, I refuse to believe in this! Hardwork, determination and discipline will liberate you! I say and I do! Amen!

Jaribu kupitia tena ili uelewe kilichoandikwa ndo utoe maoni yako. Ulichoandika hakifanani kabisa na ulichosoma, utakua hukuelewa mpendwa.
 
Huyu babu amenifanya nikumbuke maneno ya Mungu kuwa...' kiburi cha mwanadamu ni uzima', at the point of death kiburi chote cha mwanadamu kinayeyuka...Imagine watu wanaoinamiwa kwa heshima kede kede na wenye sauti za nguvu wote wamepewa amri ya kwenda kufoleni Loliondo na kibabu tu maskini bila kujali status ya yeyote (Aise Babu nakupongeza sana kwakutopenda ubaguzi) na wao bila hata kulazimishwa wakafuata amri ili tu wapate uzima. Sasa wahubiri tukisema kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kuwa Yesu ni bwana utashangaa mtu kwa kiburi cha uzima atakufanyia analysis mpaka unakaa chini...Ukiona mtu anachallenge decision ya wengine ujue
ndani kuna kakiburi cha uzima kanasumbua ndiyo maana anaweza nyanyua kifua na kujidai yeye ana akili kuliko wenzake....Tumshukuruni Mungu kwakutupa huo uzima tusidhani kuwa hao walioenda Loliondo wamemkosea sana Mungu ndo maana leo wanapiga magoti kwa Babu they are humbled by grace na tukumbuke kuwa hujafa
hujaumbika...Ni wangapi mnawapigia mafisadi magoti kwakuogopa vitumbua vyenu kuingia mchanga seuse uzima?
Tusubiri baada ya wataalamu toka Wizarani watakapo sema dawa hiyo ni bomba ili tumshauri Mkulu akapate dawa ya kuzuia kuanguka majukwaani ili wasiwasi ututoke hasa anaposafiri kwenye mikutano ya nje.
 
hii mada ina mantiki, haiwezekani watu wasafiri kutoka sehemu mbalimbali kukimbilia dawa ya mtu huyu, hii inaonesha dhahiri watu wamekata tamaa na huduma mbovu zitolewazo katika hospitali zetu

Sio huduma mbovu, bali kwa darubini malidhawa utagundua umasikini wa watanzia ni nini chanzo chake, na wala si ccm .Ila kwa akili nyepesi na kwa kupenda majibu mepesi ya kisiasa utakubali kweli tatizo la Tz ni ccm. Lakini kwa kwenda mbali utagundua vinginevyo. Subiriii.
Jiulize kwanini watanzania kwa asilimia kubwa kabisa hawajengi vijijini wanakotoka? aaaah acha kujenga kwenda kwao kijijini ni kwa kushitukiza ama hawaendi kabisa,Mhhhhhhh Tatizo la Tz nafikiri si kama watu wanavyojaribu kutafuta majibu mepesi.
 
Sina budi kumshukuru mungu kwa kumpatia dawa huyu babu yetu wa loliondo
kwa hajili ya kutibu magonjwa KATILI bin SUGU yanayoua watu kwa kukoseka
na dawa zake hapa duniani.

Nasema ahsante mungu, ahsante babu wa Loliondo.

Lakini kuna kitu nimegundua kuhusiana na watu wanaoelezea habari zinazohusu Loliondo takribani wiki tatu sasa tokea hii habari kuwa hotcake. Ukiingia kwenye mablog, magazeti, radioni na hata kwenye luninga. Hakuna mtu aliyejitokeza na kueleza live kuwa yeye ni muathirika mmoja kati ya wote waliokwenda au waliopo kwa babu na amepona iwe ukimwi, kisukari, kansa nk.

Matokeo yake kila anayekuja hapa jamvini au kwenye media nyingine, utamsikia anasema oooh ni kweli jamaa anatibu maana baba au mama yangu kaponea huko! Au nilimpeleka rafiki yangu na sasa ni mzima wa afya, au utawasikia nilidrive na familia yangu hadi huko na tulipata shida kadha wa kadha mpaka tukafanikisha dawa na sasa wote wamepona (yeye kajitoa) au utasikia mwingine anasema ooooh.... babu huyo siyo mchezo shangazi au mjomba angu nilimpeleka pale kwenye machela'lakini alipopewa tu dawa na babu mara akanyanyuka ghafla na sasa ni mzima.

