Mambo ya "Dinner Suit" Mbugani: Diamond Platinum

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
DIAMOND PLATNUMZ APIGA KAMPENI NGORONGORO CRATER......

DIAMOND PLATNUMZ APIGA KAMPENI NGORONGORO CRATER...... | This is Diamond






SANII wa muziki wa kizazi kipya,Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz' amewataka watanzania kulipigia kura bonde la Ngorongoro kuwa moja ya maajabu saba ya Afrika na pia kujenga tabia ya kutembelea vivutio vya utalii vya ndani.
Akizungumza mjini Ngorongoro, Diamond ambaye alikuwa huko kujionea bonde hilo ambalo ni la kipekee ulimwenguni, amesema hakuwahi kufikiria kwamba kuna sehemu nzuri ambayo hata watanzania wanaweza kwenda kutembea na kujionea vivutio vilivyopo.
"Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, lakini kwa kweli nimeshangazwa na jinsi palivyo pazuri, wanyama, mito ambayo inapita huku chini, mi huwa naona kwenye televisheni tu katika kile kipindi cha National Geography cha DSTV lakini sikujua kama mambo haya yapo kweli kwetu.
"Nawaomba watanzania wenzangu waweze kutembelea Ngorongoro na vivutio vyetu vya utalii kwa sababu kuna mengi ya kujifunza, leo kama isingekuwa Afrika sidhani kama kungekuwa na kipindi kama National Geography, na gharama za kuja huku si kubwa, hatupaswi kuogopa, hivi ni vitu ambavyo vinawezekana kabisa suala ni kujipanga," amesema.
Amesema wenzetu kutoka Ulaya wamekuwa wakijipanga kuweza kutembelea sehemu Fulani jam bo ambalo linawafanya waweze kutembelea nchi nyingi kufanya utalii.
"Pamoja na kuja kupunguza mawazo lakini sehemu kama hii inasaidia kuelemisha, mwito wangu kwa watanzania wenzangu, mashule hata vyuo waweze kuja hapa, inakuwa rahisi zaidi kumfundisha mtoto kuhusu Simba, Twiga, au bonde la Ngorongoro kwa kumuonyesha hiki kiko hivi, nadhani kama watoto watakuwa wanasoma kwa vitendo hawawezi kushindwa mitihani yao kwa sababu kumbukumbu inabaki kichwani kwa kile walichokiona," amesema.
Msanii huyo alikwenda Ngorongoro baada ya kumalizika kwa tamasha la Fiesta ambapo alikuwa mmoja wasanii waliofanya vizuri. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ilimualika Diamond huko. Ngorongoro ni moja kati ya vivutio vya Tanzania vinavyotakiwa kupigiwa kuingia katika maajabu saba ya Afrika



IMG_0369.JPG

IMG_0229.JPG

IMG_0044.JPG

IMG_0589.JPG


IMG_0145.JPG


IMG_0415.JPG


IMG_0608.JPG
 
Ni vizuri ila jamani picha ya sita angalia anapiga ile diamond kama ya jay z sema kwa kificho
Hata mm pia nitaenda maana ndio mbuga pekee imebakia na kilimanjaro

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
ngoshwe

Ukiona mtu anatumia NGUVU nyingi KUANDIKA huku ametoa ulimi nje .... nafikiri kuna tatizo la kutokupitia madarasa mengi!

Alafu hapo anaandika Jina lake TU kwenye kitabu cha wageni!

Hivi huyu jamaa ameishia Darasa la Ngapi?

 
Sasa huyo si limbukeni?
Kwani anajua kwamba kavaa dinner suit?
Juzi tu alikuwa akiflassh mpododo kama hana akili nzuri.

Ndo mambo ya kuiga bila kusoma au kuelewa hayo.
 
Tatizo ni mifumo tunayoitumikia.Huyu Kijana hajapata miongozo sahihi ili kuweza fikia kilele cha mafanikio.Hana meneja mwenye utimamu kabisa
 
wakiambiwa wawaulize wenye fani zao wanaona ni ujinga,ndo mana anweza kuvua pichu jukwaani since hajui inamchora yeye ni nani,sasa hili la dinner suit mbugani na lenywe mh!
 
duh dinner sut mbugan? Mie nimefanya tour kibao mbugan tarangire, manyara, kinapa cjaona watalii wakipiga suti, labda ni kwa ajil ya tangazo bt hajawa realistic!
 
Umeona ehh suti mbugani huyu dogo hajijui
duh dinner sut mbugan? Mie nimefanya tour kibao mbugan tarangire, manyara, kinapa cjaona watalii wakipiga suti, labda ni kwa ajil ya tangazo bt hajawa realistic!
 
Back
Top Bottom