Mimi sitaki kumkani huyu babu kwamba yeye ni wa Mungu lakini Neno la Mungu linasema tuzipime hizo roho.
rai yangu watu wa Mungu nisaidieni niweze fahamu ninyi ambao mmesha zipima hizo roho je ni kweli huyu ni mtu wa mungu na siyo anasaidiwa na Mizimu ya mahalia na ndiyo sababu hawezi amishia huduma yake sehemu nyingine? Na hivyo mizimu hii imekuja kwa Sura ya Malaika wa Nuru.
Wasi wasi wangu isije kuwa tunakwenda kwa Mganga wa Kienyeji tukuifikiri ni mtu wa Mungu, yaani nalataka ni watu wajue kuwa ile ni nguvu ya Mungu au la ingawa inaponya.
Nawasilisha
Mungu awabarikLi sana!
nakubaliana na wewe japo siwezi kusema ni kwa kiasi gani! Watz wengi sasa tumekata tamaa na tunaamini ushirikina (Story ya CITIZEN of Sunday 27th Feb) na kwa vile 'waumini' hawapendi kujulikana huko, wamejitokeza kwa huyu maana ni MCHUNGAJI! Trends zinaonyesha kuwa uvumbuzi juu ya elimu ya udaktari principles zake ni zile zile na maendeleo ya technology yameiboresha zaidi. SWALI: Ikiwa unaumwa na vipimo viko wazi na ukaambiwa kuchagua kwenda kutibiwa na specialist (say UK/EU, USA, India, SA nk) au kwenda LOLIONDO utachagua nini???
nakubaliana na wewe japo siwezi kusema ni kwa kiasi gani! Watz wengi sasa tumekata tamaa na tunaamini ushirikina (Story ya CITIZEN of Sunday 27th Feb) na kwa vile 'waumini' hawapendi kujulikana huko, wamejitokeza kwa huyu maana ni MCHUNGAJI! Trends zinaonyesha kuwa uvumbuzi juu ya elimu ya udaktari principles zake ni zile zile na maendeleo ya technology yameiboresha zaidi. SWALI: Ikiwa unaumwa na vipimo viko wazi na ukaambiwa kuchagua kwenda kutibiwa na specialist (say UK/EU, USA, India, SA nk) au kwenda LOLIONDO utachagua nini???[/B]
"Kanyaga Babu wa Loliondo, Sambaratisha Babu wa Loliondo, kazi za babu saga"
Nukuu ya Mwananchi Leo 7.3.11 ikimnukuu Kakobe akimwaga maombi dhidi ya Mch. wa Loliondo.
Inategemea na ugonjwa unaokusumbua, babu anatibu magonjwa sugu yasiotibika kisayansi.