Swali langu ni - hivi:

Kwanini watu tusiwe wawazi? kwanini mtu unashindwa kusema kuwa mimi ni muhusika nilikuwa naumwa ukimwi au kansa au kisukari na sasa nimepona kabisa baada ya kutumia dawa ya babu wa loliondo? Kwani kitaharibika nini? kwanini kila mtu analeta hizi habari za loliondo kwa kutuletea ushuhuda wa mtu mwingine ingali labda muhusika ni yeye mwenyewe?

Mie nafikiri ifike wakati watu tuwe wawazi kwenye mambo tatanishi kama haya ili iwe faida kwa jamii mzima!. - Nawasilisha waungwana.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki babu yetu wa Loliondo
 
babu ameanza kutibu watu huko Loliondo miaka kadhaa iliopita.
Wakazi wenyewe wq Loliondo b4 hawakusadiki na walileta kejeli, lakini kwa sasa woote bow down na ndio wanaleta vurumai kwa kudai kuwa wao ni wazawa so wanatakiwa wapate 1st priority ya kumuona Kamanda.

Kwa sasa Kamanda ameoteshwa na kuambiwa asogee sehemu tofauti na pale...

TAARIFA YA HIVI PUNDE...
kamanda kasema tujiandae kupokea wageni toka nchi mbalimbali wakija kupata Dozi.
Watakuja kwa magari, kwa ndege na kwa meli

Lakini cha kusikitisha na kukatisha tamaa ni kuwa Babu kasema ktk msafara wa Meli zitakazokuja basi kutakuwepo na adui yake mkubwa humo ndani na atakuja kwa nia mbaya....lool
 
Sinabudi kumshukuru mungu kwa kumpatia dawa babu yetu wa Loliondo kwahajili
ya kutibu magonjwa KATILI bin SUGU yaliyokosa dawa zake hapa duniani kwahajili
ya kutibu ukimwi,kansa,kisukari nk. Nasema ahsante mungu,ahsante babu wa loliondo. Lakini kunakitu nimegundua kuhusiana na watu wanaotuletea habari hizi
kupitia mablog,magazeti,radioni na hata kwenye luninga toka habari hizi ziwe hot
cake takribani wiki tatu hivi. -Swali langu ni -Hivi kwanini hakuna mtu yeyote aliyeji
tokeza hapa jamvini live au kwenye media zingine na kukili kuwa mimi ni mmoja kati ya watu waliotoka au waliopo loliondo kwa babu kwa kusumbuliwa na ukimwi au kansa au kisukari na sasa nimepona baada ya kutumia dawa za babu huyo wa
loliondo? Badala yake utakuta watu au mtu anakuja hapa jamvini au kwenye media
zingine na kusema ooooh....huyo babu si mchezo anatibu kila kitu! au utamsikia
mtu anasema mimi nilimpeleka rafiki yangu kwa babu na sasa amepona. Au utasi
mimi nilidrive na familia yangu kwa safari ya shida sana hadi loliondo,lakini baada ya mateso ya kadha wa kadha hatimae familia yangu ilipata dawa na sasa wote wamepona (yeye kajitoa hapo) na sasa tumerudi. Mwingine oooooh.... nilimpeleka
shangazi au mjomba kwenye machela,lakini baada ya kunywa dawa ya babu'ghafla
alisimama na sasa amepona kabisa. Swali langu la pili ni -hivi kwanini mtu usiseme
kuwa wewe ndiye muhusika? ulikuwa unaumwa ukimwi au kansa au kisukari na sa
sa umepona kupitia babu? kwanini kila mtu anatuletea habari ya loliondo kupitia
ushuhuda wa mtu mwingine? kwani ukiwa muwazi na kukiri wewe ndiye muhusika
mwenyewe itaaribika nini?
Mie nafikiri tufike sehemu tuwe wawazi hasa kwenye mambo tata kama haya ili iwe
faida kwa jamii mzima. - Nawasilisha waungwana

Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki babu wa Loliondo
 
ulishamuona mshindi wa jackpot bingo hata mmoja?
 
Back
Top Bottom